Je ni sahihi Mkude kuachwa kwenye Timu ya Taifa?

Je ni sahihi Mkude kuachwa kwenye Timu ya Taifa?

Kazitunayo

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2013
Posts
3,782
Reaction score
3,199
Sote tunajua kiwango cha Jonas Mkude wa Simba kilivyo msimu uu amekua na kiwango bora aana cha kushangaza kocha mkuu wa Staz ameamua kumuacha kwa sababu zisizoeleweka.
 
Hata mimi zamani nilikuwa nikijiuliza sana maswali kama hayo, mara nyingine alipokuwa anaitwa kwenye kikosi cha stars lakin bila kupewa nafasi ya kucheza hapo ndipo kichwa changu kilipokuwa kinajaa maswali tele, lakin baada ya kuanza kumfuatilia huyu mchezaji kwa ukaribu ndipo nilipogundua kwann hapewi nafasi kwenye kikosi cha starz.

Huyu mchezaji nadhani anacheza kiungo cha chini namba 6 na ni mjuzi sana wa kukaba lakin aina yake ya uchezaji sio ya kusukuma mashambuzi kwenda mbele, style yake ya uchezaji ni ya pasi fupi fupi, na ni mara chache sana kumuona yupo mbele timu inaposhambulia.

Hapo ndipo anapotofautiana na wenzake kama akina Frank Domayo na viungo wengine ambao wanaongeza mashambulizi pindi timu inapokuwa upande wa mpinzani.
 
Kaitwa Haruna Chanongo wa Stand United
 
Kama ni mzuri mbona mkia inachapwa kila kukicha?

Taifa Stars sio kikosi cha wachezaji wanaotamalaki kwenye kurasa za magazeti...
 
HAWEZI KUPATA NAFASI MBELE YA DOMAYO au TELELA au SURE BOY.
 
mkude huwa anafanya vizuri dhidi ya yanga tu....zaid ya hapo ni mchezaji wa kawaida tu
 
Mchezaji wa kupania mechi moja tu ya Yanga hana namba timu ya Taifa.
 
Huyu simjui mkuu, wa timu gani? nataka nianze kumfuatilia
Yanga africa,
Kijana anaujua mpira wa kila aina, nguvu, pasi fupi fupi, pasi ndefu yaani dogo ni jembe sana.
 
Watu kwa u-yanga na u-simba hamjambo

Mwalimu inawezekana ana malengo yake kumuacha huyu kiungo mkabaji...
Ila kwangu Mimi sio sahihi, kwani timu yenye mabeki kama Yondani, Nadir na Morris Mtu huyu ni muhimu, hasa ukizingatia timu ina watu wazuri wa pembeni kama Ngassa
 
Yanga africa,
Kijana anaujua mpira wa kila aina, nguvu, pasi fupi fupi, pasi ndefu yaani dogo ni jembe sana.

Mkuu ndo yule aliumia leo akatolewa dk za mwisho mwisho au leo hakucheza?
 
Mkuu ndo yule aliumia leo akatolewa dk za mwisho mwisho au leo hakucheza?
Yaaaaaaap!
Ndio yule mkuu, kijana anatisha sana, akicheza kiungo cha chini hata mabeki wanafurahi. Dogo anajua kukaba, anatumia nguvu, anapiga pasi ndefu ndefu za kupeleka mashambulizi mbele, Yaan dogo ni mtamu kama mcharo.
 
Kinacho muangusha Mkude ni kuhold mpira kwa mda mrefu na akija kuachia inakua ni square basi pia hapigi pasi ndefu za kuzid mita 10.
ukiwa kama namba six uwezo wa kupiga pasi ndefu sio zile za juu za kubutua hapana nazungumzia zile za chini au kitaa wanaita snake pass.
Pasi hizi ina maana unaitoa timu kutoka kwny defensive position to attacking.
Tujiulze kwanini Nditi alikua akiitwa mara kwa mara na hawa makocha wetu wa kigeni wanaokuja fundisha Stars.
Kwa io Mkude akiamua kujipa mazoezi binafsi humo ahhh panga pangua namba atapata tu.
 
wengi wamejadili kiushabiki ila kwa uwezo anaitajika taifa stars tatizo lake kubwa ni nidhamu kwani mara nyingi akiitwa alikuwa anachelewa kuripoti kambini pia kuna kipindi alikuwa anaandamwa na majeruhi kwa kiungo mkabaji Tanzania hakuna kama yeye
 
Mkude atakuwa yupo chimbo flani saa hizi anacheka kwa dharau
 
Sote tunajua kiwango cha Jonas Mkude wa Simba kilivyo msimu uu amekua na kiwango bora aana cha kushangaza kocha mkuu wa Staz ameamua kumuacha kwa sababu zisizoeleweka.
Mkude uwezo wake bado anatakiwa au imarishe yuko taratibusana, hauwezo wa kucheza mipira ya juu, mvivu kukaba ila anao uwezo wa kukaa na mpira tatzo uharaka hana. Mbaya zaidi hana nidhamu.Pale Simba mtu aliyekua akimfichia udhaifu ni Kotei.
 
Mkude uwezo wake bado anatakiwa au imarishe yuko taratibusana, hauwezo wa kucheza mipira ya juu, mvivu kukaba ila anao uwezo wa kukaa na mpira tatzo uharaka hana. Mbaya zaidi hana nidhamu.Pale Simba mtu aliyekua akimfichia udhaifu ni Kotei.

Uko sahihi. Hata fei toto naye leo alizingua tu mpaka alipotolewa na mwalimu Amunike. Kiukweli kama Taifa tunatakiwa tuwekeze tu kikweli kweli kwenye soka la vijana na pia kuwahamasisha wachezaji wetu watoke kwenda kutafuta changamoto mpya nje ya nchi badala ya kung'ang'ania Simba, Yanga na Azam.
 
Back
Top Bottom