Je, ni muhimu kulipa mahari yooooooooooooooooooooooote?

Je, ni muhimu kulipa mahari yooooooooooooooooooooooote?

KIBONGOMKUTI

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2010
Posts
1,425
Reaction score
609
Wanajamvi me nafagilia mila na desturi za Kibantu ambazo ziko bomba,mathalani hii ya kulipa mahari kwa maana ya kutoa shukrani japo kiduchu kwa wazazi/walezi wa mtarajiwa wako (mke). Lakini baadhi ya watu (ndugu na rafiki) niliongea nao kwa uchache wanadai/kushauri kuwa mahari kwa kawaida huwa hailipwi yote ili kulinda na kutunza heshima kwa wazazi/walezi wa mtarajiwa? Wajameni tujuzane katika hili wenye uelewa katika nyaja hizi?
 
Lipa tu yote...

Ila siku nyingine..neno hata likiwa fupi,wasomaji watalielewa tu.. Haina haja ya kulirefusha kama ulivyofanya kwenye heading yako!
 
By Gambachovu " Ila siku nyingine..neno hata likiwa fupi,wasomaji watalielewa tu.. Haina haja ya kulirefusha kama ulivyofanya kwenye heading yako!"

Akhsante sana kwa ushauri wako, utazingatiwa
 
By Nyani Ngabu "Huo upuuzi mimi siufagilii kabisa.

Hhahahah sio upuuzi labda pale ambapo mahari inakuwa mtaji wa Biashara mathalani Mzee anadai Binti yangu bila Milioni kadhaa hatoki. Vinginevyo me naona ni pouwa tu kutoa shukrani
 
Back
Top Bottom