abdulhamis
JF-Expert Member
- Aug 2, 2019
- 1,436
- 2,296
Nadhani 90% ya ardhi Tz haijapimwa, what do you say?Zifuatazo ni faida chache za kumiliki kiwanja kilichopimwa na kusajiliwa;
1. Ni rahisi kuwekwa dhamana ya mkopo (mortgage). Hii ni sababu kiwanja kilichosajiliwa huwa na hati inayoonesha mmiliki.Kwa hiyo mabenki hutoa mikopo kwa kushikilia hati ya mkopaji.
2. Ni rahisi kuuzika.Kununua kiwanja ni zoezi mtambuka sana. kiwanja kilichosajiliwa hurahisisha zoezi kwani kila kitu kiko kwenye nyaraka na kwa msajili wa hati.Hivyo ni rahisi kuepuka utapeli ukilinganisha na kiwanja ambacho hakijapimwa na kusajiliwa.
3. Kiwanja kilichosajiliwa (chenye hati) ni rahisi kuonesha mmiliki halali kuliko kile kisichosajiliwa.
4. Kiwanja chenye hati hupunguza migogoro ya ardhi.Si rahisi sana kutokea mgogoro wa umiliki kwa kiwanja kilichopimwa kama kile ambacho hakijapimwa.
5. Kiwanja kilichopimwa na kusajiliwa hupunguza ujenzi holela .Hii ni Kwa sababu kila mwenye kiwanja hujenga Kwa kufuata ramani ya kiwanja chake na hivyo kuimarisha mipango miji.