sembo
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 4,350
- 3,451
Baada ya TP Mazembe kuchukua ubingwa wa Klabu Bingwa Africa.. wadau wa michezo nchini wameibuka na kudai sasa ni muda muafaka wa Timu nchini kupigwa bei ili nazo ziweze kama si kufikia mafanikio ya TP Mazembe basi kusogelea.
Jambo la kujiuliza ni Je tunafahamu ni nini kilichopo nyuma ya pazia mpaka TP Mazembe imefika hapo ilipo??.
Ungana nami..
1. TP MAZEMBE = MOISE KATUMBI
Mwaka 2010.. Moise Katumbi akihojiwa na chombo kimojawapo cha habari alinena haya..
"We want to be an elephant in African football, and to achieve it we must acquire all necessary means."
Hebu tuangalie ni kwa jinsi gani Moise Katumbi alivyoanza.. na anavyopambana kutimiza ndoto yake.
Tangu akiwa na miaka 16.. Moise Katumbi alikua hakosi mazoezi wala mechi za timu yake. Furaha yake kuu ilikua ni kuokota mpira uliotoka nje ya uwanja na kumkabidhi mchezaji.. Pia alikua akiact kama Ball Boy.
Baada ya kuonesha mapenzi makubwa kwa timu, kama vile kuisadia timu gharama za usafiri, posho kwa wachezaji n.k.. Mnamo mwaka 1983 [akiwa na miaka 20 tu] alichaguliwa kua Chairman wa timu.
Mwaka 1997 timu yake ilibadili jina na kuanza kutumia TP Mazembe. Zoezi hili liliambatana na kufanya uchaguzi upya.
Ingawa kipindi hicho Moise Katumbi alikua akishi uhamishoni kutokana na kufukuzwa nchini kwake.. alichaguliwa tena kua Mwenyekiti kwa kura nyingi sana.. Na akawa anaiongoza timu akiwa uhamishoni.
Mpaka sasa unaposoma makala hii, Moise Katumbi kaiongoza TP Mazembe kwa miaka 32 mfululizo [tangu mwaka 1983].
2. Uwekezaji wa MOISE KATUMBI ndani ya TP MAZEMBE
Katika moja ya interview zake, Moise Katumbi aliwahi kunena haya..
"I once spent 90 per cent of my time on football, but now that number is more like 35 per cent because of my commitments to governance."
Kauli yake inapigiwa mstari na investment kubwa aliyoifanya na anayoendelea kuifanya katika timu yake.. Baadhi ya hizo investment ni;
1. Kugharamia timu.. ambapo bajeti ya TP Mazembe kwa miaka ya hivi karibuni ni USD 10m [zaidi ya 20B].. na hii ni kwa Kila mwaka.
2. Anaendelea na ujenzi wa Academy.. ambayo itakapokamilika itakua level moja na Academy bora zilizopo Europe.. Interesting thing ni kuwa Mke wake..ndo Mwenyekiti wa hii Academy.. Familia nzima ni mashabiki nguli wa Mazembe.
3. TP Mazembe inamiliki Private Jet mbili.
4. Mwaka 2012 TP Mazembe walizindua uwanja wao binafsi uliogharimu USD 35m [zaidi ya 70B].
NB: Ukidhani mambo yote hayo hapo juu yamefanyika kutokana na mapato ya Timu.. Utakua umekosea... Kwanini?
Mapato ya TP Mazembe kwa mwaka hufikia had USD 15m [zaidi ya 30B].. Hivyo kwa mapato haya huwezi kufanya mambo yote hapo juu.
Kwenu wadau wa Sports..
Nchini Tanzania.. Moise Katumbi wetu ni nani?
1. Moise Katumbi ametumia zaidi ya miaka 30 ya maisha yake duniani kuipigania timu yakeanatumia asilimia tisini ya siku yake.. Na hii ni kwa kuitumikia katika kiwango cha juu.. Je ni nani nchini mwenye uthubutu huo?
2. Miaka 32 ya uongozi wake, haikua rahisi kwani alikutana na vikwazo vingi, lakini alivivuka.. Je kwa Tanzania tumkabidhi dhamana ya kutuvusha salama bila kututelekeza, Moise Katumbi yupi?
3. Moise Katumbi kawekeza karibu robo ya utajiri wake katika timu.. Je Moise Katumbi wa Tanzania mwenye uthubutu wa kufanya hivyo ni nani?.... au mnataka kunitajia "Mfanyabiashara" anayetaka kuinunua timu bora kabisa katika ukanda wa CECAFA kwa 20B? [Huu ni utani].