Je, ni madhara yapi ya kununua kiwanja ambacho hakijapimwa?

abdulhamis

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2019
Posts
1,436
Reaction score
2,296
Habari wadau wa JamiiForums,

Leo naomba Msaada wenu juu ya Elimu ya kiwanja ambacho hakijapimwa. Je, inawezekana kiwanja hicho kikazuiliwa na serikali kisitumike? Na vip imeshawahi kutokea serikali ikachukua kiwanja ambacho umeuziwa na bado hakijapimwa?
 
Ukinunua kiwanja hakijapimwa wewe wahi kujenga nyumba tu. Hakutakuwa na shida kabisa.
 
Elimu hiyo kwa watanzania bado hatunayo maaana hata selikali za mitaaa huwa wanakubali mtu kununua au kuuza kiwanja kisichopimwa, na wao wanachukua 10%,nau ukija upande WA migogoro ya ardhi hawa watu wa selikali za mitaaa wanakuwa wahusika wakubwa sanaaaaaa

Sent from my itel S11 using JamiiForums mobile app
 
Zifuatazo ni faida chache za kumiliki kiwanja kilichopimwa na kusajiliwa;

1. Ni rahisi kuwekwa dhamana ya mkopo (mortgage). Hii ni sababu kiwanja kilichosajiliwa huwa na hati inayoonesha mmiliki.Kwa hiyo mabenki hutoa mikopo kwa kushikilia hati ya mkopaji.

2. Ni rahisi kuuzika.Kununua kiwanja ni zoezi mtambuka sana. kiwanja kilichosajiliwa hurahisisha zoezi kwani kila kitu kiko kwenye nyaraka na kwa msajili wa hati.Hivyo ni rahisi kuepuka utapeli ukilinganisha na kiwanja ambacho hakijapimwa na kusajiliwa.

3. Kiwanja kilichosajiliwa (chenye hati) ni rahisi kuonesha mmiliki halali kuliko kile kisichosajiliwa.

4. Kiwanja chenye hati hupunguza migogoro ya ardhi.Si rahisi sana kutokea mgogoro wa umiliki kwa kiwanja kilichopimwa kama kile ambacho hakijapimwa.

5. Kiwanja kilichopimwa na kusajiliwa hupunguza ujenzi holela .Hii ni Kwa sababu kila mwenye kiwanja hujenga Kwa kufuata ramani ya kiwanja chake na hivyo kuimarisha mipango miji.
 
Nadhani 90% ya ardhi Tz haijapimwa, what do you say?
 
zifuatazo ni hasara za kununua kiwanja ambacho hakijapimwa.

1. Kuna hatari kubwa ya kununua eneo ambalo siyo la makazi mfano eneo la wazi, eneo la makaburi, soko, barabara. n,k
2. kuna hatari kubwa ya kutapeliwa.
3. Kuna hatari kubwa ya kutumia gharama kubwa sana kulinda hilo eneo lako mfano kukitokea kuna mtu mwingine analidai hilo eneo kuwa ni lake itabidi mpelekane mahakamani na huko lazima uingie gharama kubwa sana kwa kumlipa wakili ili akutetee katika mgogoro huo.
 
Back
Top Bottom