Je ni sahihi Ahmed Ally, kutangaza biashara binafsi akiwa amevaa jezi ya Simba, Je tangazo hilo Simba inanufaika nalo?

Je ni sahihi Ahmed Ally, kutangaza biashara binafsi akiwa amevaa jezi ya Simba, Je tangazo hilo Simba inanufaika nalo?

Alexido jz instagram

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2026
Posts
4,686
Reaction score
10,018
Nimeona tangazo Instagram, msemaji wa klabu ya simba akitangaza kampuni ya uuzaji wa ac, sio kosa ila kosa nikutangaza biashara BINAFSI zisizo nufaisha klabu akiwa na JEZI ya SIMBA ilihali ni msemaji wa klabu au ni muajiriwa wa brand huru ya simba kitengo cha habari kuufahamisha umma Kwa mambo mbalimbali yanayo husu klabu

Brand inayo jitegemea, au brand huruma yenye utaratibu wake kisheria hii itaifanya klabu kukosa mapato ya Moja Kwa Moja. Nina hoja mbili tu:

FALSE ENDORSEMENT
hii itaonesha kuwa klabu imeruhusu mashabiki zake na klabu inaunga mkono bidhaa tajwa na muhusika kitu ambacho si kweli.

TRADE MARK
Hii itaonesha klabu imeidhinisha matumizi ya bidhaa tajwa hapo juu, jambo amabalo lita ikosesha klabu mapato.


Zachariano alexido

Mchambuzi maswala ya kijamii, burudani na michezo

Screenshot_20260723-203504.jpg
Screenshot_20260723-203514.jpg
Screenshot_20260723-203504.jpg
Screenshot_20260723-203514.jpg
 
Ile si jezi tu, hapo alisimama kama yeye, raia wa kawaida...
 
Ni kweli lakini, wadhifa wake kwenye klabu hakupaswa kufanya hivo
Kwa kias kikubwa sana tangazo litafikia watu wengi, hata kama asingevaa jezi...

Lakini kwa sababu pesa atakayolipa haiwezi kuhisiwa na mzani wa pesa ya simba... Basi hata timu ikichukua kias fulani katika mapato yake bado itakuwa ni pesa kidogo sana...


Lakini ni kweli sio sawa kulingana na wasifu wake
 
Mtoa mada mbona kama unamuonea wivu huyo Ahmed Ally! Kwani hiyo jezi ya simba ina nini mpaka iwe kosa kwa mtu kuivaa na kutangaza biashara?

Mbona kuna wahuni walioshiriki kuua Watanganyika Oktoba 29, 2025 walionekana wakiwa mtaani na silaha, huku mmoja wao akiwa amevaa jezi ya Yanga! Na hakuna aliyetilia maanani!
 
Kabla ya Simba ni wangapi walikuwa wanamjua Ahmed Ally, mchezaji wa Simba akifanya tangazo akiwa amevaa jezi za Simba ni sahihi sababu wote ni waajiliwa.
Kitendo cha kutangaza akiwa amevaa jezi ya Simba ni makosa makubwa sababu washabiki wa Simba wakimwona na jezi ya Simba lazima watavutiwa kutaka kujua clab yao inataka kutoa habari gani?
Anahitaji kupewa job description ya kazi yake.
 
Naunga mkono hoja....unless kuna makubaliano na club ambayo hayajawekwa wazi.
Upo sahihi mkuu kwa uelewa wangu mdogo.
Screenshot_20260724-135452.png

Huyo ni muuza tiles huko Gerezani. Yeye na wauza maduka wengine wafanye nini kwenye unachokishauri?
 
Back
Top Bottom