Hata mimi zamani nilikuwa nikijiuliza sana maswali kama hayo, mara nyingine alipokuwa anaitwa kwenye kikosi cha stars lakin bila kupewa nafasi ya kucheza hapo ndipo kichwa changu kilipokuwa kinajaa maswali tele, lakin baada ya kuanza kumfuatilia huyu mchezaji kwa ukaribu ndipo nilipogundua kwann hapewi nafasi kwenye kikosi cha starz.
Huyu mchezaji nadhani anacheza kiungo cha chini namba 6 na ni mjuzi sana wa kukaba lakin aina yake ya uchezaji sio ya kusukuma mashambuzi kwenda mbele, style yake ya uchezaji ni ya pasi fupi fupi, na ni mara chache sana kumuona yupo mbele timu inaposhambulia.
Hapo ndipo anapotofautiana na wenzake kama akina Frank Domayo na viungo wengine ambao wanaongeza mashambulizi pindi timu inapokuwa upande wa mpinzani.