Je, ni sahihi kutafsiri kitendo cha kupiga picha mwili wa marehemu kama udhalilishaji?

Je, ni sahihi kutafsiri kitendo cha kupiga picha mwili wa marehemu kama udhalilishaji?

Anonymous Caller

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2016
Posts
1,434
Reaction score
1,930
Kuna tabia mpya imezuka nchini ya kuwalalamikia vitendo vya watu wanaopiga na ku-post picha za wapendwa wao wakiwa tayari wamefariki.....aidha wakiwa kwenye jeneza, kwenye matukio ya ajari au wakiwa mawodini...

Je kuna ubaya gani mtu kuhifadhi kumbukumbu ya picha ya mpendwa wake akiwa katika hali ya umauti...

Je tatizo ni kuipiga hiyo picha au tatizo ni kuipost hiyo picha..au vyote.

Kama kitendo hicho sio fair...Kwanini Baba wa Taifa, Mwalimu Julias Nyerere alipigwa picha akiwa ndani ya Jeneza....na picha hiyo ilianikwa kwenye magazeti yote ya wakati ule...
(Hata mimi Picha ninayo hadi leo)

Kwanini Rais mstaafu wa Kenya Daniel Arap Moi mwili wake uliagwa peupe mbele ya television za nchi hiyo..ukiwa kwenye open casket.

Juzi tulishuhudia mwili wa Papa Fransis ukibebwa na baadaye kuswaliwa tena ukiwa kwenye machela?

Ukiondoa exceptions za mwili kutokuwa katika hali nzuri, je udharirishaji unakujaje hapo.
Naomba wakuu tueleweshane hapo.
 
hili swali litajibiwa vizuri siku akifufuka mpigwa picha mmoja akaja kutufanyia vurugu mara moja tuone walivyokereka na hili swala, oya sijui hiyo siku itakuwaje hata ukiwa umelewa njia utaona!..😂
 
Hivi inamanaana ipo siku utakaa seblen uangalie video ya marehemu Mpendwa wako au mtu wakaribu sababu hata wanaouchukua Video sina hakika kama huwa wanaangaliaga
Hata mm huwa najiuliza sana kuangalia tu picha ambazo akikuwa hai ni mtiti sembuse kafa.sie tulikataa msiba wa mama picha na video zote hakuna.tuliwauliza za nn sie??tutaangalia ambazo yungali hai
 
Back
Top Bottom