Je, ni sahihi kuosha engine ya gari?

fredo fred

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2015
Posts
748
Reaction score
1,615
Habari wakuu poleni na kazi,

Hivi ni sahihi kuosha eneo la engine la gari kama inavyoonesha pichani?

Maana hiyo gari ilikuwa inaoshwa ili sehemu ya engine ionekane inag'aa.

Lengo ni kuuzwa ili ionekane engine haina tatizo.

Je, ni sahihi kufanya hivyo?

 
Je hiyo engine ina leakage yoyote ya oil?? Ndiyo maana mnaosha ili mnunuaji asitambue hilo??

Ila usafi ni muhimu pote nje na ndani, kitu cha kuzingatia tu maji yasiingie katika sehemu ambazo zinaweza pelekea gari ipate, mfano maji yakiingia kwenye ignition coil au kwenye mfumo wa mafuta na uchomaji (spark plug)
hupelekea gari kuwaka kwa shida au kutokuwaka kabisa.
 
Lengo wa uoshaji huo hapo ni wizi mtupu...kwa sababu kuna boya anaenda kupigwa..

Tuachane na hayo...Ni sawa injini inaweza kuoshwa lakini kwa utaratibu maalumu.

1.Funika sehemu nyeti za umeme kama alternator, fuse boxes na starter motor.

2.Ukishaosha injini hakikisha unaipuliza kwa upepo mkali..

Kama huwezi kuzngatia hayo, usioshe injini yako, acha kama ilivyo uwe tu unaipuliza kwa upepo mkali..
 

Sijawahi kuosha engine ya gari zangu zote nilizowahi kua nazo na sijawahi kupata tatizo lolote lile sababu ya kutoosha engine.
 
Mtu mwenye kujua gari hata usioshe yeye anajua Tu,mwenye kujua gari ataiwasha Kwanza alafu anafungua bonnet kukagua kimoja baada ya kingine..
Nilipokuwa nauza Carina Ti sijasumbuka Sana Kwa upande wa engine Kwasabb ya utunzaji wangu ulikuwa wa Hali juu na kila Mteja aliyekaguwa gari hakuna ambaye aliweka mashaka hata kidogo!!

engine yenye leakage hata uoshe vipi bado itajulikana Tu
 
Mkuu kanuni za utanzaji wa gari ni zipi?
 
Mkuu kanuni za utanzaji wa gari ni zipi?
Utunzaji wa gari inajumuisha mambo mengi ikiwemo kufanya service Kwa wakati pia kubadilisha spare part Kwa wakati bila kuathiri na kitu kingine.
Ukikuta ubovu upo sehemu fulan usisubiri mpaka uambukize na kitu kingine ni Bora gari kipaki Tu home.

Gari Yangu ilikuwa ya kizamani lkn bado nilikuwa natumia coolants mwanzomwisho,kabla ya safari ndefu nilikuwa nasafisha rejeta na kuondoa uchafu wote Kwenye cooling system
 
Mkuu haya mambo ya kusafisha rejeta nilikuwa siyajui.Natamani unipe madini zaidi nisiyoyajua juu ya utunzaji wa gari.
 
Ni sawa lakini mwoshaji asitumie maji ya kisima na achanganye na sabuni yake maalum
 
Hivi mkuu hilo eneo huwa halipaswi kuoshwa?
Mkuu kuna uoshaji wake, si kama huyo anaosha kama vyombo vya sherehe..
Na kama hujui taratibu za kusafisha injini, iache kama ilivyo..

Kuna gari zikioshwa injini tu, kwikwi inaanzia hapo
 
Mkuu kuna uoshaji wake, si kama huyo anaosha kama vyombo vya sherehe..
Na kama hujui taratibu za kusafisha injini, iache kama ilivyo..

Kuna gari zikioshwa injini tu, kwikwi inaanzia hapo
Nilishawahi osha Nissan Xtrail,

Check engine ikawaka, hadi kuizima ilinitoka kama 250k. Nikaapa sirudii kuruhusu kitu kama hiki tena.

Ilikuwa mwaka 2015.
 
Nilishawahi osha Nissan Xtrail,

Check engine ikawaka, hadi kuizima ilinitoka kama 250k. Nikaapa sirudii kuruhusu kitu kama hiki tena.

Ilikuwa mwaka 2015.
Pole sana aisee
 
Oil itaonekana tu, engine ikiwa safi au chafu. Wewe utashindwa kuona michirizi ya oil toka kwenye cylinder head?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…