Je, Ni lazima kumpa mpenzi wako pesa kila akija nyumbani kwako?

Je, Ni lazima kumpa mpenzi wako pesa kila akija nyumbani kwako?

yuda75

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2020
Posts
520
Reaction score
1,385
Habarini wadau wana JF

Je, kunaulazima wa kumpa mpenzi wako pesa kila akija nyumbani kwako? Maana inakuwa kama umemnunua vile ninavyoona maana muda wa kuondoka wanakodoa macho kweli.

Mbona wanaume wakienda kwa wapenzi wao wa kike hamtupi nauli? Au ndo mwanaume utakula kwa jasho maana mbinguni tutaenda tumechoka sana.
 
Duuuuh! We jamaa haupo serious aseeee. Unataka ukienda kwa mwanamke wako akupe nauli kama wewe unavyompa yeye akija kwako? Really!!

Labda itokee yeye anakuhitaji uende kwake halafu huna hela ukamwambia kisha yeye akuambie nenda tu nauli atakulipia hapo walau kidogo inaleta maana, vinginevyo mwanaume pambana uwe na hela, la utadharaulika sana.
 
Maisha sio pie kwamba Ni 3.14..
Hamnaga formula kila mmoja abebe msalaba wake
 
You just made me laugh.

Hahahahhahaha mueleze na yeye ukienda kwake unataka nauli.
 
Yaani wanaume wa siku hizi sijui mkoje, unapata muda wa kujiuliza swali kama hilo? Huna haja ya kua na mahusiano utatesa tu watoto wa watu.
 
Ila kiukweli inazingua sana hii situation,maana anakuja kwangu sio kwamba ni barabarani tunakutana then kila akiondoka nimpatie pesa sasa si ni kama nanunua penzi.
 
Na ukienda kwake unatakiwa uache hela ya sabuni na chakula
 
Duuuuh! We jamaa haupo serious aseeee. Unataka ukienda kwa mwanamke wako akupe nauli kama wewe unavyompa yeye akija kwako? Really!!

Labda itokee yeye anakuhitaji uende kwake halafu huna hela ukamwambia kisha yeye akuambie nenda tu nauli atakulipia hapo walau kidogo inaleta maana, vinginevyo mwanaume pambana uwe na hela, la utadharaulika sana
Hivi vitu ukifuatilia kwa makini na ukafanya utafiti haswaa, conclusion inakuja mwanaume unatakiwa uwe na hela hakuna namna nyingine yaani.
 
Si tulishakubaliana kuwa wanawake wote wanajiuza, basi tafuta pesa bwa’mdogo.
 
Ndo uanaume huo mkuu, mwanaume majukumu

Au unadhani kutia tu
 
Back
Top Bottom