Mataifa mengi hususani Africa yameanza kwa kasi urushaji wa Satellite angani katika karne hii kwa kurusha wenyewe au kushirikiana na mataifa kama Japan, Russia, Marekani n.k. Dunia ya sasa matumizi ya satellite ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi husika asa kwenye sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii.
Matumzi ya satellite yanasaidia kuchukua taarifa za Duniani kwenye maswala ya uboreshaji wa kilimo, kijeshi, uchaguzi, afya, hali ya hewa na pia kupata taarifa kwa haraka zinazohusu vimbunga na matetemeko ili mamlaka zilizopo nchi hizo kutoa tahadhari za majanga kabla ya kutokea au serikali kujipanga kwa ajili ya kuchukua tahadhari.
Nchi za Africa ambazo zimeweza kurusha Satelite angani na matumizi yake ni kama ifuatavyo;_
· Misri
Misri wana satellite kama EgyptSat 1 na EgyptSat 2 ambazo wanazitumia kwa matumizi mbalimbali kwa ajili ya kuleta tija kwenye shughuli zao za uchumi. Mwaka huu 2017 wanapanga kurusha Satelite ya DesertSat kwa ajili ya ulinzi na usiamimizi wa maliasili zao ambazo zipo maeneo ya jangwani ili ziweze kuleta tija katika nchi yao.
· Africa Kusini
Afrika kusini wana satellite nyingi ambazo wamerusha toka mwaka 1999-2015. Sateliete ya Kondor-E waliirusha mwaka 2015 huwa wanaitumia kwa ajili ya matumizi ya kijeshi na Satelite nyingne nyingi kama SUNSAT, SumbandilaSat kwa ajili ya matumizi mbalimbali yanayoleta tija kwenye taifa lao n.k
· Morocco
Morocco pia wana satellite mbalimbali pia ifikapo Novemba 2017 watarusha satellite yao nyingine ambayo itatumika kwa shughuli za kijamii na kijeshi ambapo wametumia takribani Euro 500 Million kutaka kufanikisha hilo .
· Algeria
Algeria nao walianza tafiti na hatua za urushaji wa satellite toka miaka ya 2002. Algeria wana satellite zao kama Alsat-1B ambayo inatuamika kwa ajili ya uchukuaji taarifa katika maswala ya kilimo na taarifa za majanga kama vimbunga na matetemeko.
Alsat-2A wanaitumia kwa ajili ya upigaji picha za anga ambazo zinazotumika kwenye taasisi zao kama za kilimo, upimaji ardhi na mamlaka ya hali ya hewa.
· Nijeria
Wanaijeria wanazitumia sana Satellite zao kama SatX na Sat 2 ambazo zipo angani kwa ajili ya kufanya uangalizi wa vyazo vya mafuta kule Niger Delta, chaguzi mbalimbali kwa ajili ya ubainishaji wapiga kura na shughuri za kiusalama na kijeshi wakati wa kutafuta maficho ya Boko Haram pamoja na utafutaji wa watoto 273 waliotekwa kule Chibok mwaka 2014 zilitumika sana.
· Ghana
Mwaka huu 2017 Ghana wamerusha ya kwao inaitwa GhanaSat-1, ni satellite ndogo kabisa na ni satellite ya kwanza kurushwa nchini Ghana wakishirikiana na Mamalaka ya anga ya Japani JAXA (Japanese Aerospace Exploration Agency) imewaghalimu takribani Dola 50,000/=, wanaitumia kwa ajili ya upigaji wa picha za anga nchini Ghana.
MASWALI YANGU
Je Tanzania ina mikakati gani kuhusu au wazo la kurusha satellite angani kwa ajili ya matumizi kijamii na kiuchumi ili kuliletea tija Taifa letu ?
Je maproffesa wetu wanajipanga vipi kufanikisha hili?
Je Serikali inaweza kuweka bajeti ya kusomesha wadogo zetu kwenye Sayansi ya anga ili kuleta tija ya kufanikisha ndoto yetu ya kurusha hata satellite moja ndogo kama waliorusha wenzetu wa Ghana mwaka huu 2017 yenye Launch mass ya 1 Kilogramu(Kg)?
Je kuna fungu lolote huwa linatengwa kwa ajili ya tafiti za sayansi asa za anga ?
Klementos- Jamii Forum