Leo Nimemtembelea Dada yangu amejifungua mtoto wa kiume. Hila Jambo la kushangaza kampatia mtoto wake jina la Buluga, baada ya ku-google hili jina sijafanikiwa kujua maana yake then na Mama yake anadai hafahamu maana ya jina hilo.
Je, ni sahihi kumptia mtoto wako jina Ambalo halina Maana?
Majina yote yana maana ,anae toa jina ndio hujua maana yake.Hakuna jina losilo na maana.
Hilo jina la buluga ni la kijadi hivyo kwenye google linaweza isiwepo mana yake
Sasa wewe jina buluga ulitaka ulikute kwenye server za google kweli? Majina yakizungu ndio yenye maana huko google kwenu lakini yakiafrika mengi tunayajua wenyewe. Hilo ni bonge la jina muachieni mtoto.
Jina ni mtu. Jina la mtu ni mtu mwenyewe! Ndio maana sisi tunalitumia Jina la Yesu kufanyia mambo makubwa sana. Bwana Yesu anasema, "... kwa Jina langu mtatoa pepo, mtasema kwa lugha mpya, mtashika nyoka, hata mkinywa kitu cha kufisha hakitawadhuru, ... "
Siyo kila jina hufaa kupewa kila mtoto.Tulia na ufanye uchaguzi wa jina la mtoto kulingana mambo muhimu.Lakini,majina kama Shida,Mateso,Masumbuko,Mkegani,Chakupewa,Chausiku na mengine yafananayo na hayo,hapana.Yatamfanya aenende na tafsiri yake.