"MeruA jipange tu uende moja kwa moja sioni kama kuna ulazima wa kutoa mahari nusu"
Nilifika kazini kwake jioni ya Ijumaa,nilienda kumpa taarifa juu ya ugeni wetu,nilitaka amtaarifu baba yake kuwa kesho(Jumamosi) nitafika nyumbani kwao nikiwa nimeambatana na washenga wangu.
Nilikuwa naenda kujitamburisha,pia nilitaka tuelewane kabisa juu ya mahari na nilipanga nibebe kiasi cha pesa ili tukishaelewana nitoe mahari nusu na nusu nyingine nimalizie mwezi February 2022.
Alinikubalia,nikaandaa watu wangu,kesho yake (siku ya tukio) akanipigia simu na kunieleza hayo maneno hapo juu kwamba haoni haja ya mimi kwenda kujitamburisha,na kama ni swala la mahari nitume tu washenga waende wakaelewane,sasa kama mahari niliyonayo haijakamilika ni heri niahirishe nijipange siku nikikamilisha basi niende moja kwa moja.
Nilimkubalia,nikawapigia simu washenga wangu kuwajulisha kuwa zoezi limesogezwa mbele mpaka siku litakapotajwa tena.
Nilijisikia kuwa disappointed sana,maana nilikuwa na vibe kama lote,na sikutaka kukaa na ile hela maana nina majukumu mengi nilijua itaenda kwenye kutatua changamoto zingine za kifamilia.
Nilipanga kubeba laki 6,in case wakisema 1.5M nitaitanguliza hiyo mia 600k
Wakikubali kula 1M ningewapa 500k.
Basi wazo la kuoa 2021 nikawa nimeliondoa kabisa kichwani,juzikati hapo nikapata kabinti kamoja kakiislamu,binti mdogo tu 22yrs,kana mipango sana,kanajistiri sana,ni kapisi kali sana,kanatokea kwenye familia ya chini sana (kama yangu)
Nilipokatongoza hatua ya kwanza kalisema hakapo tayari kuingia kwenye mahusiano yasiyo na malengo,kama kweli nimempenda basi anipeleke nyumbani kwao akanitamburishe,then nimpeleke kwetu nikamtamburishe kisha ndiyo turudi kupanga mipango ya kuishi pamoja.
Yule binti bwana ana mipango yaani ukiongea naye huwezi amini kama ni 22yrs
Mvua imenyesha tu akanishawishi tulime hata ekari chache za chakula cha familia yetu,jana na leo tulikuwa tunalimiwa na ng'ombe,tumeshinda tunapanda pamoja.
MeruA kama mke nimepata,Jumamosi ijayo nimemwambia anipeleke kwao akanitamburishe.
Kama kawaida yangu naenda na kiasi cha hela kabisa najua ndugu zangu waislamu hawana mahari kubwa,laki tatu zangu zitatosha kabisa kumaliza mchezo.
Huyu mwanamke aliyeniwekea masharti atasikia tu mwamba nimevuta jiko,hatokaa aamini macho yake,anajidai kuniwekea masharti mimi??
No no no,nawezaje kumwacha huyu binti ambaye tangu tufahamiane leo tuna mwezi lakini hajawahi kuomba hata 100,isipokuwa mimi tu ndiyo nimekuwa namnunulia vizawadi vya vidogovidogo.
Pengine Mungu katumia njia fulani kuniepusha na matatizo mbeleni akaona aniletee mtu sahihi.
December hii MeruA naoaa.