HOJA Je, ni sahihi kulipia kodi ya bango lililopo kwenye eneo lako la biashara?

HOJA Je, ni sahihi kulipia kodi ya bango lililopo kwenye eneo lako la biashara?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
A

Anonymous

Guest
Je, ni sahihi mfanyabiashara kulipia kodi ya bango lililowekwa juu ya fremu yake ya biashara, wakati tayari analipa kodi ya pango, leseni ya biashara na kodi nyingine zinazohusika kupitia TRA?

Ninaelewa kuwa bango likiwekwa kwenye eneo la umma, kama vile barabarani au kwenye eneo linalomilikiwa na Serikali, kunaweza kuwa na sababu za kutozwa ada. Hata hivyo, inakuwaje pale bango linapowekwa ndani ya eneo lako la biashara au juu ya fremu unayopanga na kulipia kodi?

Naomba ufafanuzi kutoka kwa mamlaka husika: Je, kisheria mfanyabiashara anatakiwa kulipia bango hilo hata kama lipo kwenye eneo lake la biashara? Ikiwa ni hivyo, ni sheria au utaratibu gani unaotumika kukokotoa na kutoza ada hiyo?

Tunaomba suala hili lifafanuliwe ili wafanyabiashara waelewe wajibu wao na msingi wa kisheria wa malipo hayo.
 
Back
Top Bottom