Uchaguzi 2020 Je, ni nani alikuwa nyuma ya biashara ya waunga juhudi? Je, imemlipa ama kala hasara kubwa?

Hii biashara ilikuwa ya Mr. Magufuli na Pole pole huku wakitumia fedha za ofisi ya rais ambazo kwa sasa CAG haruhusiwi kuzikagua.

Sasa, sawa na biashara zingine kwa kweli haikuleta matokeo yaliyokusudiwa na ni hasara kubwa kwa walioiasisi.

But what can they do now, it was the ultimate gamble designed to eliminate the opposition to easily pave the way for the incumbent president to change the constitution to enable him to stay in power indefinitely.
 
Nasubiri maamuzi ya wajumbe WA uchaguzi mkuu WA rais ,wabunge na madiwan tar 28 Oct 2020.maana wajumbe Sikh hiz hawatabirik
 
Mungu awasamehe bure waliounga juhudi..malipo ni hapa hapa duniani na adhabu zingine huwa zimo kwenye kitendo ... Hawakujua walitendalo , ila waliowaingiza mkenge walijua bila kujua ya kesho... Ndo hasara ya kufanya biashara pasipo kufikiri kwa kina.
Kuna UKAKASI katika statement yako.... moja katika nchi huru na haki/uhuru wa Binadamu kufanya chochote anachokiona sawa kwake sioni kosa au kuwashupalia wale waliofanya maamuzi hata kama kwa upeo wetu maamuzi hayo ni ya kipuuzi

Pili unavyosema kufanya biashara (mentality hii ya hata sisi wapiga kura kukubali kwamba siasa, au kuwapa kura wawakilishi wetu watuwakilishe ni biashara na sio utumishi...) ni kwamba tumekubaliana na kuona ni sawa huu upuuzi unaofanyika
 
Ila madalali wamefaidi sana tu aaaaiiisseee! Yaaani mkuu wa mkoa anamnunulia bmw mkewe zawadi ya birthday!!!! Brand New kabsa wanachana nylon kwenye seat
[emoji44][emoji44][emoji44][emoji44][emoji44][emoji848][emoji848][emoji848][emoji2827][emoji2827][emoji2827]
 
Waliobuni mradi wa kununua wapinzani lazima walikuwa ni watu wenye akili ndogo sana. Hawakuwa na uwezo wa kuyaona mambo kwa mbele.

KILICHOPO

Ununuzi wa wapinzani haujaleta matokeo waliyoyatarajia. Kitu ambacho hawakukijua ni kuwa wengi wa walionunuliwa walikuwa viongozi kwa sababu tu wananchi walitaka mabadiliko, na hao viongozi wala hawakuwa sababu ya wananchi kutaka mabadiliko. Walinunua matokeo bila kugusa kisababishi. Uwezekano mkubwa ni kwamba majimbo yote yaliyokuwa ya wapinzani, yatarudi tena upinzani.

Walionunuliwa walikuwa wanajua kuwa wao si chochote ndani ya majimbo yao. Kwao kununuliwa kulikuwa na faida mbili. Moja, watapata fedha. Pili, waliamini mfumo wa demokrasia unafikia mwisho, demokrasia inauawa, hivyo ni vema kuungana na muuaji wa demokrasia ili waendelee kuwepo kwenye siasa bila ya kujali watakuwepo kwenye saisa za mfumo gani. Waliangalia zaidi maslahi binafsi.

MATOKEO

1) Majimbo yaliyokuwa ya upinzani yanarudi tena upinzani

2) Walionunuliwa toka upinzani hawatakuwa wagombea kupitia chama chochote, na Mwenyekiti wa CCM akilazimisha wawe wagombea, kutaleta mtafaruku na chuki kubwa ndani ya CCM kiasi cha baadhi ya wanaCCM kupigia kampeni upande wa pili kwa siri na kwa uwazi.

3) Wachache walionunuliwa na kupitishwa na CCM kuwa wagombea, hawatashinda kwenye kura za wananchi.

MAHESABU

Mradi wa CCM wa ununuzi wa wapinzani umekuwa na hasara kwa CCM na kwa walionunuliwa. Hakuna hata mmoja kati yao aliyepata faida. Ni mradi uliobuniwa na watu wenye IQ ndogo, utekelezaji ukasimamiwa na wenye upeo duni, ukashangiliwa na wajinga wengi. Umetoa funzo kubwa kwa wenye akili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Biashara imefeli na mtaji umeliwa 😂😂😂😂
Kwa CCM mission accomplished................wameweza kupunguza imani ya wananchi kwa wapinzani.............kwa namna walivyokua wananunuliwa yale majimbo yote ya wapinzani waliounga juhudi effect lazima zitaonekana
 
. Ni mradi uliobuniwa na watu wenye IQ ndogo, utekelezaji ukasimamiwa na wenye upeo duni, ukashangiliwa na wajinga wengi. Umetoa funzo kubwa kwa wenye akili
 
Kwa CCM mission accomplished................wameweza kupunguza imani ya wananchi kwa wapinzani.............kwa namna walivyokua wananunuliwa yale majimbo yote ya wapinzani waliounga juhudi effect lazima zitaonekana
Sidhani...kwa kile walichofanya wajumbe sidhani
 
Wamarekani wanavyopenda kuingilia cases kama hizi kwenye mataifa mengine, now wanaendelea kukusanya ushahidi tu. Siku utashangaa file linakuwa disclosed na mpaka waliokuwa wanamwagiza na kiasi cha pesa alichokuwa akikabidhiwa kitatajwa.
Hapo ndipo patakapokuwa patamu, kumbe kwa njia nyingine watu wanaichafua madhabahu unapofika muda wa kutubu wanalia haswa dhamira zikiwachoma ila madaraka yanapofusha
 
Sidhani...kwa kile walichofanya wajumbe sidhani
Wajumbe hawana shida............shida ipo kwa wapiga kura maana watu walioawaamini wakajiuza wataamini tena wachague wa upande ule ule halafu waje kununuliwa tena??? Kwa CCM naona hii ilikua planned kwa sababu maalum
 
M Makubaliano ya awali ndiyo siri ingawa ya watu wengi,lakini wanapomaliza kuunga mkono juhudi hewa,wameliingiza Taiga hasara ya kurudia chaguzi zilizokuwa na maigizo kulikoni Comedy. Watu waliruka sarakasi,usipime.Niliyaona pale Duka Bovu kwa late kalanga,kuna Mbunge moja wa CCM Mpya toka Mbulu aaah.Huyo jamaa ni Acrobat,kitambi hakikuwa kikwazo cha kubinuka kwake.
Leo Kalanga hawezi itisha mkutano hata wa kitongoji chake,hana tena ile bashasha ya kuunga mkono juhudi za Jiwe.
Gharama za chaguzi hizi tulibeba Watanzania kupitia Force Account sawa na miradi mingine ya Ujenzi wa Vituo vya Tiba.
 
Aliyekuwa Mbunge wa Monduli, Julius Kalanga akamatwa na kikosi kazi kwa madeni
 
Ahahhaha kaka Mshana Jr umejaribu sana kusokota maneno umetumia sitiari kwa umakini kaka, siku hizi umekuwa sana kiuandishi.
 
Aliyekula hasara ni wale waunga juhudi ambao pengine hata dau waliloahidiwa hawajapewa lote na wajumbe wamefanya yao.
Ccm hawana hasara sababu hatumii pesa zao za mfukoni ila ni kodi ya watanzani ndio wanajivunia ujinga
 
Pesa ya manunuzi ilitokea mfuko gani?Au ni pesa walionyanganywa watuhumiwa wa kifisadi?
 

Kinachoniuma ni upoteaji wa mamilion ya fedha za wananchi kuwanunua wanasiasa kumbe fedha zile zingetumika kuwaongezea wakandarasi wanaojenga barabara ya morogoro eneo la mbezi Luis na daraja la Sinza Mugabe shekilango road, wakandarasi hao wangeweza kujenga usiku na mchana ili kuwahi kumaliza ujenzi na kuwapunguzia shida ya foleni wanayoipata wananchi kwa sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…