Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 1,679
- 2,123
Kimaandiko, kujiita "Kiboko ya Wachawi" sio sahihi kwa sababu inahamasisha kiburi na kujitwalia mamlaka ambayo ni ya Mungu pekee.
Sababu za Kimaandiko:
Yesu ndiye anayeangamiza kazi za shetani
1 Yohana 3:8 – "Kwa sababu hii Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Shetani."
Yesu ndiye mwenye mamlaka ya kuharibu kazi za shetani.
Hata wanafunzi walipopewa mamlaka ya kutoa pepo, waliambiwa watafanya hivyo kwa Jina la Yesu, sio kwa nguvu zao.
Marko 16:17 (SUV)
"Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo, watasema kwa lugha mpya."
Luka 10:17
"Na wale sabini na wawili wakarudi kwa furaha wakisema, Bwana, hata pepo wametutii kwa jina lako."
Kwa Maandiko hayo tunaona kuwa ushindi dhidi ya wachawi na nguvu za giza unatokana na uwezo wa Jina la Yesu, sio nguvu za mtu binafsi. Hivyo ni bora tukawa wanyenyekevu kuliko kujitukuza na kujipa majina makubwa.
Yakobo 4:6-7 – "Mungu huwapinga wenye kiburi, bali huwapa wanyenyekevu neema..."
Badala ya mtu kujiita "Kiboko ya Wachawi," afadhali aseme:
"Mimi ni mtumwa wa Yesu Kristo au mimi ni mtumishi wa Mungu aliye hai."