Je, ni sahihi kwa nchi moja moja za kiafrika kuota Maendeleo? Je, sio kujidanganya?

Je, ni sahihi kwa nchi moja moja za kiafrika kuota Maendeleo? Je, sio kujidanganya?

JingalaFalsafa,
Mkuu wangu maneno yako mazito sana na sijui kama watu wanaelewa uzito wake kwa mwafrika kama waasisi wa Uhuru wa nchi zetu - Sidhani na kama wapo leo wameshaondoa hisia hizo kutokana na umbu la vijana waliokamata tawala sasa hivi..

Adui mkubwa wa maendeleo ya Waafrika ni Umaskini na Ujinga wenyewe. Leo inajionyesha wazi wazi kwamba muungano wa nchi maskini hauwezekani tena kutokana na umaskini pamoja na Ujiunga walotuachia wakoloni..Unajua waasisi wetu wa Uhuru walijua uyasemayo na ndio maana ktk maandalizi ya Uhuru wa nchi zetu waliweka vikao kwanza wakielewa wazi kwamba Uhuru wa Bendera tu hauwezi kutuondolea matatizo yetu. Walijua wazi tuna maaadui wawili wakubwa mmoja wa nje (UKOLONI) na mwingine wa ndani UMASIKINI na UJINGA hivyo wakatafakari njia na mbinu za sio tu Afrika iwe huru bali pia kuunganisha mataifa yetu, ili tupate nguvu ya kiuchumi dhidi ya ukoloni na ule wa mamboleo ambao walikuwa wakituibia rasilimali zetu..

Kwa bahati walifanikiwa nusu ile ya kwanza kumwondoa mkoloni lakini kwa bahati mbaya zaidi wakashindwa kutuunganisha..Na sii kwamba haikuwezekana isipokuwa Umaskini na Ujinga ulichukua nafasi kubwa ktk maamuzi kama nisemavyo maskini hugombania hata chakula badala ya kugawana chakula.. Inashangaza lakini ndio ukweli. Na nadhani unazidi kuyaona maajabu ya waafrika tukizidi kugawanyika hata nchi zilizweza kuungana jana leo hawapendani tena kwa sababu ya Umaskini na Ujinga.

Kifupi mkuu wangu UTU wa mwanadamu ni ajizi kwa maskini, tunaweza sana kulalamika kunyoioshea watu vidole lakini siku zote itabakia kuchumia mkono uendao kinywani. Hatuwezi kupambana na Ukoloni mamboleo kwa fikra za nchi moja moja haiwezekani na ndio maana leo nchi yoyote inayojaribu kupambana na wezi hawa huwekewa vikwazo na utajikuta peke yako. Nchi za magharibi wamehakikisha hilo haliwezekani kutokana na kwamba wana control nguvu ya umaskini wetu na Ujinga wetu...Hata elimu tunayosomeshwa ni ELIMU inayoweza tu kuendesha biashara zao, unayoweza fanya kazi tu ndani ya mfumo wao lakini kwa undani wake ni elimu inayomweka Mwafrika kuwa mtumwa na mhitaji zaidi..

Tumefikia mahala lazima tukubali, wachache waliopo leo wenye fikra kama zako huitwa Magaidi - Terrorists kwa sababu unatishia interest zao..Na wanasema wazi kabisa kwamba watalinda interest zao nje kwa njia yoyote ile possible hivyo IMF, World Bank, UN yvote hivi ni vyombo vinavyounganisha maskini na matajiri jinsi gani tunaweza kuishi pamoja tukinyonywa kwa kipande cha mkate. Mimi na wewe hatuwezi kuiokoa Afrika, hatuwezi kupandikiza mbegu mpya kwa sababu hata mkulima hupanda kwenye ardhi yenye rutuba na maji sio juu na magugu au jangwa.. Vichwa vya waafrika ktk umaskini ni sawa kabisa na magugu au jangwa kwa umaskini na Ujinga, hakitaota kitu..

Kibwagizo:- AFRICOM si wameingia Tz tayari sasa tazama hapa:-

The U.S. needs oil. And Africa has it. Lots of it. It's in this context that the Bush administration has announced a new central command for its military presence in Africa called AFRICA COMMAND (AFRICOM).

Please listen to Avis Lewis live on Africa's Ungoverned Spaces!......Play the video, get the big picture!

http://www.cbc.ca/onthemap/fullpage.php?id=119
 
Last edited by a moderator:
Mmh! Mkuu wangu Mkandara, unanitoa machozi ya damu moyoni mwangu! Unatia siki kwenye madonda yangu mabichi!
Inauma sana Kuyafikiria! Yanakatisha tamaa ukishayajua. Lakini....NAAMINI KABISA KWAMBA KUNA KITU TUNAWEZA KUFANYA! Japo ukweli si rahisi hata kidogo, ni sawa na kutoa maji kwenye pipa kwa kijiko, haitofautiani hata kidogo, haijalishi ni muda gani atatumia huyo mtoa maji, lakini kuna siku atatoa tone la mwisho pipani!

Narejea tafsiri yangu ya Maisha kuwa, "Maisha ni Furaha, kama haipo ni upuuzi. Na hakuna Furaha ya mtu ila watu"
Ni ukweli kabisa kwa watu wenye unyonge kama wetu sisi, wanaoandamwa na magonjwa, njaa, unyonyaji, unyanyasaji, ukandamizaji, vita, na kila aina ya mateso, watu hawa hawana tafsiri nyingine ya maisha kwao zaidi ya UPUUZI, HAKIKA kwao maisha ni ushenzi mtupu! Swali! Je, tujiue tuondokane kabisa na upuuzi huu? Huku ni Kukata Tamaa, HAKUNA NAFASI! Je, tuvumilie tu hadi mwisho wa dunia! LINI? (ikiwa miaka 1000 mbele je) UPI? Tutawezaje?

Tusijiue ila TUISHI. Kwangu KUISHI kwa sasa ni kuandaa "what will determine your death" je ni Furaha Batili au Upendo? KIFO, ni nafasi atoayo mtu kwa watu kuishi kile alichokiamini! (najua, anaweza kufa mtoto mdogo, pia tunaweza kuishi imani ya mtu kabla hajafa-muhimu hapa ni kifo kwa mtu aliyeishi, yaani yule aliyeandaa diterminant ya kifo chake, je ni furaha batili au upendo?)

(a) Yule aliyechagua furaha kuwa "king'amuzi" cha kifo chake, ni yule mtu atakayejitafutia furaha binafsi, atakeyetafuta kucheka hali wenzake wanalia, atakayetaka kujikweza katikati ya wanyonge, ni yule atafutae furaha ya mtu sio watu na hapo ubatili ndipo unapoingia! Ni mpumbavu!

(b) Yule achaguae upendo kuwa "king'amuzi" cha kifo chake, ni yule aishie kwa kumfikiria mwenzake, ni yule ajitoae kutafuta furaha ya kweli ya maisha, yaani furaha ya watu si mtu, ni yule aongozwaye na Mantiki-Utu! Huyu atakufa, akiwa anaitafuta na kupigania furaha ya kweli!

Ukweli wa Mambo:
Hakuna apingae kuwa sisi ni wafu walio hai kaburini! Tumezikwa hai na hatuwezi kamwe kujinasua! Tumekufa huku bado tupo hai! (inauma sana ndugu zangu) Lakini ndio ukweli huo! Tumezikwa hai, tumezikwa huku TUNAISHI.

Swali, je tuishi furaha batili humu kaburini tulimo kwa kuanza kuviziana wenyewe kwa wenyewe tuuane na kulana nyama? Au, tuishi UPENDO? Kupi ni kuishi upendo kaburini humu tulimo? Ni wazi tutakufa/tunakufa! Je, ni sahihi kuendelea kujifikiria mimi tena? Nani anapaswa kufikiriwa, je ni wewe mwenzangu tunaokufa wote jioni? HAPANA si wewe wala huyu afae kesho! Kuna huyu azaliwae kaburini, afae siku za mbele zaidi kama tutamuacha afe! Ndiye huyu atakayekusanya mifupa yetu ama kuitupa chooni ama kuitunza, nafasi yetu i leo Mkuu Mkandara! Nafasi ya kuishi upendo na si furaha batili, nafasi ya kuonesha upendo kwa kizazi chetu kijacho! Tumwambie tulimokosea, tumtafutie njia ya kulikimbia kaburi, sisi hatuwezi kulikimbia maana njia ni ndefu mno, ni wazi tutaanguka njiani! Upendo wetu kwa kizazi chetu kijacho, ni kuwajengea misingi bora ya japo kuitambua na kuiishi Mantiki, kabla hawajaifikia furaha ya maisha! TUSIJIFIKIRIE SISI.

"Mito ya machozi ya furaha kutoka machoni mwa watoto wetu, italowesha mifupa yetu aridhini! Gharama ya Upendo wetu kwao!" Tulishazikwa hai, tusiache watoto wetu nao! Ee Mungu, na usimamie hili.

TUNAWEZA....nguvu yetu ni UMOJA na KUTHUBUU.

Mungu wetu yu tayari kutupigania vitani, anaita sasa!
 
Last edited by a moderator:
JingalaFalsafa

Nakumbuka siku moja nikisoma kitabu cha mashujaa wa zamani. wakisia vita huchukua mikuki, panga na sime zao kwenda vitani lakini siku hizi babu tukisikia mlio wa bomu wengi wetu hutafuta nchi za kukimbilia mbali kabisa na mali zetu japo kuokoa roho.

Nakusikia sana lakini kilio chako, changu na cha mwingine kitabakia sawa na mfungwa gerezani ambaye siku zote hufikiria njia ya kutoroka na sio kuasi amri..Afrika imekuwa nchi ya wakosa na kwa kila kitu sisi ni wakosa, wakosa wa hali, mali na akili ya upembuzi japokuwa roho zetu zimejaa UTU. Wako wapi kina Steve Biko, Kina Lumumba, Nkurumah, Kenyatta, Nyerere wote hawa hata ktk ukumbi wa AU hakuna makumbusho yao, hatuna nukuu hata za mapambano ya Majimaji kuwakumbuka mashujaa wetu isipokuwa wale waliopanda mlima Kilimanjaro.

Mtu huthaminika zaidi akisha kufa na kufukiwa kaburini kuliko uhai wake, eeeeh! Mola wangu kheri mtumwa wa Israel aliacha maajabu Misri kuliko mtumwa wa akili kuinafiki nafsi yake mwenyewe. Kwa fahari tunazicheza na ngoma kumwalika Bush, rasilimali zikiibiwa wala tusishangae, maana tunachotumaini sio thamani ya tunu bali shanga urembo wa shingoni. ..

- NDIVYO TULIVYO!
 
Last edited by a moderator:
Mkandara,

HAPANA mkuu wangu, ni mwiko kusema "ndivyo tulivyo" lazima tufanye kitu kwa ajili ya watoto wetu! Ikumbukwe kuwa, waovu wetu waliumiza vichwa sana, walitumia muda mwingi sana kutufikisha hapa tulipo! Babu za wazungu, wangejifikiria wao binafsi basi leo ulaya isingekuwa pale ilipo!

Kweli tunapaswa "Kutangaza Vita" Vita halisi! Lakini si vita mapanga! Hatuwezi hata siku moja! TUTANGAZE VITA YA AKILI, JUU YA FIKRA ZETU! Tuzipindue Fikra zetu na za watoto wetu! Waifahamu KWELI, na Kweli hiyo itawaongoza kupigania furaha ya kweli-MANTIKI-UTU!

Tuwaambie Nyeupe ni nyeupe na Nyeusi ni Nyeusi. Si kufumba macho na kupindua mantiki! Hata kama wewe umeambiwa uamini kuwa nyeusi ni nyeupe na nyeupe ni nyeusi, isiwe kwa mwanao! ACHA MARA MOJA! Mwambie ukweli, naye ataupigania! Tusiwavishe miwani meusi watoto wetu ili waone wali mweupe ni pilau! Sawa na kumvika farasi miwani ya kijani ale majani makavu! Ni upumbavu! Adui wa kwanza ni nafsi zetu wenyewe, zinakiuka mantiki iliyomo humo-tuwajengee misingi ya kuishi mantiki hiyo watoto wetu! Hakika, tukiweza HATUTAKUFA kama mbwa, ila TUTAENDELEA KUISHI HATA BAADA YA KIFO CHETU! Huko ndiko kuishi kwa mara ya pili! Naipenda sana Afrika, vile neno lisivyoweza kueleza!

Bob alinena hivi "WAR....until the philosophy, which holds one race superior and another inferior" "emancipate yourself from mental slavery, None but ourself can free our minds, Have no fear for a-atomic energy, because none of them can stop the time"
Lets bless War, and sing Redemption song! It's not physical but LOGICAL WAR...Mungu wetu yupo kutushindia!
Anaita sasa!

Mungu wetu anaita!
 
Last edited by a moderator:
JingalaFalsafa

Labda nikuulize hili:

Zanzibar wanataka kujitenga, je unafikiri ni Fikra gani zinaweza kuwasogeza karibu zaidi na watanganyika.. Malawi wanadai ziwa Nyasa ni lao na kuheshimu mipaka ya mkoloni aliyetuteka na kutugawa unafikri ni fikra zipi leo hii zitawafanya watuelewe sisi na kuacha madai yao acha swala zito zaidi la kufikia Afrika moja!. Tazama ramani ya Afrika leo inazidi kuongezeka nchi zake badala ya kupungua halafu tunafikri tunaweza kweli kuwa wamoja. Binafsi yangu naamini afadhali hata ya Mkoloni aliweza kutawala eneo kubwa lakini sisi tunapokwedna tutarudi ktk utawala wa Makabila..

NDIVYO TULIVYO sote hatuipendi kabisa lakini msukuko wa tamaa za kibonadamu uloambatana na umaskini na Ujinga mkuu wangu tuna kazi ngumu sana kuwaelimisha Maskini na Wajinga. Kwa sababu siri ya kundi hili ni nzito kuliko zote. Hawa ni ktk kundi la watu Wanafikiri wanajua kumbe hawajui lakini hawajui kama hawajui ila wanajua kuliko wanaojua.

Hawa ndio kisa cha Punda kumpeleka mtoni huwezi kumlazimisha kunywa maji. Huwezi kutumia kigezo hiki kwa binadamu mwenye akili timamu lakini Wabongo nimewaona wakitumia hata kwa madaktari kuwafanya wao wana reputation of stubbornness kama Punda, very cautious na hupima situation (safety) kabla ya ku react..maana mnyama huyu asili yake ni jangwani hapendi maji hata iwe mvua na huwa halazimishwi sii tu kunywa maji bali hata kuwa karibu na maji..Sasa ni afadhali ya huyo Punda kuliko sisi Waafrika tuliotawaliwa kwa zaidi ya miaka 500 ya utumwani na kukoloniwa bado tuna shindwa kujilinda wenyewe dhidi ya maamdui wetu.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mkandara,

Malawi na Zanzibar hawawezi kumfikiria Mtanganyika, sawa na vile kwa Kenya na Somalia au Ghana na Nigeria, hatimae Afrika nzima!
Huwezi kuwaambia hao kuithamini THAMANI YA UAFRIKA, si leo wala kesho! Kwani UAFRIKA wetu haumo kwenye maisha yetu kwa sasa, si Uchumi, Siasa wala Tamaduni, vile unaweza kumwambia Mmalawi embu angalia hiki kinatuunganisha ili akithamini! Mfano mdogo: Mfumo wa Uchumi umeruhusu private ownership, utaepuka vipi UBINAFSI/UMIMI KWANZA? Haki za Binadamu zinasema Uhuru wa kuabudu, utaepuka vipi aenezae imani potofu za Ndugu wa muislamu ni Muislamu mwenzake, au aenezae "nuru na giza avichangamani, aliyeokoka ni ndugu wa aliyeokoka tu"?

Hii mitego ndugu zangu, sio kazi rahisi!

Uafrika wetu haupo kwenye mifumo yetu ya maisha, ni Ndoto za mchana kuota leo au kesho tunaweza kumshawishi Mmalawi au Mzanzibar kutanguliza Uafrika! Si mimi wa mwanangu, hata mjukuu wangu atakayeweza kushuhudia Uafrika wetu na kuuthamini!
Ni vitukuu vyetu watakaoweza kuishi thamani hiyo, ila tu kama mimi na wewe leo TUTAWASIMIKIA MISINGI BORA YA KUISHI HAYO, tucheze nafasi yetu vizuri katika hilo! Ni MIMI na WEWE si WATOTO WETU!

Mungu wetu anaita!
 
Last edited by a moderator:
JingalaFalsafa

Shukran sana na kwa maelezo haya ndio maana nasema NDIVYO TULIVYO kwa sababu hatuna sababu ya maana kabisa kwa nini tunalilia mipaka ya nchi ama Uhuru wa mipaka. Unaweza kuamini kwamba Wazanaibar wanadai UHURU kamili kutoka kwa Tanganyika.. Uliwahi kusikia kitu hii? yaani sisi Watanganyiika tumekuwa wakoloni kiasi kwamba sijui tunachukua kipi kutoka Visiwani kwa manufaa ya bara, Kwao na wengine wote iwe Malawi, Zanzibar, Rwanda, Uganda na wanataka utengano wa kurudisha makabila na mipaka yake kwa kjutazama watu waishio mipakani wana asili ya makabila gani hivyo kuhalalisha madai yao ama kutumia fikra za mkoloni kutugawa kuwa na uhalali ili watutawale ndio sawa..

- Hivyo, hatutaweza kuwa na Afrika moja, na kwa bahati mbaya sana tumesahau malengo ya Afrika huru kiasi kwamba nguvu kubwa ilowekwa na waasisi wa jitahada hizi hazithaminiki tena..Let's just forget development, tuendelee kupigania ku survive ndani ya Umaskini na Ujinga ulotulemaza.

Na kuhusu Imani ya kiislkaam isemayo Ndugu wa Muislaam ni Muislaam mwenzake ina maana tofauti kabisa na unavyoilewa ama niseme mnavyofundishwa. Kwanza lazima ujiulize Muislaam ni nani? Musilaam ni mtu yeyote aliyejitoa kumtumikia Mungu -Total submission to God ambaye katuamrisha Kuuthamini UTU wetu.

Na hakika ndugu ya Muumini huyu atakuwa Mtu mwingne anayeabudu UTU..Tafuta tafsiri zote za Humanity utazikuta ndizo Mola alotusisitiza sisi binadamu kuzifuata na kama utashidwa kuzifuata ndipo Uislaam wako huondoka. AS to say, Uislaam ni kuthamini UTU.. Acha hizi habari za Masheikh Udwanzi wanaofikiria Muislaam ni yule alotiwa maji na kuitwa Abdallah au Jakaya kwa kuweka ahadi ya kumuabudu Mwenyezi Mungu lakini asifite UTU isipokuwa kwa kusubiri mwezi wa Ramadhan...Huyu hana tofauti na Kafir!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mkandara,

Kusema NDIVYO TULIVYO isimaanishe kwamba hakuna tunachoweza kufanya! Kwanza sisi tumetengenezwa kuwa TULIVYO, basi nasi tuna nafasi na tunaweza kujitengeneza kuwa tupendavyo! Ila ni mchakato wa muda mrefu na wenye kujitoa hasa! Ndio maana nasema, TUWATAZAME WATOTO WETU WA KESHOKUTWA, SI WA JUZI, JANA, LEO, WALA KESHO, tuwafanyie jambo! Muhimu ni kutambua kwanza, kuchanganua kisha kuchukua hatua mahususi. Swali tuanze nini, aje, na wapi? Ni lazima mimi na wewe, tukae chini, tuumizi vichwa katika tafakari kuu, tufikie Azimio Jipya, then TULIPIGANIE kwa kulipenyeza mioyoni mwa watoto wetu! Tujenge Fikra sahihi vichwani mwao, tufanyie mapinduzi nafsi zao za kinafiki na kisaliti, tupande MANTIKI vichwani mwao- UTU.

Kuhusu ndugu wa muislamu ni muislamu, nazungumzia wale wapotoshaji wa uislamu, wako huru kupotosha uislamu kwakuwa mifumo inaruhusu! Ni kwamba kama uislamu ni UTU, UTU huo unakufa kwa muislamu kwani analazimika kuishi mifumo mingine ya uchumi na siasa ambayo UTU haupo ndaniye! Ndio maana nasema "UCHUMI, SIASA na TAMADUNI havitakiwi kukidhana kwani vinategemeana mno, vinatakiwa kuongozwa na msingi mmoja wa maisha, na kila kitu kilalie humo, hakuna msingi mwingine zaidi ya UTU! Haumo kwenye Demokrasia, wala Private Ownership, hivyo kama uislamu ni UTU, basi HAUPO TENA! Je, tukubali tu pasi kuupigania? Sawa na kwa Ukristo, wanasema ukristo ni Upendo, ambao ni mwana wa UTU, Upendo huo haumo kwenye Demokrasia wala Private Ownership, basi ukristo nao umekufa, kwani hakuna mtu asiyeishi demokrasia au Private Ownership leo hii. Je, tukae kimya tu pasi kuutetea ukristo ama uislamu wetu?

TUSIJIDANGANYE, DINI NI PAMOJA NA SIASA UCHUMI NA TAMADUNI, huwezi kuwa muislamu au mkristo kwa kuingia msikitini au kanisani tu, ni lazima dini yako ikuzunguke katika kila kitu chako! Ndio maana nasema, Mungu wetu yu tayari kutusimamia kupigania imani ya kweli, UTU-MANTIKI-KUFIKIRIANA-UWIANO SAHIHI.

Anaita sasa!
 
Last edited by a moderator:
JingalaFalsafa

Waislaam na Wakristu wa kweli wapo?... Ndivyo Tulivyo ina maanisha tumekataa UTU na kubeba visivyo kwa sababu kila haramu ilokatazwa sisi tumeihalalisha..na unapotaka kutumia imani yako ya UTu kwanza utaitwa gaidi na umati mkubwa watakutenga, utatafuta hadi mapangoni iwe Torabora au ZengaZenga na utundikwe..

Binafsi yangu haya yote nayoyaandika humu ni fikra pevu lakini hazina ushawishi wa kutosha kwa maskini wanaogombania sinia la biriani, maana ndipo tulipokaa ktk janvi kubwa la mkeka tukisubiri kuhitimisha. Nakwa maskini wa hali na mali walokuja na ndizi mifukoni wakitegemea biriani wakati wa maombolezi ya kifo cha Mtanzania na rasilimali zake. Usipoweka sini la Biriani hitma yako haitaheshimiwa, na wala marehemu hata pongezwa.. Mimi na wewe hatuna uwezo nalo isipokuwa mkono mtupu ambao haulambwi na hekima za vitabu vya ibada ambavyo havina wokozi wa kimwili. Hizi ndizo Athari za Umaskini na hakika NDIVYO TULIVYO ni pamoja na kukataa unyonge tolokuwa nao...

Neno Maskini linashikamana na Unyonge na ndio maana mtu akionewa husema oooh masikini Mkandara!.. Bahati mbaya ni kwamba anayeweza kunisaidia naye hana uwezo, hana elimu na dhaifu hivyo tunabakia kuzunguzia EVENTS kwa mapana yake. Kwa maskini kuzungumzia IDEA pasipo ELIMU ni sawa na tungo za Shaaban Robert tunazisoma na kuzisetiri vichwani kama misahafu lakini hatujui maana wala thamani yake.

Naipenda sana AFRIKA yangu, naililia AFRIKA yangu lakini siwezi kukataa ukweli ulio hali kwamba sisi ni watumwa wa maamuzi yetu wenyewe, utumwa ambao tumeshindwa kuuondoka ktk fikra zetu hata baada ya kuupata Uhuru wa bendera. Na athari zake zimetuponza kutothamini maadui wetu ndizo zinatuweka ktk unyonge hii leo..Wako wapi mashujaa wetu? wako wapi kina Umsolopogaas, kina Mkwawa, Mangi Sina na wengineo walozipoteza roho zao kwa kuutukuza Auafrika wetu.

Ebu nambie JingalaFalsafa, leo hii ukisema hatutaki uwekezaji nchini ikiwa hatupewi ownership, utapongezwa na wangapi? Pengine hutaamka na kuiona nuru kesho yake, kwa sababu utaondoa riziki za watu, unaondoa sinia la Hitma japokuwa ni maombolezi ya kunyonywa na kifo cha uchumi wetu. Unayoyaona leo ni hitma ya Afrika ambayo kwa viongozi wetu wamekuja na ndizi zao wanategemea kukaa meza kubwa kuomboleza kwa chakula chenye mapande ya nyama!. Ni shibe ya siku moja lakini muhimu sana kwa mapana ya itifaki za mtumwa...

Siwezi kuikarifu nafsi kwa kujaribu lisilowezekana. Sina ubavu wala ushawishi wa kutosha kumwambia Mtanzania maneno mazito kama ya Umsolopagass mwana wa Chaka aliposema Makumazan kwa shauku kubwa ya vita ilokuwa mbele yake akisema "Kama wale wachovu wakija basi ni mimi nitakayelinda ngazi kuu hadi mlango umejengwa.."

Siwezi kwa sababu maadui tayari wameisha ingia ngome kuu na wako ndani na wanashinda vita baina yetu sisi wenyewe. Leo hii mabinti zetu ndio wake zao, ndio wanaowajengea majumba na wengine ndio wanetu wameoa na kuleta Ustaarabu mpya unaotukuza UTWANA...Hii ni dunia ya kugombea Uchumi upate kutukuka na sio tena UTU ulokamilika..
 
Last edited by a moderator:
Nakusikia Mkuu wangu Mkandara,

Kuhusu Uwekezaji, ni wazi kabisa ukikurupuka leo ukasema ni marafuku, basi utapigwa na raia wako kwanza kabla ya mabepari wa nje hawajakuburuza barabarani ukiwa maiti tayari. Lakini haiondoi ukweli kwamba Uwekezaji ni Unyonyaji! Tujiulize sasa, kwanini nipingwe na ndugu zangu wenyewe kwanza?

Ni wazi, raia wamejengewa imani potofu, imani iliyoingia fikrani mwao, hawajiamini tena, wanaamini pasi uwekezaji sisi ni bure, hatuna imani wala utayari wa kujiamulia mambo yetu binafsi. Hawa ni watumwa wa fikra! Utumwa wao vichwani mwao hauondoki kwa kuwashikia fimbo, ni lazima tuumize vichwa! Katika hilo sasa, ndipo jukumu letu sasa linapoibuka, TUTOE UTUMWA HUU KWA NDUGU ZETU, na silaha pekee ni kuwafundisha MANTIKI-UKWELI-UTU, tusiseme ndivyo tulivyo au hatuwezi kufanya chochote, ni UTUMWA PIA-Inferiority Complex=Mental Slavery! Je, mimi au wewe tukubali tu! HAPANA!

TUNAWEZA KUFANYA KITU. Nguvu yetu ni UMOJA na KUTHUBUTU-TUNAWEZA! TUPANDE MBEGU KWANZA-watoto wetu wetu wataipalilia-vitukuu vitavuna mazao yake! Huko ni Kuishi hata baada ya kifo chetu!

Mungu wetu anaita sasa!
 
Last edited by a moderator:
Kwanza naomba kumshukuru mtoa mada, umenifanya nifikirie sana siku nzima ya leo na pia mkuu Mkandara, hoja zenu nzito sana!
Nakubaliana kwa kiasi kikubwa sana kwamba hii kitu inaitwa "democracy" na viambatanisho vyake HAIJAWAHI na HAITAWEZA kututoa hapa tulipokwama infact (correct me if am wrong) hakuna Jamii, Empire, Kingdom au Nchi iliyowahi kutoka katika hali kama hii tuliyokua nayo na kufikia maendeleo kwa kutumia democracy. Democracy kwangu ni kiini macho,kipindi cha nyuma nilikua naamini kwamba democracy inahitaji mazingira na maendeleo ya fikra za watu kama za hizo nchi zinazoitwa "developed", kwa nchi kama yetu ambayo idadi ya wasiojua kusoma na kuandika inakua kwa kasi kila siku, democracy ni mazingaombwe.

Kwa Mkuu Mkandara unanikumbusha nadharia ya Plato ya "Allegory of the Cave", Waafrika kwa kiasi kikubwa tunasadifu maudhui ya hiyo nadharia ya Plato,tumekuzwa na dhana potofu na mbaya zaidi tumekua "brainwashed", hatujui kiini wala misingi ya mambo mengi ambayo yamekua ni utaratibu wa maisha yetu, (kama sio yamekua ndio utamaduni wetu) kama, elimu,dini na imani, siasa, maendeleo ya teknolojia na vitu inavyoambatana navyo kama utandawazi n.k. Tupotupo tu tunapokea kila kitu kinachokuja kwa hii milango mitano ya fahamu bila kukifikiria wala kushuku undani wale na maudhui yake,tumekua kama vifaranga wa ndege kwenye kiota wasio na uwezo wa kuruka wala kuona vizuri, kazi yao ni kupanua midomo yao kila wakimsikia mama yao wakiamin kawaletea chakula,hata kama kabeba kinyesi wao watakula tu si kimeletwa na mama!

Swali langu ni tunaanzia wapi,maana lazima tuanzie somewhere,je tuipige chini democracy na tulete Aristocracy ya maphilosopher kings kama Mwalimu Nyerere? Je hii jamii yetu inao uwezo ndani yake kuzalisha viongozi wa namna hiyo au tutaishia kuleta madikteta? Tukikubali kushindwa ni dhambi kwa UTU na kwa "race" ya mtu mweusi, kwa vizazi vilivyotangulia, kwa mshujaa wetu waliokufa wakipigania UTU wetu na kwa vizazi vijavyo.

Najiulizaa halafu naishia kujiuliza tuu,ila napata faraja nikikutana na hoja zilizoshiba kama hizi na inasadifu ile dhana kwamba maendeleo halisi yaanzia kwenye fikra!
 
Last edited by a moderator:
"Tukikubali kushindwa itakuwa ni dhambi kwa UTU na kwa 'race' ya mtu mweusi", huu ni mkuki wa moto upenyao moyoni mwangu kila uchao! Kauli hii ndiyo iumizayo kichwa kuifikiri, kwani hiyo ndio MANTIKI, nao ndio UTU! Ee Mungu wetu, tuangazie njia! Ni MANTIKI-UTU!

Thamani ya mtu mweusi ni UAFRIKA wake. Inauma haipo kwa sasa! Tumekuwa duni! Tumekuwa kama vifaranga vilivyopoteza mama mvuani! Thamani yetu itajengwa na sisi wenyewe! NI LAZIMA TUUMIZE VICHWA! Hizi ni HESABU ndefu zilizotunasa! Tupigane sasa kujinasua!

Nachoamini ni hiki "HULKA ZA BINADAMU ZINAPOKIDHI VIWANGO VYA UKAMILIFU WAKE, BASI ZINAWEZA KUUHAMISHA MLIMA KILIMANJARO KWENDA POPOTE, lakini matokeo yake huwa HASI siku zote! Naita Shetani-evil! Vile vile, MANTIKI INAPOKIDHI VIWANGO VYAKE VYA UKAMILIFU, BASI INAWEZA KUKAUSHA HATA BAHARI KWA SEKUNDE MOJA TU, na matokeo yake yakawa CHANYA. Naita Mungu-UTU"

Hakuna kinachoshindikana kwetu, ila tu...tukiamua, nguvu yetu ni UMOJA na KUTHUBUTU!

Mungu wetu anaita sasa!
 
AFRIKA:
Ndivyo tulivyoingizwa kaburini tukiwa hai!

SASA KIPI NI TIJA KWETU? Je, tufuate MANTIKI ama HULKA zetu? MANTIKI ina nguvu na mamlaka juu ya HULKA lakini si HULKA kwa MANTIKI! HULKA hufika mwisho na kufa, lakini MANTIKI haiwezi kufa!

Binafsi, kama mtu mweusi. "AFRIKA ni Taifa moja, lenye MAZINGIRA na NYAKATI zinazoshabihiana kwa kiwango kikubwa! Sote ni WAHANGA wa janga moja, HATUNA BUDI KUFIKIRIANA! Sote tumo kaburini tulikozikwa hai! Tusipofikiriana hata kwa atakayejitolea mfupa wake kaburini tulimo, ili kuchhmba shimo la kutokea, HAITASAIDIA! Kwani wapo watakaochinjana kugombea mfupa au kuuvunja, wapo watakaotoka na mfupa na kuziba shimo wengne wasitoke! Wapo watakaokubali kuuza watoto wao na wake zao kwa mabwana wa nje ya kaburi, walau watupiwe karanga!

Mwishowe kizazi kitakuja, kitapita bado tu kaburini! Vitukuu vyetu vitawaka hasira zao juu yetu, kwa kushindwa kuwaachia japo msingi wa kutoka nje ya kaburi. Huu ni Unafiki na Usaliti wa nafsi zetu wenyewe!

Ni lazima mwishowe kila mtu afikirie AFRIKAMOJA!

Je, inawezekana? Je, ni ndoto za kitoto kama tunavyoamini sasa? Mimi nasema HAPANA, si ndoto! Na sababu ni hii! UMOJA wa Afrika ni zao la MANTIKI na si HULKA! Na MANTIKI haijawahi kushindwa hata siku moja, ila tu kwa kukosa wapiganiaji HUKIUKWA! Na mara tu wanapopatikana hupata Ushindi mnono! Lets Live Logic! We will never die alive! But we will live even after our death!

Swali muhimu: NI KWA NAMNA GANI TUNAWEZA KUIFANYA AFRIKAMOJA! Tufanye nini?

Vichwa ni lazima viume, HESABU za hali ya juu kabisa zinahitajika! Ni lazima Tufanye Ubunifu Wa Hali ya Juu Sana! Tucheze na vitu vitatu, MAZINGIRA, NYAKATI na MANTIKI. TUNAWEZA! Nguvu yetu ni Umoja na Kuthubutu!

Ubunifu Haujawahi Kufika Mwisho. TUUMIZE VICHWA SASA! AFRIKA MOJA.

Mungu wetu anaita!
 
Waislaam na Wakristu wa kweli wapo?... Ndivyo Tulivyo ina maanisha tumekataa UTU na kubeba visivyo kwa sababu kila haramu ilokatazwa sisi tumeihalalisha..na unapotaka kutumia imani yako ya UTu kwanza utaitwa gaidi na umati mkubwa watakutenga, utatafuta hadi mapangoni iwe Torabora au ZengaZenga na utundikwe..

Binafsi yangu haya yote nayoyaandika humu ni fikra pevu lakini hazina ushawishi wa kutosha kwa maskini wanaogombania sinia la biriani, maana ndipo tulipokaa ktk janvi kubwa la mkeka tukisubiri kuhitimisha. Nakwa maskini wa hali na mali walokuja na ndizi mifukoni wakitegemea biriani wakati wa maombolezi ya kifo cha Mtanzania na rasilimali zake. Usipoweka sini la Biriani hitma yako haitaheshimiwa, na wala marehemu hata pongezwa.. Mimi na wewe hatuna uwezo nalo isipokuwa mkono mtupu ambao haulambwi na hekima za vitabu vya ibada ambavyo havina wokozi wa kimwili. Hizi ndizo Athari za Umaskini na hakika NDIVYO TULIVYO ni pamoja na kukataa unyonge tolokuwa nao...

Neno Maskini linashikamana na Unyonge na ndio maana mtu akionewa husema oooh masikini Mkandara!.. Bahati mbaya ni kwamba anayeweza kunisaidia naye hana uwezo, hana elimu na dhaifu hivyo tunabakia kuzunguzia EVENTS kwa mapana yake. Kwa maskini kuzungumzia IDEA pasipo ELIMU ni sawa na tungo za Shaaban Robert tunazisoma na kuzisetiri vichwani kama misahafu lakini hatujui maana wala thamani yake.

Naipenda sana AFRIKA yangu, naililia AFRIKA yangu lakini siwezi kukataa ukweli ulio hali kwamba sisi ni watumwa wa maamuzi yetu wenyewe, utumwa ambao tumeshindwa kuuondoka ktk fikra zetu hata baada ya kuupata Uhuru wa bendera. Na athari zake zimetuponza kutothamini maadui wetu ndizo zinatuweka ktk unyonge hii leo..Wako wapi mashujaa wetu? wako wapi kina Umsolopogaas, kina Mkwawa, Mangi Sina na wengineo walozipoteza roho zao kwa kuutukuza Auafrika wetu.

Ebu nambie JingalaFalsafa, leo hii ukisema hatutaki uwekezaji nchini ikiwa hatupewi ownership, utapongezwa na wangapi? Pengine hutaamka na kuiona nuru kesho yake, kwa sababu utaondoa riziki za watu, unaondoa sinia la Hitma japokuwa ni maombolezi ya kunyonywa na kifo cha uchumi wetu. Unayoyaona leo ni hitma ya Afrika ambayo kwa viongozi wetu wamekuja na ndizi zao wanategemea kukaa meza kubwa kuomboleza kwa chakula chenye mapande ya nyama!. Ni shibe ya siku moja lakini muhimu sana kwa mapana ya itifaki za mtumwa...

Siwezi kuikarifu nafsi kwa kujaribu lisilowezekana. Sina ubavu wala ushawishi wa kutosha kumwambia Mtanzania maneno mazito kama ya Umsolopagass mwana wa Chaka aliposema Makumazan kwa shauku kubwa ya vita ilokuwa mbele yake akisema "Kama wale wachovu wakija basi ni mimi nitakayelinda ngazi kuu hadi mlango umejengwa.."

Siwezi kwa sababu maadui tayari wameisha ingia ngome kuu na wako ndani na wanashinda vita baina yetu sisi wenyewe. Leo hii mabinti zetu ndio wake zao, ndio wanaowajengea majumba na wengine ndio wanetu wameoa na kuleta Ustaarabu mpya unaotukuza UTWANA...Hii ni dunia ya kugombea Uchumi upate kutukuka na sio tena UTU ulokamilika..

Mkandara
Umeandika hapa maneno mazito sana, leo ni kama umenitandika makofi usoni mwangu. sidhani kama umebakiwa na nguvu kwenye mifupa yako baada ya kuweka hizo nukta mbili za mwisho.
 
Dhana POTOFU "UHALISIA WA DUNIA/MAISHA-DUNIA/MAISHA NDIVYO YANAVYOTAKA" Utumwa wa Fikra! (Gogo limelazwa, ole ashupazae shingo)

Ole wangu maana bado naishi, kwanini sipendi kujiua? Poor me!

Mambo mazito leo ni kawaida kuamuliwa kwa hoja nyepesi, eti "Dunia ndivyo inavyotaka-hatuna budi kufuata-ndio Uhalisia wa dunia" Pumbavu sana! Nani kasema huo ndio uhalisia wa maisha? Kwa vigezo vipi? Kwanini tukubaliane nae? Kwani UHALISIA ni nini katika KUISHI yaani maisha? Je, unaoitwa leo ni UHALISIA si huu UBATILI MKUBWA? Je, si fedhea kuishi UBATILI?

Kwa Upeo wangu, labda ni wakipumbavu, hakuna UHALISIA mwingine ila ule unaohakikisha UENDELEVU wa mwanadamu kamili (REALITY-guarantees sustainability of the proper human qualities-physically/materially-biologically-mentally/cognitive-spiritually as well as environmentally)

Binadamu hapaswi kuishi Reality of the Situation ila tu kama ndio huo uhalisia wa maisha! Wanataka tuishi kitumwa kwasababu wao ni ma-slave masters! Ni UBATILI si UHALISIA! Tusidanganywe! Pumbavu!

Leo tunaweza kuhoji sasa juu ya yale yatuzungukayo kila siku, je ni UBATILI au UHALISI? Do they guarantee the Proper qualities of human being? Au zinamuharibu? Chukulia mfano mdogo sana, leo kuna mapinduzi makubwa sana ya kiteknolojia katika kila sekta yamejikita humo! Hiyo ni Situation iliyopo, sasa je ni BATILI au HALISI? Wameweza kumkuza kuku kwa wiki tatu akawa mnofu, vyakula vya kopo kuokoa muda, neti na dawaze, ona kansa magonjwa ya moyo, kuzaa kwa kisu, ni kitu cha kawaida leo! Bado tunashinikizwa kuafikiana nao, eti ndio uhalisia wa maisha! Je, huo si UBATILI? Pumbavu!

Ona ma-TV yavyoharibu watoto, vijarida na magazeti-maadili yamepotea! Bado mnakenua meno kuita ndio UHALISIA-utandawazi! Huo ni UBATILI! Msidanganyike, huo ni UBATILI. Ni mwovu tu ndio anayeweza kuishi huo ubatili!

Ona leo demokrasia, utumwa na machafuko inayoyazalisha, lakini bado wanasema si UBATILI ni UHALISIA! HALI HALISI na UHALISIA WA MAISHA ni vitu viwili tofauti. Siku zote ni lazima tupiganie Uhalisia wa maisha. HATUTAKIWI KUUPIGANIA UTUMWA KWAKUWA TU NDIO ULIOPO KWA SASA, ila UHALISIA WA MAISHA uliokiukwa.

Always the REALITY guarantees the sustainability of the proper human qualities katka maisha!

Kwa kigezo cha "NDIO UHALISIA WA MAISHA/DUNIA" wameweza kutu-shape na mambo yao mengi tu-KUMBE WANATUPITISHA JUU YA GOGO LAO...TUNAANGAMIA.

Wao ndio wamekuwa kila siku wakinadi yao kuwa ndio uhalisia, na yetu ndio ubatili nasi hatuhamaki hata! Hivi inamaana sisi hatuna jema lolote la dunia kuiga? Ni UBATILI si UHALISIA.

Siku zinapita kwa kasi, kizazi chetu kinapita chaja kingine ki karibu, lakini bado hakuna jitihada za kuwanasua na UBATILI uliopo. Na laana na kisasi cha watoto wetu iwake juu yetu kwanza, kama tutakaa kimya pasi kufanya jambo kwao.

Makanisani na misikitini, mikutano ya wanasiasa, wanaharakati, wasomi na wanazuoni, kote huko mahubiri ni ya kutukuza UBATILI waliombiwa ndio UHALISIA. Huo ndio msingi mkubwa wa UTUMWA WA KIFIKRA-UKOLONI MAMBOLEO. Ukishajenga hoja zako kwa vigezo vya Uhalisia, umeshapotea tayari. Tusiishi reality of the situation(can be a system) maana humo ubatili hufanya maskani, ila tu kama uhalisia huo ndio wa maisha ishi.

Anything or situation that guarantees the sustainability of proper human being qualities-spiritually-mentally/cognitively-physically/materially-biologically anda environmentally, ikiwa hivyo basi ndio UHALISIA, kama sivyo-huo ni UBATILI.

Nguvu yetu ni Umoja na Kuthubutu. Ubunifu hahujawahi kufika mwisho.

Mungu wetu yu tayari kutupigania vitani.
Anaita sasa.
 
Utayari wa watu kujiletea maendeleo yao wenyewe huanza kwa watu. Mimi ni mtu ambaye ninaye pinga nadharia ya kuwa Afrika ikiungana kwamba itapata maendeleo yake kwa haraka kwanini? watu wanaweza kunipinga sana lakini sababu zangu ni za kimsingi.

Huwezi kuunganisha Afrika wakati nchi moja moja zenyewe ndani yake watu wake sio wamoja. Ni muhimu kwanza tukatengeneza solid foundation ndani ya nchi zetu kwa watu wetu kuwa wamoja na wenye malengo khalafu baadae tukaangalia mbele.

Jamii zetu bado hazijakuwa ipasavyo utaifa bado ni mdogo. Kwahiyo ni lazima tusisitize kwa utaifa ndani ya mataifa yetu. Watu wetu wawe wamoja na wenye malengo ya pamoja ya kuzikomboa nchi zao kutoka katika maradhi ujinga na umaskini khalafu baada ya hapo tuangalie mbele kuunganisha watu wetu wengi zaidi. Hatutaweza kufanikiwa tukiangalia katika kitu kikubwa kabla ya kuangalia kitu kidogo kwanza ni lazima kwanza tuwajibike kwa mataifa yetu, viongozi wetu wawajibike kwa mataifa yao kwa kuwaleta watu pamoja na kuwekeza katika roho ya utaifa.

Na hata hivyo muungano wowote ule ni lazima uwe wa watu ile uendelee sio wa wafanyabishara au wanasiasa ila watu wenyewe washirikiane na waone kuwa wana nia ya wao kuwa wamoja. Kwahiyo katika muungano mingi kuna matatizo ndani ya mataifa yenyewe ya kiutawala bora, ukabila, ufisadi, utii wa sheria nk.

Kama ningekuwa rais wa nchi hii nisingekubali muungano wa Afrika mashariki ningejenga watu wangu kwanza kuwa wamoja zaidi na wenye malengo na uhusiano kati ya nchi zilizotuzunguka ungekuwa uhusiano wa majirani na uhusiano wa kibiashara ukawa ni kama uhusianio mwingine wowote ambao nchi na nchi wanaweza kuuanzisha na kuwa na makubaliano fulani ya kibiashara ambayo yatafanya mahusiano ya kibiashara kati ya nchi hizi kufanyika vizuri. Sijakubaliana na shirikisho la Afrika mashariki na wala sifikirii kama litadumu.

Kenya wanatakiwa wajenge nchi yao kwanza wasuluhishe matatizo yao ya ukabila na uganda ambayo inaongozwa ki dikteta ina matatizo yake. Kila nchi ni lazima ijiendeleze yenyewe kwa juhudi zake na maarifa ya watu wake lakini tunaweza kuwa na mahusiano kama majirani, Tunaweza kuwa na mikataba ya kibiashara ili watu wa nchi hizi mbili wafanye biashara bila matatizo hili halihitaji sisi tuungane.

Kama ni nguvu ya kijeshi tunaweza kuijenga sisi wenyewe kama tukitia juhudi kama tukiwa wamoja na kama tukitafuta maarifa katika mambo ya uvumbuzi na intellejensia. Mambo yote haya yanahitaji raia waliojitolea kuilinda na kuitetea nchi yao, yanahitaji raia wazalendo. Mwisho kwa kupatikana kwa gesi na mafuta katika Tanzania sidhani kama Tanzania itakubali Mataifa ya Afrika mashariki kuwa moja. Kila Taifa ni lazima lijenge character za watu wao na character ya Taifa na litengeneze matumaini kwa watu wake.
 
Nchi nyingi za ki Afrika zinashindwa kufikia malengo yake, kutoka na kutokua na umoja, na hili linatokana na baadhi ya viongozi kua vibaraka wa mataifa ya Afrika wengi wao kua vibaraka wa mataifa ya nje.
 
JingalaFalsafa,
Nakubaliana na wasiwasi ulioonyesha kutokana na kinachoendelea kwa mataifa maskini uchumi kuhodhiwa na mataifa tajiri. Katika ulimwengu wa leo jambo hilo vigumu kuepukika kwani wenye kujenga viwanda vikubwa vya uzalishaji ni makampuni yale yale yenye viwanda nchi zilizoendelea na ndio wanaozungu duniani kushikilia uchumi wa dunia. Matajiri hao ndio wanaodhoofisha nguvu ya viwanda katika mataifa ya magharibi kwa kuamua kuwekeza nchi maskini kwa vile uzalishaji uwe karibu na raw material hali kadhalika cheap labor.

Japan na nchi nyingine za Asia kama Korea, china zimenufaika na matajiri hao kuanzisha viwanda huko kwao, Wazawa nao wakajifunza kutoka kwao na kuanzisha viwanda vidogo vidogo ambavyo vingine vimekua na kuwa viwanda vikubwa. Serikali ya nchi hizo imefanikiwa katika kuwathibiti matajiri hao kuweka sheria zenye kuinufaisha serkali na nchi zao. Sharti moja wapo ajira lazima ifanyike kwa wazawa, kwani ni marufuku ku-import labor kutoka nchi nyingine.

Uthibiti wa kodi ni mkubwa sana, kwani nchi nyingi kama ilivyo nchi za magharibi hakuna msamaha wa kodi kwa wawekezaji. Pia uthibiti wa mapato na matumizi ya viwanda vyao kwa kuwekwa maofisa wa forodha pale kuhakikisha hakuna jeuri inayofanyika utoroshwaji wa products kinyemela. Uthibiti wa account zao kwenye mabenk pamoja na uthibiti wa kiwango cha usafirishaji pesa nje ya nchi.

Tatizo ni mfumo wetu wa utawala wenye kukumbatia wawekezaji kwa kuwapa misamaha ya kodi na hata pale yanapojitokeza wazi makosa kama ilivyotokea utoroshwaji wa dhahabu uliogundulika hakuna hatua za kinidhamu zilizochukulia. Jambo la msingi ni uthibiti wenye kutujengea faida zaidi kubaki nchini si kutoroshwa na wawekezaji.
 
Pamoja sana wakuu wangu:
Mkuu wangu Shayu, LAITI KAMA TUNGEWEZA KUISHI PEKE YETU BILA KUFUNGAMANA NA TAIFA LOLOTE LILE JIRANI NASI, basi tungesema "UMOJA WA AFRIKA SI KITU KWA MAENDELEO YETU"
Lakini huo ni UBATILI kwa sasa, kwani hakuna Tz kama hakuna Kenya, Uganda, Rwanda hadi Gambia to Namibia. Mwishowe unakuta hakuna Tz kama hakuna AFRIKA.
Mafungamano yetu ni lazima kwanza yasimamiwe na misingi imara ya MAHUSIANO, mahusiaono hayo ili yalete tija ni sharti yasiegemee upande wowote! Si kenya wala Tanzania, wala si Uganda wala Tz.
Sasa tujiulize, kipi kitakachomfanya Kenya awe na Positive Consideration kwa Tz ili asitufanyie HILA? Hivi tunajua kwamba leo Marekani ikitaka kupigana nasi atapigana nasi akitokea Kenya? Utasemaje sasa kuwa unaweza kujisimamisha mwenyewe halikuwa umezungukwa na maadui?
HAKUNA silaha bora na yenye nguvu ya kujenga mahusiano sahihi kwetu kama wote tutatanguliza UAFRIKA wetu! Ipi ni thamani halisi ya Uafrika? Hakuna nyingine ila ni UMOJA TU! Uafrika wetu haupingani na Umoja wetu!
Na Umoja si kupeperusha bendera moja au kuwa na serikali moja tu, hapana! Umoja wa kiafrika unamaanisha FIKRA MOJA-izaayo imani moja-sera na mikakati yenye kutufikisha sehemu moja tuitakayo!
Kipindi Tz inapanga bajeti ya maendeleo ya Kigoma, Burundi wameuana wakimbizi wamejaa Kigoma! Wanakuja na kila aina ya dhahama! Kipindi tunapanga bajeti ya maendeleo Malawi analeta chokochoko! Mwl. alipokuwa anahangaika kuiweka Tz katka mstari mnyofu, Amini akaleta chokochoko, kilichotukuta tunajua wote. Kipind sisi tunahangaika na malaria, Kenya na A. Kusini wanatuingzia madawa fake na yaliyoisha muda! Kipindi Kongo wanahangaika na vita mataifa jirani wanaingiza silaha waasi! HATUTOKI NG'OO!
Ni lazima TUFIKIRIANE KWANZA....Ni AFRIKAMOJA TU, inayoweza kujenga MAHUSIANO SAHIHI kwa maendeleo ya Afrika yote.
Mkuu wangu Candid Scope:
Ni kweli kwamba "NI VIGUMU KUEPUKA UCHUMI WETU KUHODHIWA NA NCHI ZA MAGHARIBI" lakini huo ni Ugumu tu, sio kwamba HAIWEZEKANI, "INAWEZEKANA" Afrikamoja ndio silaha bora na yenye nguvu na kutuletea ushindi! Hata wao wenyewe wanaihofu!
HATUWEZI KUONGELEA MIKAKATI KWA SASA KAMA HATUJAPATA FIKRA NA KUZIUNGANISHA KWANZA.
Mungu wetu yu hai, tayari kutushindia vitani!
Anaita sasa!
 
AFRIKA:


Na Haki za Binadamu-hii ndio mbeleko ya Unyonge wetu Afrika, taka tusitake HAKI ni mama wa Ukoloni Mamboleo, ni msingi mkuu wa Utumwa wetu wa Fikra, haki ni silaha ya kukiuka UTU-MANTIKI, HAKI ndio sumu ya Ustawi wetu Afrika! Haki ndio chanzo cha maovu mengi Afrika, Haki ni baba na mama wa UNYONYAJI, Haki ni UPUMBAVU ni UPUUZI MKUBWA! Kama ilivyo kwa maji na moto, ndivyo ilivyo kwa Haki na Mantiki-Utu!

Tafsiri iliyopo juu ya Haki, ni UHALALI wa ama kufanya au kufanyiwa jambo fulani! Uhalali huu ukazaa neno Uhuru-Huria, ukaingizwa kwenye mifumo ya siasa, ikazaliwa Demokrasia, kwenye Uchumi ikazaliwa private ownership, kwenye Utamaduni ikazaliwa neno "vile nijisikiavyo-nitakavyo" pasi kujali Mantiki ya mambo, yaani UTU, kama msingi mkuu wa maisha! Haki zikaongozwa na HILA, kutokana na asili ya binadamu kuzaliwa na Tamaa ya kujikweza-kutafuta Ukuu "kuabudiwa", ni baada ya kupewa uhuru-uhalali, na neno Haki, HILA - ubinafsi na choyo zikashika hatamu, ikaanza mtu na mtu hadi taifa na taifa!

KIMANTIKI (ki-UTU), kila kilicho juu kinasehemu kinashikizwa, yaani kuna kitu kinatoa nguvu yake kulinda uwepo wa kile kitu juu! Kama B ipo juu, basi inashikizwa na A au C au yoyote ili isianguke kwa kupenda ama kulazimika! Huo ndio uitwao UNYONYAJI!
(Hatujadili nani kasema nini juu ya nini, ila vile MANTIKI inavyoweza kutafutwa)

HAKI ikamuweka binadamu Huru, binadamu huyu huyu anaewaka tamaa, matokeo yake-hisia za watu zinatumika kufanya maamuzi na kuongoza maisha, MANTIKI ya mambo ikatupiliwa mbali, watu wakajifikiria binafsi (HILA ZA HAKI), mtu akawa juu ya mtu, taifa juu ya taifa, vita, mauaji, uhasama, fujo, mateso, unyonge, nk vikashika hatamu! Bado Haki, inasadikishwa kuwa suluisho, hatutafiki milele!

MANTI-UTU kama msingi mkuu wa Maisha ya binadamu, inapokiukwa kinachobaki Unyama! Nataka niwe juu yako, ni wazi nitakufanyia hila uwe duni! Tanzania inataka kuwa juu lazima tumfanye Kenya au Uganda awe duni, ili sisi tujikweze (tamaa za binadamu), kama walivyofanya Ulaya, wenyewe kwa wenyewe kwanza, mwisho wakawa wamoja dhidi yetu! Wao wameshafika, lakini sisi hatutofika milele, tutapigana kila siku, kupigania ukuu, tutafitiana kila siku kutafuta ukuu-kumbuka ilianza baina yangu na wewe tu sasa ni taifa na taifa, baada ya kupewa uhuru wa tamaa zetu, nasi tukatumia hisia zetu na mioyo yenye hila, tukabariki upumbavu HAKI, tukakiuka Mantiki UTU !

Mungu wetu yuko hai! Anaita sasa!

Mheshimiwa Jingalafalsafa inaelekea hujachukua muda wako mwingi kutafakari kunijibu. Kwa Afrika kuwa moja hiyo ni ndoto isiyoweza kutimia kwa sasa mpaka nchi mojamoja kutengeneza solid foundation katika nchi zao. Wawe womoja, wazalendo na wenye kujitambua kama Taifa moja moja wakifikia hatua hiyo ya kujitambua kwao kama Taifa hapo ndipo watakapo kuwa na uwezo wa kujiunga na kuwa kitu kimoja.
 
Back
Top Bottom