Je ni muda muafaka wa sisi kuzikabidhi timu zetu kwa Mabilionea?

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
Baada ya TP Mazembe kuchukua ubingwa wa Klabu Bingwa Africa.. wadau wa michezo nchini wameibuka na kudai sasa ni muda muafaka wa Timu nchini kupigwa bei ili nazo ziweze kama si kufikia mafanikio ya TP Mazembe basi kusogelea.
Jambo la kujiuliza ni Je tunafahamu ni nini kilichopo nyuma ya pazia mpaka TP Mazembe imefika hapo ilipo??.
Ungana nami..

1. TP MAZEMBE = MOISE KATUMBI
Mwaka 2010.. Moise Katumbi akihojiwa na chombo kimojawapo cha habari alinena haya..
"We want to be an elephant in African football, and to achieve it we must acquire all necessary means."

Hebu tuangalie ni kwa jinsi gani Moise Katumbi alivyoanza.. na anavyopambana kutimiza ndoto yake.

Tangu akiwa na miaka 16.. Moise Katumbi alikua hakosi mazoezi wala mechi za timu yake. Furaha yake kuu ilikua ni kuokota mpira uliotoka nje ya uwanja na kumkabidhi mchezaji.. Pia alikua akiact kama Ball Boy.

Baada ya kuonesha mapenzi makubwa kwa timu, kama vile kuisadia timu gharama za usafiri, posho kwa wachezaji n.k.. Mnamo mwaka 1983 [akiwa na miaka 20 tu] alichaguliwa kua Chairman wa timu.

Mwaka 1997 timu yake ilibadili jina na kuanza kutumia TP Mazembe. Zoezi hili liliambatana na kufanya uchaguzi upya.

Ingawa kipindi hicho Moise Katumbi alikua akishi uhamishoni kutokana na kufukuzwa nchini kwake.. alichaguliwa tena kua Mwenyekiti kwa kura nyingi sana.. Na akawa anaiongoza timu akiwa uhamishoni.

Mpaka sasa unaposoma makala hii, Moise Katumbi kaiongoza TP Mazembe kwa miaka 32 mfululizo [tangu mwaka 1983].

2. Uwekezaji wa MOISE KATUMBI ndani ya TP MAZEMBE
Katika moja ya interview zake, Moise Katumbi aliwahi kunena haya..
"I once spent 90 per cent of my time on football, but now that number is more like 35 per cent because of my commitments to governance."

Kauli yake inapigiwa mstari na investment kubwa aliyoifanya na anayoendelea kuifanya katika timu yake.. Baadhi ya hizo investment ni;

1. Kugharamia timu.. ambapo bajeti ya TP Mazembe kwa miaka ya hivi karibuni ni USD 10m [zaidi ya 20B].. na hii ni kwa Kila mwaka.
2. Anaendelea na ujenzi wa Academy.. ambayo itakapokamilika itakua level moja na Academy bora zilizopo Europe.. Interesting thing ni kuwa Mke wake..ndo Mwenyekiti wa hii Academy.. Familia nzima ni mashabiki nguli wa Mazembe.
3. TP Mazembe inamiliki Private Jet mbili.
4. Mwaka 2012 TP Mazembe walizindua uwanja wao binafsi uliogharimu USD 35m [zaidi ya 70B].

NB: Ukidhani mambo yote hayo hapo juu yamefanyika kutokana na mapato ya Timu.. Utakua umekosea... Kwanini?
Mapato ya TP Mazembe kwa mwaka hufikia had USD 15m [zaidi ya 30B].. Hivyo kwa mapato haya huwezi kufanya mambo yote hapo juu.

Kwenu wadau wa Sports..
Nchini Tanzania.. Moise Katumbi wetu ni nani?
1. Moise Katumbi ametumia zaidi ya miaka 30 ya maisha yake duniani kuipigania timu yakeanatumia asilimia tisini ya siku yake.. Na hii ni kwa kuitumikia katika kiwango cha juu.. Je ni nani nchini mwenye uthubutu huo?
2. Miaka 32 ya uongozi wake, haikua rahisi kwani alikutana na vikwazo vingi, lakini alivivuka.. Je kwa Tanzania tumkabidhi dhamana ya kutuvusha salama bila kututelekeza, Moise Katumbi yupi?
3. Moise Katumbi kawekeza karibu robo ya utajiri wake katika timu.. Je Moise Katumbi wa Tanzania mwenye uthubutu wa kufanya hivyo ni nani?.... au mnataka kunitajia "Mfanyabiashara" anayetaka kuinunua timu bora kabisa katika ukanda wa CECAFA kwa 20B? [Huu ni utani].
 
Miaka70 hamjachukua hilo kombe mkiwa na mfumo huo huo.

Why msichange??

Kama hamtaki kumuuzia Mo timu basi mkodishieni kwa miaka 5 msiporidhika chukueni timu yenu.

Timu ina mashabiki milioni zaidi ya 10 lakini bado wachezaji wanadai madeni.
 
Ya Moise Katumbi mwachieni Moise Katumbi na ya Mzee Akilimali mwachieni mzeee Akilimali
 
Miaka70 hamjachukua hilo kombe mkiwa na mfumo huo huo.

Why msichange??

Kama hamtaki kumuuzia Mo timu basi mkodishieni kwa miaka 5 msiporidhika chukueni timu yenu.

Timu ina mashabiki milioni zaidi ya 10 lakini bado wachezaji wanadai madeni.

Mkuu, Mo alikabidhiwa African Lyon ikiwa moja ya timu bora kabisa, huku akitoa ahadi ya kuifanya kua timu bora kabisa katika CECAFA.. Lakini baada ya msimu mmoja.. Timu ilikua hoi bin taabani.. Akaona isiwe tabu, akaipiga bei.

Kama Mo kashindwa kuaminika katika vitu vidogo.. Ataweza vipi kuaminika katika mambo makubwa?
 
Ya Moise Katumbi mwachieni Moise Katumbi na ya Mzee Akilimali mwachieni mzeee Akilimali

Mkuu sina Habari kabisa na ya Multimillionaire Moise Katumbi.. Ila nilichojaribu kukiainisha hapa ni kuwa.. "Usione vyaelea, Jua vimeundwa".. Na si kukurupuka tu.
 

Ilikua timu bora Wapi?

Kwa hiyo hamumtaki mo au hamtaki timu imilikiwe na mtu binafsi?
 

TP Mazembe imeng'ara baada ya soka ya uarabuni kuvurugwa na machafuko ya kisiasa,ila sio kama nabeza investment za Katumbi.
 
Ilikua timu bora Wapi?

Kwa hiyo hamumtaki mo au hamtaki timu imilikiwe na mtu binafsi?

Had timu kua katika VPL.. Inamaana ni bora.. But kwa resources alizokua nazo.. Alikua na kazi ndo sana.. ya kuitransform kutoka good mpaka best.

Si kwamba sipendi timu imilkiwe na mtu binafsi.. La hasha.. Nataka mtu mwenye dhamira ya dhati kama Katumbi.. Hata akisema nataka kuivusha timu yenu.. Tumuone kweli machoni anamaanisha.

Naheshimu sana mchango wake.. Na bado tunauhitaji sana.. Lakini si ndo tumkabidhi timu.
 
Issue sio timu kumilikiwa na mabilionea,bali ni kubadilisha mfumo ambao utaziwezesha hizi klabu kujiongea mapato na sio kutegemea hela za viongozi wajanjawajanja tu.Kuna ubaaishaji mkubwa kwenye soka letu ni aibu kubwa ,watu kama Hans Pope wanajifanya wao ndio miungu sababu mfumo uliopo unawaruhusu kufanya huo upuuzi.Mfano ile issue ya kuuzwa Emanuel Okwi hata haielezeki
 

Unakumbuka sembo ?
 

sikubaliani na wewe.....kwa hoja kabisa

MO wakati anaidhamini samba ...miaka ya mwanzoni mwa 2000 timu ilikuwa na mafanikio...ameondoka...10 years down the line matatizo lukuki

Hatuwezi kuendelea na hawa kina Hanspope sijui dalali sijui rage sijui aveva and so forth....Tumpe mtu mmoja MO afanye kazi...full stop
 
Hata akisema nataka kuivusha timu yenu.. Tumuone kweli machoni anamaanisha.

Aisee .....wewe macho yako peke yako ndio yanaona hawezi kutuvusha?...kwa kifupi ni kuwa MO ni Forbes recognized billionaire na 21 kwa Africa.......Anazo success zake nyingi na failures as well but ni mtu ambaye unajua anaweza kuwekeza pesa na kutotuibia

sasa hao kina Hanspope wako wapuuzi na viongozi wengine kwa miak 80 iliyopita wamefanya nini? Hopelesss,....timu haina hata kiwanja cha mchangani cha mazoezi???? aibuu huna

Umaskini Mbaya sana
 
Mkuu naheshimu muono wako.
Mkuu siyo jicho langu tu ndo linaona hivyo.. Jana Mo katika Mahojiano yake na SALEHJEMBE, baadhi ya maswali aliyoulizwa ni haya;

SALEHJEMBE: Uongozi wa Simba ulikubali kwenda kwenye mabadiliko, ilionekana ni shinikizo la wanachama. Lakini hawakusema wataufanya kwa muda gani, nini ushauri wako hapa?

Mo: Katika barua yangu niliyowaandikia, nimewaomba angalau mchakato uchukue miezi mitatu ili tuingie na kuanza kazi.

SALEHJEMBE: Umesema kuna viongozi hawataki mabadiliko, kina nani hasa?

Mo: Nilisema wanaongozwa na Evans (Aveva), lakini wengi tunafahamiana. Tena ni wachache tu na mmoja nimemwandikia ujumbe kumueleza nashukuru sana kuona ananipinga na hataki mabadiliko.

Hii inaonesha kuna kundi la wanachama hawajaridhika na hili la Mo kukabidhiwa timu, sembo nikiwemo.
 

Hiyo kawaida....sio lazima wote waridhike....wengi wamekubali

Nakufahamu wewe na kwa historia yako humu jukwaani uko kundi lao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…