Mzee mimi nakatisha usiku mitaa ya Uhuru,mtakuja,Lumumba na mingine kedekede kuna masaluni ya kike mengi na wateja wapo halafu na mengine yanafunguliwa wewe unataka ukimbie....Unajua idadi ya watu wanaopita kwa siku makoroboi mkuu.... Wanawake wengi sana kule na ndio maana wauza nguo za kike wamejazana kule... Kamuulize msafisha kucha tu wa pale anakamata shingapi per day... Sembuse saloon... Wewe unachokosa ni uthubutu halafu unaogopa... Basi nenda mitaa ya kitangiri,pasiasi buzuruga na kwingine coz huko kumetamalaki barbershops tu saluni za kike za kisasa si nyingi... Huko unapotaka kukimbilia kuna ambao wamepanga wapakache waende mji kama mwanza wenye soko,mtapishana tu... Kwan hujawahi pita sehemu ukakuta maduka ya nguo yamepangana tu au ya simu hadi ukajiuliza wanapataje faida ila kajaribu kuwauliza.
My take; Usihame huo mji pamechangamka mno,jaribu kujitanua maeneo ya pembeni kidogo kama unaona maeneo ya city center kuna competition.