Jerry Farms
JF-Expert Member
- Jul 18, 2022
- 202
- 167
Kama kawa wanajamvi!( Na mimi nimeona nianze na kasalamu kama ndg Pasikali!)
Imezoeleka huku majimboni pindi cha ziara za viongozi kuona wawakilishi wa wananchi wakisimama na kuomba miradi ya maendeleo kwa viongozi walioko ziara!
Na wananchi pasi kujua kama hayo mambo yalikaliwa vikao na kupitishwa, huruka ruka kwa nderemo na vifijo kuwa wamefikiwa katika utatuzi wa jambo lao!!!
Lahaula!...swali la msingi, je ni ujinga wetu wananchi wakutokusoma bajeti za wizara ama ni viongozi wetu wanatuchezea akili! Ama ni viongozi wenye ziara wanachezewa akili!
Ni vimaswali fikilishi saana huku majimboni! Tunaomba wawakilishi muwe mnawasilisha kero ( "kama zinaweza kuamuliwa kwa kusikilizwa na kufanyiwa kazi pasi majadiliano ya vikao vya wataalamu na bodi za maamuzi") zile ambazo bado hazijaguswa katika maeneo yenu na si kufanya marudio ya kile kile. Tunawaomba saana, maadamu tunaelekea kwenye chaguzi basi mjitahidi kutowatumia wapiga kura wenu kwa manufaa yenu binafsi!
Wassalaamu!!
Mwananchi.