Je, ni manukato (perfume) gani yanafaa zaidi kwa hali ya hewa ya joto sana?

Je, ni manukato (perfume) gani yanafaa zaidi kwa hali ya hewa ya joto sana?

Superficial

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2023
Posts
232
Reaction score
471
Ninaishi katika jiji lenye joto kali na halijoto hufikia 35°c kwa urahisi kwa hivyo karibu harufu yoyote ile huhisi kuudhi. Je, ni perfume gani inayoweza kuburudisha hisia hiyo?

Kwasababu kwa ninavyofahamu kila perfume hutengenezwa kulingana na hali ya hewa la eneo,sasa juzi nilijichanganya kuchukua perfume flani bana (siwezi kuitaja kwasababu inapendwa na wengi) ,kumbe ule mzigo ni unafaa zaidi katika mazingira ya baridi flani ivi.

Nashangaa nashuka zangu kwenye AC na ile scent yangu ya bei kidogo inapotea,nikaja kutafuta zaidi taarifa kumbe kuna perfume hutakiwi zichukua kutokana na mazingira unayoishi🙌.
Basi kwa wataalam wa perfumes nahitaji ufafanuzi kwa perfumes ambazo zinaweza kidhi hali ya hewa ya jiji la daslaam

Over ,nawasilisha.
NB;Msinisumbue kujua jina la perfume 😂,nyie endeleeni kuyakanyaga tu.
 
Back
Top Bottom