Wana jamvi poleni na majukumu yenu kwa pamoja. Naomba kufahamishwa au kuelekezwa ni mashirika yapi naweza kupeleka business plan yangu na angalau ikafanyiwa kazi kama si kukubaliwa na kupata ninachohitaji.
Natafuta jinsi ya kuchakata mazao ya kilimo na kuongeza thamani, nimeshafanya baadhi ya hatua lakini ningepata sehem na kupata fund kwa uelewa, uwezo na uzoefu wangu naamini M.Mungu hatonitupa.
Pamoja na michango yenu lakini ninavutiwa sana na taasisi ambazo sio za serikali. Bali taasisi zisizo za kiserikali.
Wasalaam karibuni na mwanzo wa kutoa hoja