Je, ni sahihi kwa sisi tusio wa dini ya Kikristo kusheherekea Mwaka Mpya?

Je, ni sahihi kwa sisi tusio wa dini ya Kikristo kusheherekea Mwaka Mpya?

Kwani mleta mada labda sijakuelewa,unamaanisha kusherehekea kwa kupiga vigele gele au kitu gani maana me mwenyewe sijasherehekea au unamaanisha zile wishes kutoka kwa wadau wako ndiyo huzitaki?

Watu mnafanya maisha yawe magumu sana unashindwa nini kumjibu tu mtu kwa neno “Asante“ au ”na kwako pia” kisha uka-lock simu ukaweka mfukoni maisha yakaendelea?
 
Huu mwaka siyo wetu...ni Mwaka wa Kikafir kabisa. Si kama kwenye Kalenda yetu.

Nashangaa naona watu wanatakiana heri na fanaka.
Hii ni misconception kubwa sana miongoni mwa waislamu wengi wenye ilimu ndogo ya dini. Mwaka kama mwaka hauna signifance yoyote katika dini, iwe ni Gregorian ama Hijria. Waislamu hatuna sababu ya kusherehekea mwaka mpya huu kama ambavyo pia hatusherehekei mwaka mpya wa Hijria, ulishawahi kuona kuna sikukuu katika tarehe za kidini kusherehekea mwaka mpya wa kiislamu? hakuna kitu kama hicho.

Sababu ya sisi kuwa na hesabu za mwaka wa kiislamu ilikuwa ni purely uhitaji wa kuwa na kalenda, kitu ambacho kabla ya hapo haikuwa katika ustaarabu wa kiaraabu kwa kuwa huko hapakuwa na dola (tawala zilikuwa za koo na makabila). Baada ya kuanza rasmi dola ya kiislamu ndo pale ilipoonekana uhitaji wa kuwa na Kalenda (if I recall correctly ilianzia kwenye utawala ya Seyyidna Omar). Kwa kuwa Gregorian kalenda imeegemezwa na imani ya kikristo na upagani (reference ya counting na majina ya miezi) ilibidi dola ya kiislamu iwe na kalenda yake isiyokuwa na hayo.

Idadi na majina ya miezi iliyopo kwenye kalenda ya kiislamu ilikuwepo kabla ya kurasimishwa kwa kalenda ya Hijria, na namna ya kuhesabu siku katika mwezi pia ilikuwepo kabla. Tofauti tu ilikuwa hakuna number ya miaka kwa kuwa hapakuwa na hesabu ya miaka bali mwezi flani wa mfunguo flani (tarehe ya mwezi flani) bila ya reference ya mwaka.

Kuhesabu tarehe kwa gregorian kalenda sia makosa as long as dola iliyopo si ya kiislamu.
 
Watu wako busy na dini wakati Mungu mwenyewe Hana habari na dini zetu yuko busy na maisha yako unayoishi kama yanampendezq yeye na ya usafi Mungu kanuni zake za maisha haziiko that complicated ndio maana kwenye Matayo 5 :8 amesema heri wenye moyo safi ndio watamwona Mungu.Tafuta kuwa na Moyo safi na sio dini safi haipo na Mungu hakuwahi kuanzisha dini sisi sasa tunavyoqngaika nazo .Mimi naamini binadamu wote sawa ,Mungu ametupa nguvu ndani yetu kwenye universe ya kuwa na mamlaka ya kila kitu na kupendna basi hayo mengine ni shida za kutuleletea utengano tu hence moyo wako uchafuke.Mwaka mpya sherehekea ,uhuru wa Tz sherehekea ,kuzqliwa kwa Mtume sherehekea kuzaliwa kwa Yesu the same nothing will make you bad or good. Fanya kazi kwa bidii ,penda watu wote ikiwepo kusaidia wasiojiweza nk jinenee mambo mazuri ,kataa ubaya ndani yako ,usimwonee mtu ,usichukue cha mtu na kama umechukua mzudishie kwani hata ukiwa na dini ukitubu husamehewi mpaka urudishe au umwombe msamaha mhusika .Sasa wewe fia dini na utakuta wapagani wanaoishi kwa kanuni safi wanafanikiwa na watamwona Mungu
 
Kwani mleta mada labda sijakuelewa,unamaanisha kusherehekea kwa kupiga vigele gele au kitu gani maana me mwenyewe sijasherehekea au unamaanisha zile wishes kutoka kwa wadau wako ndiyo huzitaki?

Watu mnafanya maisha yawe magumu sana unashindwa nini kumjibu tu mtu kwa neno “Asante“ au ”na kwako pia” kisha uka-lock simu ukaweka mfukoni maisha yakaendelea?
Hii ni miaka ya kikafir
 
Huu mwaka siyo wetu...ni Mwaka wa Kikafir kabisa. Si kama kwenye Kalenda yetu.

Nashangaa naona watu wanatakiana heri na fanaka.
Acha Ukafiri wako mwaka ndiyo huo huo, kama una kalenda yako mbona hutumii katika maisha yako. Acha ku complicate mambo kisa tamaduni za Mwarabu zimemeza uwezo wako wa kufikiri.
 
Back
Top Bottom