Je, ni sahihi kumgeuza X wako kuwa rafiki yako kindakindaki?

Je, ni sahihi kumgeuza X wako kuwa rafiki yako kindakindaki?

GEMBESON

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2012
Posts
1,463
Reaction score
3,193
Utafiti uliofanywa na Oakland University unaeleza kwamba Watu wanaowageuza Wapenzi walioachana nao (Ma- EX) kuwa Marafiki zao wa karibu mara nyingi huwa na uwezekano mkubwa wa kuwa na matatizo ya afya akili.

"Kuendelea kumkumbatia Ex na kumgeuza Rafiki yako wa karibu kunaweza kukufanya upate hasira, chuki na huzuni hasa kama ulimpenda sana, akishakugeuza Rafiki kuna wakati atakusimulia hata raha anazopewa na Mpenzi wake mpya itakuyumbisha, atapost picha akijiachia na Mpenzi wake itakupa jaka la moyo"

"Kuna ile hali pia ya kujipa matumaini kwamba utaendelea kunufaika na EX wako kwa kupata penzi, fedha n.k, pia kuna wengine hujigeuza Mamba na Ma-EX ndio nyama kwamba nyama imewekwa kwenye eneo fulani Mamba akijisikia kula anaamini atakwenda kuila wakati wowote, hata ukiwa na Mpenzi wako mpya unaweza kushindwa kumove on kisa EX"

Unaupa ngapi Utafiti huu, BIG YES au BIG NO!?, je, ni sahihi kumgeuza EX kuwa Rafiki yako kindakindaki?

Credit: Millardayo
 
Inategemea mliachana vipi. Kama mliachana kistaarabu bado mtaendelea kuwa marafiki na mtakuwa mnaweza kupasha viporo pale mke anapogoma kutoa mdinyo unapata pa kupoozea.
 
Tafiti za wazungu huko (hasa hizi za kisaikolojia na kijamii na hata kisiasa) mara nyingi sisi Waafrika huku huwa hazituhusu kivile. Best friend ambaye ni ex wako na hampashi kiporo we ulisikia wapi kwa Mwafrika? Tafiti zingine za wazungu tuziache huko huko aisee!
 
Inategemea mliachana vipi. Kama mliachana kistaarabu bado mtaendelea kuwa marafiki na mtakuwa mnaweza kupasha viporo pale mke anapogoma kutoa mdinyo unapata pa kupoozea.
Hii ni moja ya faida. Japo hasara ya hii tabia ni chanzo cha kuambukizwa magonjwa ya zinaa na kuyaleta kwa mkeo au mumeo.
 
Sio vibaya kufanya hivyo kulinda heshima yako!
 
Kuna X wangu tulipendana sana. Amenifanyia mazuri 99% baya ni moja tu.

Tulipanga kufunga ndoa sijui nini kilimpata ,akanimwaga akaolewa na mwanaume wa kabila lake siku hizi ananitafuta anataka tuwe marafiki.

Dr K. stay the f*ck away from me, we can't be friends.
 
Kuna X wangu tulipendana sana. Amenifanyia mazuri 99% baya ni moja tu.
Tulipanga kufunga ndoa sijui nini kilimpata akanimwaga akaolewa na mwanaume wa kabila lake siku hizi ananitafuta anataka tuwe marafiki.
Dr K. stay the f*ck away from me, we can't be friends.
Kwa senario yako inaonyesha alikusaliti na kwenda kuolewa na mtu mwingine, hivyo bado wewe una hasira nae. Huyu hamuwezi kuwa marafiki kwa kuwa hamkuachana vizuri, labda mpaka wewe ukubaliane na hali ya kuachwa.
 
Kwani kuachana vizuri ndo kupoje mkuu
 
Kwan kuachana vizuri ndo kupoje mkuu
Vizuri ni Kuachana bila kuwa na kinyongo cha yeye kuolewa na mtu mwingine. Unamtakia mema tu na wewe unatafuta kifaa kingine.

Mfano ulimfumania demu wako yupo na mtu mwingine, ukampa kichapo cha paka mwizi, ukamnyang'anya kilakitu ulichowahi kumnunulia - Huko ndio kuachana vibaya.
 
Ok, mchepuko kapigiwa cm na wife baad ya wife kushstukia cm kadhaa za uck na mchepuko ukaamua tuachane hii imekaaje ki wema au baya
 
Back
Top Bottom