nguzi wa kitaalamu
unaonyesha kwamba hakuna madhara kwa
mwanamke kuendelea kumnyonyesha mtoto
mchanga iwapo atajikuta amepata ujauzito.
Hayo yamebainika wakati uchunguzi mwingine
unaonyesha kwamba asilimia 86 ya vifo vya watoto,
vikiwamo vya utoaji mimba, vinasababishwa na
wanawake wanaokwepa kulea ujauzito au
kuendelea kunyonyesha kwa fikra potofu kuwa
maziwa yamechafuka.
Hayo yamesemwa na Daktari Bingwa wa Magonjwa
ya Wanawake wa Chama cha Madaktari Wanawake
Tanzania (Mewata), Dk Caroline Mayengo kwenye
mahojiano na gazeti hili.
Hakuna madhara yoyote kwa mama mjamzito
kuendelea kunyonyesha. Mtoto aliyeko tumboni na
mtoto mwingine ambaye bado ananyonya
wataendelea kukua vizuri, alisema.
Alifafanua kuwa, iwapo mwanamke yeyote atabaini
amepata ujauzito wakati akiwa bado ana mtoto
mchanga ataendelea kumnyonyesha hadi mimba
itakapofikia umri wa miezi saba.
Ila ameonya kuwa mwanamke anayenyonyesha
huku akiwa ni mjamzito anapaswa kutunzwa vizuri
zaidi kwa kupatiwa vyakula bora vya kutosha ili
kujitunza binafsi na watoto anaowalea.
Mtoto asiachishwe kunyonyeshwa kwa sababu
mama ni mjamzito
Hali ya utapiamlo ya mama
ndiyo inaweza kumwathiri mtoto lakini kama
anapata chakula cha kutosha hakuna madhara,
alisema Dk Mayengo.
Kuhusu vyakula, alisema mama mjamzito anapaswa
kula vyakula vyote muhimu vikiwamo vya vitamini,
madini na vya protini kwa ajili ya kujenga mwili na
madini mbalimbali mwilini.
Alisema kitaalamu inashauriwa mtoto mmoja
anapozaliwa hadi kupata mimba ya mtoto wa pili
angalau wapishane kwa miaka miwili.
Kama mama akibeba mimba nyingine chini ya
miaka miaka miwili(care)utunzaji wa mtoto
mwingine unakuwa si kubwa sana na ukiangalia
watoto wanaokufa utakuta mama zao wana watoto
wengine wachanga,alisema.
Alisema kumekuwa na kupishana kwa watoto
ambako hakuendani na taratibu za kiafya hivyo
alishauri watu kutumia huduma za uzazi wa mpango
ili kutoa nafasi kati ya mtoto mmoja hadi mwingine.
Hata hivyo alisema baadhi ya watu wamekuwa
wakieneza mitazamo hasi juu ya uzazi wa mpango
wakati ukweli ni kwamba manufaa ni mengi.
1 | 2 Next Page»
Je, sababu hizi zinatosha kuiangusha
Ukawa 2015?
1 comment 3 days ago
Avat revocatus Jibu ya swali hili ni
HAPANA kwa sababu Viongozi wa
vyama vya siasa wamethubutu na
wameunganishwa kwa jambo
MAONI: Mradi Vitambulisho vya Kura
unatia shaka - Maoni -
4 comments 3 days ago
Avat Mzalendo Hongera mwariri kwa
kuthubutu. Ila Mwariri hakutupa
mifano wa nchi ambazo zilitumbukia
katika matatizo kwa kutumia BVR
BRAZIL 2014: Mambo sita
yatakayokushangaza - Michezo -
2 comments 3 days ago
Avat Dennis Ogutu Hii ni hali ambayo
Watanzania waige.
Bajeti Kuu yapita gizani, Mkuya atema
cheche
4 comments 3 days ago
Avat Dennis Ogutu Sawa kabisa Waziri
waFedha inabidi watu watozwe kodi
ALSO ON MWANANCHI SITE
0 Comments Mwananchi Site Login d
Sort by Best Share ⤤
Be the first to comment.
WHAT'S THIS?
Subscribe ✉ Add Disqus to your site d
Favorite ★
Kp Mei Kipanya
April Kp Machi
powered by Visit worldcup
site
BRAZIL 2014: Algeria yapania kulipa
kisasi 1982
Wanachama Simba chali
Maximo amleta Coutinho Yanga
MAONI: Tusipokuwa makini utamaduni
utapotea
UKATILI: Baba abaka bintiye,
amwambukiza Ukimwi
Waziri wa Fedha Zanzibar amshikia Raza
bango la kodi
Dar hatarini kwa unga wa lishe, visima vya
maji
Watumiaji wa huduma za kibenki
waonywa
USAFIRI: Sumatra yaiamuru Uda
kushusha nauli
Dk Salim apongezwa
Vita ya Werema, Kafulila yakolea
Dk Salim: Sina mpango na urais 2015
Werema nusura ampige Kafulila
Mtawa aagwa, dereva asimulia
Msekwa atoboa siri ya CCM
kungangania serikali mbili
Ada vyuo vya ualimu juu
Katibu: Bila Ukawa hakuna Katiba Mpya
Mabilioni yapelekwa nchini India
Wanachama 34 CUF wawakataa Seif,
Lipumba
Kisumo: Baraza la Mapinduzi Zbar
limeuawa kimyakimya
MVUTANO: Werema, Maswi, Kafulila
ngoma nzito
Kp Juni
Email Privacy Policy Wasiliana nasi RSS
MCL Blog | Daily Nation | NTV | Business Daily |
The East African | Daily Monitor | KFM |
Mwanaspoti | The Citizen | Nation Media Group
Juni 28, 2014
false
false