Je, ni Mkoa upi wenye mzunguko mzuri kwa Saloon ya wanawake?

newbeliever

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2015
Posts
248
Reaction score
48
Habari wanajukwaa,

Samahani nauliza ni mkoa upi na maeneo yapi naweza kufungua saloon classic ya wanawake?

Saloon inayotoa huduma zote kuanzia kusuka kawaida, make up, dread n.k?

Natamani/ nina mpango huo ila bado sijajua niende mkoa gani ambao bado haujawa na competition kubwa lakin pia wenye mzunguko mzuri wa pesa kwa biashara hiyo.

Kwa sasa niko mwanza ila naona kuna changamoto ya hii biashara kuwa ya watu wengi, nataka nibadili eneo.

Natanguliza shukrani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Moja ya jambo la kushauri ni utazame wapi Wanawake na Mabinti wanapenda kupendeza (Mikoa mingine Wanawake wamewekeza nguvu kwenye kilimo na ujasiriamali)

Ikiwa Daslam, Arusha, Mwanza na Dodoma wameliteka soko tayari jaribu kusogea Mara au Kagera (Bukoba).

Kila lenye kheri.
 
Mkuu naomba wewe unishauri sasa, kwa Tanzania hii ukiitoa Mwanza kama angelikuwa ni wewe ungefungua hii biashara mkoa gani? I mean kwako wewe ni mkoa upi unafikiri wanawake wanapenda kupendeza zaidi?

Nitashukuru kwa jibu lako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ningelikuwa mimi baada ya kuwepo competition Daslam, Arusha, Dodoma, Mbeya huku nipo Mwanza ningeliweka majeshi yangu Bukoba Municipal kutumia fursa zilizolaliwa na wazawa.

Sababu kubwa ni Ke wa maeneo hayo kupenda Urembo, Ukaribu wa kuamisha biashara na kutumia fursa zilizo wazi.
 
Asante Mkuu, Vip Moshi unapaonaje? Na vip dsm maeneo ya msimbazi? Maana pale ni city center ijapokuwa zipo huduma za saloon pale ila nahisi nyingi zinazofahamika zaidi zipo maeneo ya pemben kama sinza,mwenge etc.

Am just asking Sir

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dar es Salaam au Moshi inawezekana lakini nilichokiangalia ni demand! Uhitaji.

Daslam tayari Wateja wana Saloon zao na soko ni competitive hatari kila pande saloon tena yenye hadhi. Kikubwa kama umejipanga na tayari unazo tactics za kutoa huduma za kipekee unaweza fanikisha.

Same to Moshi tayari soko limeshikwa though nina muda maeneo hayo. Pia hata Tanga ingewezekana lakini culture hauruhusu na tayari watu wamejizolea watu wao. Tabora naona Vyuo vingi na hapo ndio penyewe lakini last year na last month nimeona Saloon zenye hadhi ya kuwa Toronto na sio Tabora.

Kikubwa ni wewe uonavyo pia lakini kama imekuwia vigumu Mwanza usitegemee Dar es Salaam au Arusha.

Ni mawazo yangu lakini waweza changanya na zako
 
Kahama, babat, dom ,karatu,arusha stand ndogo, dsm mwenge ,tegeta, kkoo,kinondon , survery njia ya UDSM competition utakutana nazo tu popote sababu biashara yako sio mpya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kahama, babat, dom ,karatu,arusha stand ndogo, dsm mwenge ,tegeta, kkoo,kinondon , survery njia ya UDSM competition utakutana nazo tu popote sababu biashara yako sio mpya.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ila mkuu kuna competition na competition aisee! Kuna sehemu unakuta wanatoa hizi huduma lakin ukiwaangalia unaona kuna gape flani hiv. Na kuna sehemu ukiwaangalia unakosa nafasi maana kila pembe kuna saloon.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unapoamua kufanya biashara habari za changamoto nilazima ziwepo

Na kupata wateja lzm uwe na huduma nzuri na uwe na utofaut hapo ndo utawateka ( kujifunza kila siku vitu vipya/kwenda na fashion)

Kwa jiji la dar expect kusota angalau mwaka mzima

Japo dar pesa hipo sanaaa


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Yaani wasukuma wakushinde ujanja(competition) halafu ndio uje uwaweze wachaga(Moshi)?

Utapigwa fitna mixer stiff competition na kupotea kwny ramani fasta tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…