Dropout
JF-Expert Member
- Nov 16, 2017
- 641
- 533
Nawasalimu wanajukwaa wenzangu, salamu iende mbali zaidi kwa wewe kijana mwenzangu ambaye hapo ulipo sio muajiriwa, muajiri wala hujajiajiri.Salamu hii iwe chachu ya kuleta jibu juu nani anapaswa kubeba msalaba wa ukosefu wa ajira ambao umekuathiri baina ya vijana Tanzania.
Kitakwimu yaelezwa kuwa kwa kila vijana ambao wanasaka ajira Serikalini na Waajiri wengine kila mwaka ni kwamba fursa ya kupata ajira ni asilimia 6 tu ya vijana ambao wanaotafuta kazi wote.
Kila mwaka kundi la vijana wanaohitaji ajira nchini Tanzania linaongezeka kwa ukubwa ikiwa ni wale wanaomaliza vyuo vikuu, vyuo vya ufundi,sekondari na wale wanaofikisha miaka 18.Wote hawa wanatafuta ajira.
Nakupatia maswali nane(8) fikirishi yanayokuja kichwani katika kutafuta nani anapaswa kubeba msalaba huu kama sehemu ya UWAJIBIKAJI katika kumaliza tatizo hili nchini, kama ifuatavyo;
1.Je?, Serikali inapaswa kumaliza Tatizo hili kwa kuboresha sera zake kuwezesha na kuongeza vyanzo vya ajira kwa vijana?
2.Je?, Vijana wanapaswa wao wenyewe kujiajiri kwa kuanzisha au kutengeneza na kubuni kitu ambacho kitawapatia ajira?
3.Je?, Ubunifu na Sanaa unaweza kutatua changamoto ya ajira kwa vijana?
4.Je?, Mchango wa Sekta binafsi pekee unaweza kumaliza suala la ukosefu wa ajira?
5.Je?, Wawekezaji wanapaswa kutoa ajira zaidi kwa vijana wazawa kupunguza Tatizo?
5.Je?, Watu waambiwe ukweli mchungu juu ya soko la ajira ili sasa waamue kujua wapeleke wapi watoto wao ili kufikia malengo ambayo wangependa wayapate hapo baadae?
6.Je?, Serikali itumie njia ya wazi kuomba msaada kwa watu binafsi wenye uwezo mkubwa kiakili na wanaofahamu mbinu za kutatua tatizo la ajira kwa vijana kuliko kuendelea kufanyia kazi sera ambazo hazionekani kuleta mafanikio.
7.Je?, Vijana wajifunze mbinu mpya za kujipatia ajira kama kubashiri,kujifunza masoko ya kubadilishia fedha(forex), kazi za mtandaoni(freelancing), kujifunza sayansi ya komputa na sarafu digitali?
8.Je?, Kila mtu abebe mzigo wake yaani kila mtu apambane na hali yake?
Mpaka muda huu anayepaswa kubeba msalaba huu wa ukosefu wa ajira nchini Tanzania bado ni fumbo kwa kila kijana, hii pia inaonesha kila kijana anaelekeza msalaba huo pale anapohisi panapaswa kutatua tatizo hilo.
Kila kijana anayetafuta ajira analalamika kupata ajira ni vigumu sana, hata wale wenye Connection bado wanadai soko limekuwa halisomeki.
Kijana anayejaribu kujiajiri anakutana na ukaribisho mgumu sana kuanzia suala la Mtaji, sehemu za kufanyia biashara, sheria kali za kodi, na Tozo mbalimbali.
Hali ni tete! Keki ya nchi inaliwa na wachache, vijana wengi wanajuta kuingia katika hili kundi maana katika hatua hii inabidi kijana aanze kujitafutia maisha kupitia kazi au ajira ambazo zimekuwa adimu sana.
Je?, Wewe unasema nani abebe msalaba huu mzito?
Nawasilisha Kwenu JF!
#uwajibikaji

Upvote
1