SoC02 Je, ni mfumo wa elimu?

SoC02 Je, ni mfumo wa elimu?

Stories of Change - 2022 Competition

betrand44

New Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2
Reaction score
5
Vijana wengi hasa wahitimu wa vyuo vikuu wamejikuta katika wimbi zito la ukosefu wa ajira. Siku ya kuhitimu pamoja na kufanya mahafali huwa ni siku nzuri sana na inayopendeza kwa wahitimu, familia zao pamoja na jamii nzima kwa ujumla. Ila wiki chache baada ya kuhitimu ndipo jamii inapokuja kupata taswira halisi ya kijana aliye kwenda kusoma na kuhitimu.

Kijana ambaye takribani miaka kumi na saba (17) au zaidi amekuwa akiketi mara kwa mara kujibu mitihani kutoka katika mabaraza ya mitihani husika. Mwisho ni kijana asiyekuwa na msaada tena katika jamii.

Katika maandishi ni kijana mwenye sifa kedekede za ufaulu mzuri wa masomo aidha sayansi, sanaa, utabibu na kadhalika. Pia ni kijana mwenye vyeti vilivoshiba alama za juu. Lakini katika fikra ni kijana mwenye wigo na upeo finyu wa mawazo asiyeweza kutatua hata matatizo ndani ya kaya yake. Kwa jamii je ataweza?.

Pindi alipokuwa katika daraja la elimu ya msingi ameweza kujifunza ama kufundishwa vitu vingi ambavyo vinamzunguka yeye mwenyewe pamoja na jamii yake(kwa hakika vyote vilikuwa muhimu sana kwa yeye kuvisoma). Katika daraja hilo la elimu ya msingi amepata kutahiniwa kwa njia ya kukoleza alama katika majawabu kwa kulinganisha na maswali(tujiulize je hakuna aliyoyajibu kwa kufanya bahati nasibu). Basi kufaulu kukawa ni kwake kuanzia hapo.

Elimu ya sekondari nayo vivyo hivyo vitu alivopata darasani vilikuwa ni vya uhalisia kabisa. Kwa mfano elimu ya sayansi kwa masomo kama fizikia, kemia pamoja na baiolojia. Lakini kijana huyu huyu aliyetoka kutahiniwa kwa njia ya kukoleza alama katika majawabu ndipo anakutana misamiati mipya inayohitaji namna ya kukariri kwa hali ya juu. Hivyo ili kuweza kufaulu vizuri ni lazima kukariri maana nzima ya neno mfano tu baiolojia.

Huu ni mfumo mpya kabisa katika saikolojia yake na ni lazima kwenda nayo sambamba kwa kuzingatia kufaulu mitihani ni ulazima ili kwamba apande ngazi nyingine ya mtiririko wa kielimu. Ndipo kwa namna hiyo atafanikiwa kupita na kwenda ngazi nyingine ya kielimu ambapo katika mtiririko ni sekondari ya juu(advanced level).

Basi hatimaye masomo yanapungua kwa idadi isipokua yanaongezeka kwa uzito. Ndipo ufanisi wa kifikra unapohitajika kwa zaidi na hapa ndipo changamoto huanzia na maisha ya elimu kuanza kuonekana ni magumu.

Kwa sababu ni miaka michache(takribani miwili) yenye kuhitaji kujua mambo mengi zaidi kulinganisha na hapo awali ilikuwa miaka mingi(takribani minne) lakini kukariri mambo machache kwa kiasi chake. Hatimaye kutokana na shinikizo la waalimu, familia na jamii kwa ujumla inambidi kijana huyu kuweka bidii kubwa ili kufaulu kwa kuwa ndio daraja la mwisho yeye kuweza kupata kuaminiwa na baraza la elimu.

Kwa kutahiniwa ndani ya masaa kadhaa mambo hayo mengi aliyopewa muda mchache kuweza kuyaelewa. Hivyo atafanikiwa kufaulu ila uelewa utakuwa wa juu juu tu.

Ni mantiki kabisa. Kwa sababu baada ya tu ya kutahiniwa hatokuwa na chachu tena ya kufanya tafakuru ya kitu hata kimojawapo ya vingi alivyosoma. Bali itakuwa ni furaha na nderemo kwake kwa kuweza kuutua mzigo na kuumaliza mwendo salama.

Hatimaye chuo kikuu kinapata mgeni amabaye amefanikiwa kutahiniwa na kuaminiwa na baraza la mitihani yote kwa ngazi zote husika. Tunampata kijana mwenye ndoto za kuwa injinia makenika zilizokuja baada ya kuweza kuchaguliwa katika chuo bora katika kutoa mainjinia bora nchini(ila kiuhalisia ni juhudi zao binafsi).

Kwa kuwa yeye ni ngazi ya astashahada basi mtaala wake hautamruhusu kusoma vitu kwa undani zaidi. kwa maana ya kuvichimba zaidi kwa mantiki ya kuvielewa na kuviweza kiuhalisia.

Hivyo kozi moja tu ya magari(automotive) ataisoma ndani ya miezi nane(8) tu na karakana atakwenda siku thelasini na mbili(32) yaani kwa wiki mara moja tu. Na hatimaye kozi imekwisha na kozi nyingine nayo vivyo hivyo. Kimsingi kuepuka mhitimu mwenye ujuzi na ufanisi mdogo katika kazi ni kwa asilimia chache sana na ndio wengi wanaoulizwa na kusema ajira hakuna.


TUTAJIKWAMUAJE ILI KUEPUKA HAYO YOTE?

Kwa muda mrefu sana taasisi ya elimu imejitahidi kujinasua katika tatizo hili lakini tunaishia kuona tu kwamba katika madaraja ya elimu za juu, sekondari na msingi ufaulu kuongezeka kila mwaka.

Na hicho ndicho kimekuwa kiini macho hasa katika jamii zetu na kushindwa kupambanua kwamba kwanini ajira ziwe chache na kama hazipo au hazitokuwepo basi yatupasa nini kuendelea kutoa watahiniwa kila mwaka.

Ni wazi kabisa jambo hili linapolekea familia husika kuteseka kiuchumi, jamii na taifa kwa ujumla katika upande huo.

Serikali imeishia kubadili mitaala tu na imeshindwa kujiuliza kwamba kama mitaala inabadilika je namna ya ufundishwaji wa hiyo mitaala inabadilika pia?. Ukweli ni kwamba mitaala inabadilika lakini namna ya ufundishwaji ni ule ule kabisa. Hivyo hakuna mantiki ya mabadiliko.

Hii ni kutokana kwamba hakuna ujuzi mpya wa kufundisha kwa ufanisi na wa kuleta tija kwa maana ya kwamba kumuandaa mtoto ama msomi ataeweza kutatua changamoto zilizopo katika jamii kupitia ujuzi ule ule aliyofundishwa akiwa darasani katika mtaala ule ule uliobadilishwa. Hivyo badala ya mtaala kubadilishwa namna ya ufundishaji kwa kupitia wafundishaji ndivyo vibadilike.

Hivyo ukipatikana ujuzi(ambapo upo) wa kumwelezea mtoto au mwanafunzi umuhimu wa kile anachokisoma ukiachana na kwa ajili ya kujibia mtihani na shule kupata sifa. Bali kumuandaa mwanafunzi ambaye mwisho wa siku kwa kuwa kile alichokisoma darasani kina umuhimu katika utatuzi wa changamoto zilizopo katika jamii basi yeye mwenyewe apate kutambua umuhimu wa kukitambua na kukitoa katika karatasi na kukiweka katika vitendo.

Hatimaye jamii itapata kunufaika na taifa kwa ujumla. Hapo ndipo tutaliona tatizo la ukosefu wa ajira likitokomea kabisa kwa kuwa fursa ni nyingi isipokuwa mawazo ya kuchanganua izo fursa ndio yanayokosekana na huu utakuwa ushindi kwetu.

Imeandikwa na: ALOYCE ROBERT BETRAND.
Simu: +255682412066.
 
Upvote 5
Mkuu,

Tatizo sio sayansi na ugumu wake wa kukariri terminologies sababu hata somo la Kingereza kwa masomo yote Form one ni changamoto hasa kwa vijana wanaosoma shule za serikali.....

Binafsi nadhani tutoke kwenye mfumo wa elimu ya kukariri na kuelekea mfumo wa kuelewa na strategy mojawapo ni kuweka lugha moja ya kufundishia....kuanzia msingi,secondary mpaka chuoni...kwa shule zote private na za serikali.

Second, ni serikali kuinvest kwenye elimu,kuanzia maslahi ya walimu, vifaa,maabara ya kisasa etc.

Suala la ajira litapungua kwa vijana kusoma vitu relevant, namaanisha vitu vinaakisi mazingira yetu,mfano kwa engineer asome vitu sio general au kwa vitabu vya kizungu bali kwa mazingira yetu, sio engineer anakariri mavitabu ya nje anatengeneza daraja mvua ikija linavunjika,angesoma kwa mazingira yetu angejua miundo mbinu inavyokuwa affected na matukio...hivyo angetumia utaalamu wake kujenga daraja linalo withstand hayo matatizo....kila mtu kwa kada yake akichagizwa vizuri kusoma kwenye mazingira yetu watajua challenges na fursa zilizopo hivyo kuweza kujiajiri ama kuajiriwa.
 
Nashukuru sana Anita kwa kuongezea hoja hapo. Katika hoja niliotoa mimi naweza kunukuu "Ukweli ni kwamba mitaala inabadilika lakini namna ya ufundishwaji ni ule ule kabisa. Hivyo hakuna mantiki ya mabadiliko.

Hii ni kutokana kwamba hakuna ujuzi mpya wa kufundisha kwa ufanisi na wa kuleta tija kwa maana ya kwamba kumuandaa mtoto ama msomi ataeweza kutatua changamoto zilizopo katika jamii kupitia ujuzi ule ule aliyofundishwa akiwa darasani katika mtaala ule ule uliobadilishwa". Hivyo ni hoja inayo landana na uliyotoa niki nukuu "Binafsi nadhani tutoke kwenye mfumo wa elimu ya kukariri na kuelekea mfumo wa kuelewa" na pia nilitolea mfano tu katika nanja ya sayansi zaidi isipokua zipo nyanja nyingi za kielimu. Na swala la kubadilishwa kwa lugha, ndio ni hoja nzuri ila binafsi naona pia itakumbana na changamoto zake tu mfano serikali itahitaji kutafuta wataalamu wake binafsi wa kutengeneza vitabu vitavyo endana na umahiri kidunia(world wide competence) hivyo itahitaji kuanza upya. Pia hoja ya lugha ni nzuri sana katika nyanja zote isipokua itahitajika nguvu kubwa katika kuanza upya(japo itawezekana tukiamua). Ila gharama ndio kitu kikubwa kitakachopewa kipaumbele japo mafanikio yatakuwa makubwa yenye kuhitaji muda wa kutosha. Nimalize kwa kusema ajira zipo sana na kama upo ukifuatilia(updates) utaona zipo isipokua wanaoomba hizo ajira ndio hawana umahiri(competence) wa kutosha hivyo ni ngumu kupata ajira hizo. Ahsanteh, karibu sana
 
Nashukuru sana Anita kwa kuongezea hoja hapo. Katika hoja niliotoa mimi naweza kunukuu "Ukweli ni kwamba mitaala inabadilika lakini namna ya ufundishwaji ni ule ule kabisa. Hivyo hakuna mantiki ya mabadiliko.

Hii ni kutokana kwamba hakuna ujuzi mpya wa kufundisha kwa ufanisi na wa kuleta tija kwa maana ya kwamba kumuandaa mtoto ama msomi ataeweza kutatua changamoto zilizopo katika jamii kupitia ujuzi ule ule aliyofundishwa akiwa darasani katika mtaala ule ule uliobadilishwa". Hivyo ni hoja inayo landana na uliyotoa niki nukuu "Binafsi nadhani tutoke kwenye mfumo wa elimu ya kukariri na kuelekea mfumo wa kuelewa" na pia nilitolea mfano tu katika nanja ya sayansi zaidi isipokua zipo nyanja nyingi za kielimu. Na swala la kubadilishwa kwa lugha, ndio ni hoja nzuri ila binafsi naona pia itakumbana na changamoto zake tu mfano serikali itahitaji kutafuta wataalamu wake binafsi wa kutengeneza vitabu vitavyo endana na umahiri kidunia(world wide competence) hivyo itahitaji kuanza upya. Pia hoja ya lugha ni nzuri sana katika nyanja zote isipokua itahitajika nguvu kubwa katika kuanza upya(japo itawezekana tukiamua). Ila gharama ndio kitu kikubwa kitakachopewa kipaumbele japo mafanikio yatakuwa makubwa yenye kuhitaji muda wa kutosha. Nimalize kwa kusema ajira zipo sana na kama upo ukifuatilia(updates) utaona zipo isipokua wanaoomba hizo ajira ndio hawana umahiri(competence) wa kutosha hivyo ni ngumu kupata ajira hizo. Ahsanteh, karibu sana
Uko sahihi mkuu
 
Back
Top Bottom