Je ni sahihi kukodi 'wajasiriamali' wa Kulia msibani?

Farolito

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2018
Posts
12,001
Reaction score
27,175
Habari Wakuu,
Nilikuwa naangali UTV kipindi cha KAZI ambapo wanahoji watu wanaofanya kazi mbalimbali za kujipatia kipato.

Sasa katika kipindi cha Leo walikuwa wanawahoji watu wanaouza majeneza,wachimbaji wa makaburi na baadae waliwahoji watu 'wanaolia msibani' kwa kulipwa pesa.

Hawa ni kikundi cha akina mama ambao kazi yao ni kulia kwenye misiba kwa malipo ya fedha.Unachofanya wewe ukiwa na msiba unawatafuta halafu unawapa taarifa fupi ya marehemu(alikuwaje) na uhusiano wako na marehemu,hapo mtakubaliana malipo kutokana na muda wa Kulia kama ni Masaa kadhaa au siku nzima na wao watatengeza 'script yao' ya Namna ya kulia.

Swali ninalojiuliza hawa wenye msiba(wafiwa) ambao wanakodi hawa wajariamali wa Kulia msibani huwa wana Lengo gani? (aliyewahi kuwatumia atuambie)

Je unadhani Kulia msibani ni kazi halali?na kama ni hivyo kuna haja ya kurasimisha hivi vikundi vitambuliwe na serikali?

Na Je wanaume pia wapo?maana mi niliona wanawake tu.

Asante.
 
Mzee baba hujazingua kweli

Au ndo vile kila kitu kinafeki yake
 
Hujui kwamba ili upate pesa ni lazima utoe pesa...

Hujaelewa... ni hivi unapokuwa umefiwa watu wanaleta pesa kwajili ya mahanio sasa kuguswa kwa mtu mpaka atoe hiyo pesa kunatokana na mfiwa. Unapolia huku unalalamika ndo watu wanavyozidi kuguswa na kutoa ila Ukila ganzi sana utaambulia pole za mdomo tu

Sasa chukulia umekodi mtu analia kwa kulalamika " marehemu umetuachia yule mtu wa mkopo anayedai pesa zake nani atalipa na wewe ndo ulikuwa tegemeo, vipi hawa watoto ada zao na mahitaji yao ya msingi ya kila siku, mama kijijini alikuwa akikutemea na yale matibabu yake yanayogharimu hela nyingi na kesho ndo ilikuwa siku ya kupeleka advansi ya watu, mungu kwanini umemchukua kaka yetu sisi tutaenda wapi jamani"... nk

Unadhani atakosa wa kuwapata hapo
 
Kama umemuua ndugu yako inabidi utafute watu wa kulia ili msiba ufane.
 
Kwahio tuseme wafiwa wanakuwa na tamaa ya kutengeneza pesa kupitia msiba?
 
Hiyo Ndiyo dawa ya waswahili wanaopenda kususia wenzao misiba wakizani wanawakomoa eti kwa kigezo kuwa mtu fulani haendagi kwenye misiba ya wenzio [emoji87][emoji87]
 
Kwanza mimi huwa nawashangaa wale wenye kupenda kuhusudu wenzao kuwa hawaendagi misibani!

Inamaana Mpaka ujue fulani haendagi kwenye misiba Je umethibitishaje?

Je vipi iwapo ulipishana naye kwenye msiba wakati wewe umeenda yeye alishatoka?

Tuache kuhusudiana, tupendane !

Tuwiwe upendo tu!
 
Hiyo Ndiyo dawa ya waswahili wanaopenda kususia wenzao misiba wakizani wanawakomoa eti kwa kigezo kuwa mtu fulani haendagi kwenye misiba ya wenzio [emoji87][emoji87]
Sasa mkuu ukisusiwa msiba hata ukileta hao waliaji watano au kumi wanakufariji nini?gharama za msiba si bado ziko palepale?na wanazidi kukuongezea mzigo tu
 
Mpaka kufikia hatua ya kukodi waombolezaji ujue huyo alofiwa mara nyingi siyo mtu wa choka mbaya!

Na Ndiyo maana wengine humuonea wivu mkali Yani husuda.

Ukisikia kuna mtu au familia fulani imekodi waombolezaji ujue hawana hela ya mawazo [emoji108][emoji108]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…