Je ni lini Tanzania itaweza kurusha satellite angani?

siku ccm itakapo toka madarakani...

kama sivyo, basi KATIBA ya nchi hii, itakapo fanyiwa marekebisho....
 
Satellites sio mchezo mchezo, kama mnavyodhani huwezi miliki sate alafu silaha unanunua, huko juu watu wanavyogombania viwanja utadhani wapo ardhini.
 
Kila kitu kinawezekana cha msingi ni mikakati ya kufanikisha hiyo nia.
 
Una mawazo mazuri ila viongozi hawawazi ivo na hawashauriki sibiri wapite uje tena na hoja kama hii,,
 
Kutengeneza calculator tu tumeshindwa sembuse satellite hyo

OvA
 
Tutaweza atakapokufa yohana mvinyo.
 
Sidhani kwamba Kurusha satellite ndio kigezo cha maendeleo, tuangalie priorities zetu zitakazotuwezesha kupiga hatua kimaendeleo. Maana najua wenzetu walipitia hatua kadhaa za maandalizi mpaka wakafika hapo walipo, tufanye kazi kwa bidii na tuwe tayari kuumia katika harakati za kufika huko.......sio lelemama.
 
Dawa mahospitalini ni shida, halafu mnakuwa na mawazo ya kurusha sattelait....

Ngoja trafic waendelee kukusanya hela zikifika tutairusha
 
Umeongea kweli mkuu, lakini Tanzania ina watu milioni 50, hawa watu wote wote tukiamua kugawana majukumu, hatuna sababu ya kusubiri, wanasiasa wafanye kazi yao kuhakikisha kuna haki na uwajibikaji, wanasayansi wafanye kazi zao kwa weledi, kujituma na ubunifu wa hali ya juu, wanaotaka kuunda satelites waunde, wanaotaka kuunda magari, meli, matrekta wote wafanye hivyo, mwisho wa siku tutajikuta tumekuwa kama Wenzetu walioendelea. Tusiogope kuota ndoto za mafanikio kwa sababu tu kuna watu watatuona mahayawani! Bila hiyo tutajikuta kila mtu anawaza kubeti, na mambo mengine yasiyokuwa ya msingi kwa taifa letu.
 
Katika umiliki wa anga kuna mipaka na vibali, sasa kuvipata hivyo vibali peke yake ni mtihani mkubwa maana kuna vibali vya kimataifa na vya kitaifa kwamba unaweza kupewa kibali ndani ya anga lako tu basi na sio anga la kimataifa kama marekani, japani, urusi na china hayo mataifa yana satellite katika anga za kimataifa ndio maana unaona wanabishana kuhusu nyuklia maana wanajua zilipo

Sasa nchi ulizozitaja kaka ni anga la kitaifa tu sio kimataifa maana hawawezi kukubali kimataifa maana huenda ukawa unatumiwa na maadui zao kupata habari zao hivyo wanakuwa na vikwazo ili usiweze kufikia hapo.

Lakini kuna mataifa kama Canada, chile nk wamejiunga kwenye satellite ya marekani ambapo wako chini ya uongozi wa marekani kupata habari za nchi zao
Hivyo TZ kama ikitaka inaweza kurusha kwenye anga la kitaifa tu hiyo inawezekana kama ambayo iko ghana au la sivyo ikaomba kuungwa kwa marekani japo ni ngumu maana tunaukaribu na maadui wa marekani hivyo hatutaaminika

Pointi ya kuwasomesha watu wetu nje ya nchi ili kuwa na wataalamu n pointi kubwa sana yenye mashiko makubwa sana na hilo viongozi wetu hawajaligundua

Satellite ni kitu cha muhimu sana ingetrack hata mienendo ya waliomshambulia lissu
Ingesaidia kujua madini na mafuta yako wapi, miamba, baharini kama kuna nyambizi zinaingia kinyemela au meli, mawasiliano nk yaani inasaidia sana

Mwaka 2014 kulitokea wachimba madini kufa kwenye migodi yaani walifukiwa na kifusi
Lakini satellite iliwaonyesha walipo na kuwaokoa

Tanzania bado sana tuwaze tu maisha haya haya ya kuwafuatilia wenye malengo na nchi ili wauwawe

Kama wasomi wananyanyasika na wanafunzi wanaonewa ni lini tutakaa sawa? Mawazo ya wenye maono yanafukiwa, sauti ya mwenye maono inazimwa, jitihada za wazalendo zinabomolewa
Bora ulale tu ndugu waza kula na kuvaa tu
 
Dawa mahospitalini ni shida, halafu mnakuwa na mawazo ya kurusha sattelait....

Ngoja trafic waendelee kukusanya hela zikifika tutairusha
Kwa hapa tulipo fika teknolojia na uchumi ni kama kuku na yai, kipi kinaanza na kipi kinafuata, usipokuwa dawa hospitali, afya itakuwa mashakani na huwezi kuwa productive, lakini pia usipokuwa na hizo teknolojia huo ichumi wa kukuwezesha kununua dawa pia ni shida kuipata. Lakini kwa nini tusigawane majumu serikali ikusanye kodi na kutoa huduma, wananchi tufanye kazi ya kuibua na kubuni teknolojia na kuanzisha viwanda, hii siyo kazi ya serilkali, kwa kuwa serikali inaongozwa zaidi na mahitaji ya kisiasa, hata hivyo hao wanasiasa wanatoka miongoni mwetu sisi wenyewe, tunachowaza sisi ndivyo hivyohivyo na wao wanawaza. Teknolojia mbalimbali zinazotamba duniani ni kazi za watu binafsi na si serikali japo serikali huchangia kuziendeleza kwa manifaa ya watu wao. Watanzania tunaweza tukiamua.
 
Umefafanua vizuri sana kiongozi. Mi nadhani kumiliki satelite au kuanza kusomesha watoto wetu nje au kuanza tafiti za maswala ya anga si anasa, kuna faida nyingi tunaweza kupata ili kutuletea maendeleo katika nchi yetu .
 
mkuu ngoja tuwe na Radar za kutosha kwa ajili ya usafiri wa anga na maswala ya kijeshi
 
Bado malaria na kipindupindu vinatutoa jasho unataka turushe hyo kitu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…