Sitasahau ile siku niliyoachwa na aliyekuwa mpenzi wangu.nakumbuka kuna demu alinipa kazi niiprint t shirt yake ya birthday pamoja na kudesign poster ya birthday yake..Nikafanya kazi,akanilipa pesa yangu,nikamtumia kazi yake kisha nikaipost pia kwenye accounts zangu zote..
Nakumbuka hiyo ndy ilikuwa sababu ya kuachwa na mpenzi wangu,nilitumia kila mbinu kujitetea kwa Rose wangu nikamwambia Ile ni kazi Tu na nimelipwa alichonijibu ni Kwa nn yeye sijawahi kumpost hata siku moja lkn hawa 'malaya zangu' kila siku nawapost mitandaoni,amenichoka na hii Tabia ya umelaya