Je, ni sahihi Msando kujibu masuala ya diplomasia?

Je, ni sahihi Msando kujibu masuala ya diplomasia?

Ktk makosa ambayo kama taifa tutakuwa tumefanya ni kuruhusu hiyo barua kwenda kwa taifa kubwa kama USA, kwani badala ya kuponyesha kidonda ndiyo itazidi kukitia bakteria na kukifanya kuoza kabisa.

Msando ni nani kwenye uongozi wa kitaifa wa nchi hii?
Na Thadei Ole Mushi.

Nimeisoma Barua ya Msando yote aliyowaandikia USA.

1. Achana na Makosa ya Address aliyoyafanya Brother Msando twende kwenye Hoja nyingine za barua ya Msando. Kwenye barua ile kuanzia mwanzo Hadi Mwisho Msando kaonyesha kuwa hata Marekani huwa wanavunja haki za binadamu. Msando anataka kutuaminisha kuwa Marekani leo wakiamua Kula Kinyesi na sisi ni sawa kukila. Hakuna mahali ambapo Msando kaweza kusema Kama ni kweli haki za Binadamu zinavunjwa ama lah!... Kwa kifupi Msando anatuambia kuwa ni Kweli tumekiuka haki za Binadamu simply kwa kuwa Marekani nao wanazivunja.

2. Issue za Kidiplomasia hujibiwa Kidiplomasia na hupitia Chanel ambazo ni sahihi. Kilichofanywa na Msando ni kutaka kufurahisha watawala lakini akumbuke kuwa barua yake inazidi kuzorotesha uhusiano wetu na Marekani. Mh Kabudi sio mjinga kutafakari, Serikali kwa ujumla sio wajinga kutokumjibu Pompeo, wanatafakari kwa namna gani wanaweza kusulihisha mgogoro huu wa Kidiplomasia. Fani hii ya Diplomasia watu huisomea huwezi kukurupuka tu from no where mtu individual ambaye Hana taaluma hiyo kuanza kutuhumu mataifa Mengine. Kwa bahati mbaya kabisa barua ile copy yake ameielekeza kwa Rais wetu. Msando Hana tofauti na vijana waliovamia ubalozi wa S.A kudai Bombadia.

3. Msando naye kaingia kwenye Makosa yale yale kuwa naye anatetea ukiukwaji wa haki za Binadamu. Kwa maana hiyo Msando Siku akiwa Kiongozi hawezi kutuwakilisha Tena Marekani pamoja na washirika wake.

4. Serikali na hasa Rais hahitaji utetezi Sana anachohitaji ni Solutions, tunatetea Sana badala ya kutoa solutions. Barua ya Msando haitoweza kuitisha Marekani na Wala Marekani haitobadili msimamo kwa sababu ya barua ya Msando. Kwa maana hiyo bado tatizo linabaki na linaweza kukuzwa kwa barua hii ya Msando. Tumepoteza uwezo wa kutoa Solutions kwa sababu ya kusaka madaraka na Vyeo.

5. Kuna kasumba imeibuka kuwa ili uwe mzalendo Kila Jambo la Serikali ni la kutetea, nchi hii haiwezi kujengwa kwa kutetea makosa, nchi hii itajengwa kwa kuyaondoa makosa, kuambiana ukweli kuwa hili hapana lile sawa.

Wahenga walisema "two wrongs don't make a right". Narudi Jalalani..

Ole Mushi
0712702602

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza naunga mkono hoja.
Nchi yako inapochafuliwa na mabeberu ni jukumu la wazalendo kuitetea nchi yako.
Huo ndio uzalendo
Hakuijibia serikali, amejibu kama mwananchi Mzalendo.
P
Paschal wacheni siasa za maji taka na kupelekea kuichafua nchi yetu, kama ni uteuzi utapata tu na kama mungu hajakupangia kuupata uteuzi basi shukuru na uendeshe maisha yako kama ulivyo zoea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna kitu nakiona kipo. Mwananchi Msando sio mkurupukaji kuandika barua ile,Kuna msukumo wa nje wa kimbinu ukiachilia uzalendo ,huenda Kuna mpango unatengenezwa ili kujua km barua itajibiwa legally na mhusika ili kujua reaction yake upande wa pili itakuwaje. Hi Mimi kwangu naiita intermind confrotation techniques ambayo bado haijawa in reality form.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aongezwe kwenye listi ya ban kuingia USA hakuna kuchezea beberu
 
Kwenye mitaala ya shule zetu tangu primary hadi chuo Kikuu, tunapaswa tuwe na mtaala wa uzalendo ili Tanzania tuzalishe wasomi wazalendo badala ya kuzalisha wasomi mamluki.
P
Wazalendo usimama na pompei kupinga uzuiaji Wa haki ya kuishi
 
Hapana brother, katika hili Hapana, kuna mtanzania hajui kuwa kuna mahali tumejikwaa? Tumesaidiwa kuabiwa kuwa tuko uchi!
Sisi wazalendo tumeshindwa kuusema ukweli huo.
Tunaogopa tutamkosea Tanzania,kumbe tunaogopa vivuli vyetu wenyewe.
Tanzania Analia uchungu wa mama alie poteza mwanae mpendwa.
Je ni uzalendo kumfariji kwa maneno matam kuwa mama nyamaza usilie Sana kwani mtoto mwenyewe alikuwa haramu!
 
Back
Top Bottom