Je, ni nyakati za kufanya maamuzi haya?

Je, ni nyakati za kufanya maamuzi haya?

Uliho

New Member
Joined
Sep 13, 2024
Posts
3
Reaction score
1
Katika historia mwanadamu Kila kipindi cha wakati ni muhimu kufanya maamuzi sahihi, kama unataka uwe sahihi zaidi unaweza kuomba ushauri Kwa watu sahihi ili kufikia utimamu Kwa Asilimia kubwa katika usahihi wako, unapokosea lazima wakati ukuhumu na utabaki na hatia au uharibifu wa wakati unaweza kukuharibu, mfano ukikosea ujanani unaweza ukakumbana na uharibifu ujanani au ukabaki na hatia ya maamuzi yasiyo sahihi katika ujana wako.

Mwaka huu wa uchaguzi ni muhimu Kila jambo tukalindea Kwa tafadhali kubwa iwe Kwa Neno au Kwa tendo, hasa tujizuie katika katika kauli na matendo hata kama unaona yanaweza kukusaidia kufikia kupata nafasi ya kisiasa.

Tangu tupate uhuru waasisi wamesisitiza sana umoja na utengamano wa kitaifa na kuepuka vitendo vinavyoleta chuki ya kikabila , kidini na kikanda.

Mimi naona wakati huu si jambo njema Kwa mamulaka kuchukua hatua ya kufuata usajiri wa Kanisa, au hatua nyingine Kali zaidi Kwa kanisa wakati aliyefanya au aliyeonekana kwenda kinyume ni mtu Mmoja.

Kanisa ni taasisi ambayo ndani yake Kuna watu wa idikadi tofauti. Hivyo kiongozi wa kanisa anaweza kutofautina misimamo na baadhi mambo lakini wakauganishwa na Imani Yao.

Hivyo unapofungia kanisa unagusa hisia za wakristo wote wa TANZANIA, kumbuka watanzania wanaweza kutofautina idikadi lakini maslahi ya TANZANIA yanapodhumiwa na mtu nje ya TANZANIA watayapigania kama watanzania, waislamu wanaweza kutofautiana kiimani katika mambo madogomadogo lakini lipokuja suala la Imani Yao kunyanyaswa wataungana kama waislamu, vivyo hivyo Kwa wakristo, ni wazi masuala ya kiimani ni mambo nyeti sana si ya kuendea Kwa papara.

Hivyo ni Rai yangu Kwa mamulaka hili kufuta usajiri wa Kanisa mliangalie vizuri, hasa wakati huu
 
Wewe jamaa una kibali kweli cha kuishi nchini! Maana usipokuwa makini Mamulaka watakubeba na kukurejesha nchini mwako ukiwa taabani kwa maumivu.
 
Tungekuwa na watu hata 10 kama wewe kwenye MAMULAKA, nchi ingekuwa mbali sana
 
Back
Top Bottom