Je, ni sahihi kumuita mtoto jina ambalo halina maana?

Je, ni sahihi kumuita mtoto jina ambalo halina maana?

DR HAYA LAND

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2017
Posts
23,928
Reaction score
63,499
Leo Nimemtembelea Dada yangu amejifungua mtoto wa kiume. Hila Jambo la kushangaza kampatia mtoto wake jina la Buluga, baada ya ku-google hili jina sijafanikiwa kujua maana yake then na Mama yake anadai hafahamu maana ya jina hilo.

Je, ni sahihi kumptia mtoto wako jina Ambalo halina Maana?

Mfano Mimi naitwa TID maana yake Top in Dar.
 
Sasa wewe jina buluga ulitaka ulikute kwenye server za google kweli? Majina yakizungu ndio yenye maana huko google kwenu lakini yakiafrika mengi tunayajua wenyewe. Hilo ni bonge la jina muachieni mtoto.
 
Kwa kisukuma lina maana nzuri tu moe mtoto hilo jiina
 
Mpe jina kulingana na nyota yake. mnakosea sana. dada yako kaona nyota ya mtoto ndio jina lake
 
Akija kufanya makubwa , hilo Jina unaloliona halina maana litakuwa maarufu na watu wataliiga.
Kila kitu kina mwanzo.
By the way Jina ni Jina
 
Jina ni mtu. Jina la mtu ni mtu mwenyewe! Ndio maana sisi tunalitumia Jina la Yesu kufanyia mambo makubwa sana. Bwana Yesu anasema, "... kwa Jina langu mtatoa pepo, mtasema kwa lugha mpya, mtashika nyoka, hata mkinywa kitu cha kufisha hakitawadhuru, ... "

Umeona???? Kwa "Jina" mambo yanafanyika.


JESUS IS LORD
 
Beluga ni aina ya nyangumi ila hilo lingine sijui, au kakosea umsahihishe amuite BELUGA
 
Siyo kila jina hufaa kupewa kila mtoto.Tulia na ufanye uchaguzi wa jina la mtoto kulingana mambo muhimu.Lakini,majina kama Shida,Mateso,Masumbuko,Mkegani,Chakupewa,Chausiku na mengine yafananayo na hayo,hapana.Yatamfanya aenende na tafsiri yake.
 
Hakuna jina ambalo halina maana labla umpe Jshdjsnshsjs ndio halina maana mbali hapo Lina maana tatizo lugha lugha
 
The Google Syndrome Disease (GSD), kwamba kila jina utafute maana google.
Huenda kwa kilugha chao lina maana ila hakuwa na maneno ya kukuridhisha
 
The Google Syndrome Disease (GSD), kwamba kila jina utafute maana google.
Huenda kwa kilugha chao lina maana ila hakuwa na maneno ya kukuridhisha

katika wajinga ni wewe.
Hivi ulishwai kutumia kifaa cha tovuti bila search engine
 
Back
Top Bottom