Je, ni sahihi Steven Mbazi kusimamia mali za Bilionea? Tumpe ushauri DC Jerry Muro katika utatuzi wa sakata hili la mali

Nimekusoma mkuu ila hii kesi imekaa kama ila ya sharifu ngoja tuone mahakama itatoa hukumu gani
hapana labda Kesi (Miriam) imekaa km ya Chusa kule Hospitalini Baraa alipowekwa akiwa ana kesi ya Mada alipanga na Sharif aliyekuwa na hasira za kuzidiwa utajiri
Jua Kesi ya Mauaji ya Dada wa Bilionea iimekosa muuaji(muuaji atatoka km Chusa hata kwa chonee)
nambie hapo Kesi imesimama
Hakimu kesi ya mke wa bilionea Msuya ataka muda zaidi kusikiliza mashahidi

  • Mtanzania
  • 20 Jul 2019
  • Na KULWA MZEE -DAR ES SALAAM
-PICHA: IMANI NATHANIELMAHAKAMANI: Aliyekuwa mke wa bilionea Msuya ambaye ni marehemu, Miriam Mlita, akielekea Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam jana kusikiliza kesi ya mauaji inayomkabili.
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imesema ili kuwepo usikilizaji wa haki katika kesi ya mauaji inayomkabili Miriam Mrita, mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya na mwenzake, inahitaji muda wa kutosha ili mashahidi 45 wa Jamhuri na wale wa utetezi wote wasikilizwe.
Hayo yalisemwa jana na Jaji Sekela Moshi, wakati akiahirisha kesi hiyo kwa sababu mbalimbali, ikiwemo siku mbili zilizopangwa kusikiliza shauri hilo kuwa hazitoshi.
Akiiwakilisha Jamhuri, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mkunde Mshanga, alidai shauri lilikuja kusikikizwa, lakini wazee wa baraza ambao kisheria wanatakiwa kuwepo hawapo.
Alidai pia Jamhuri inasikitika mashahidi wao hawajapewa hati ya wito wafike mahakamani kutoa ushahidi, hivyo aliomba mahakama itoe wito wafike.
Jaji Moshi alisema kesi hii isingeweza kuendelea, ilipangwa siku mbili ambayo ni jana na Jumatatu, lakini kuna mashahidi 45 wa Jamhuri, bado mashahidi wa upande wa utetezi.
“Tumeona ili tuwe na usikilizaji wa haki, mashahidi wote wasikilizwe, hii kesi inahitaji muda zaidi, tutaiahirisha hii kesi ili tuipangie muda wa kutosha.
“Kesi itaendelea wakati mwingine kwa tarehe itakayopangwa na Naibu Msajili, washtakiwa wataendelea kukaa rumande,” alisema.
Mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni Revocatus Muyella.
Wanadaiwa Mei 25 mwaka 2016 katika eneo la Kibada Kigamboni, walimuua kwa makusudi Aneth Msuya ambaye ni dada wa Bilionea Msuya.
 
Hotel inabiashara kubwa sana msimu wa utalii kuna kampuni nyingi za utalii zinalaza wageni pale,kuna kampuni ya climbkili inalaza wageni hapo wa kutosha mana ni kampuni kubwa
Sawa kwa kodi za anko Magu ni nyingi sana
 
Ukwaju hii kesi hatoki mtu hukumu inampeleka,aliehusika na huyo mama ni mshkaji na alikua na maisha yake ila alipopoteza kazi ndio akawa mishentwn.ndio kukutana na huyo maza na kupanga unyama wao.
Kuna jamaa mwingine alishikwa pamoja nao anaitwa magoma yeye aliachiwa mana hakua anajua chochote na ndio anatupa story kua maza mhusika mwanzo mwisho
 
hukumu inampeleka,aliehusika na huyo mama ni mshkaji na alikua na maisha yake ila alipopoteza kazi ndio akawa mishentwn.ndio kukutana na huyo maza na kupanga unyama wao.
Kuna jamaa mwingine alishikwa pamoja nao anaitwa magoma yeye aliachiwa
sawa Mkuu lkn ukizungumzia Hukumu kabla ya upelelezi mnakosea, huyu Mama kapanga mipangilio ya mauaji ndio maana kuna MANSLAUGHTER na MURDER upelelezi kwa DPP bado, mara ya mwisho ilikuwa Julai mwaka huu leo November
kwenye RED km huyu mshikaji kawataja waliokamata kisu na kuua au aiwashuhudia pale chumbani wameshakamatwa basi hukumu ipo na jamaa yako na Mke wa Bilionea hawahusiki wao wataambulia kifungo na wakitoka watarejea Uraiani na Mama akaendelee na usimamizi wa mirathi. Nionavyo mm il revenge itakuwepo tu kwa watu hawa mpaka akosekane mshindi
 
Murder is defined as killing somebody with “malice aforethought,” which is malice. The two types of malice is “express malice” and “implied malice.” Express malice is when a person intended to kill another person or persons. Implied malice is when a person intentionally commits an act they knew was dangerous to other people and human life resulting in death. In other words, the murder was committed with a conscious disregard for human life.
If a crime involves expressed or implied malice its defined as “murder.”
 
TANMOJA Nimekubali ila hukumu yake ni ipi? maana hizi Sheria nyingi za lugha za kigeni
Lakini Mueder kwetu naona wengi wanapangua nikirifaa Kesi ya Asha Mkwizu na Zombe na kwa wenzetu USA wanazaidi ya aina 52 na Murder
Mm nasubiri km unayo Hukumu ya hii Kesi ya Mke wa Bilionea kwa faida ya wote ingawa hatuingilii upelelezi
 
Kisasi huwa kinatambaa...

toka erasto hajafa huyo aneth alikuwa haelewani na wifi yake...
Erasto na mdogo wake inazungumzwa kuwa walikuwa
" wakipendana sana yaani!"
 


Maza yupi muhusika kwenye yapi ya mwanzo mwisho?
 
Kimsingi upande wa baba ndiyo ndugu halisi na chimbuko la watoto.
 
Mara nyingi upande wa baba huwa wapo busy na mambo yao. Ila familia ya Erasto inaonekana kuwa ya kueleweka zaidi kuliko ya Mrita.
 
Uku Tanganyika atufati sheria za dini , Tunafata sheria za jamuhuri ya muungano wa Tanzania, ata ndoa za kiislam wakigombana au kutallikiana kama mmoja wapo ajalizika ukimbilia mahakani ya hakim mkazi, nasiyo mahakama za kadhi.
Kaulize vizuri mahakamani.sheria ya dini inatumika,ninyinyi tu ndio munachagua mugawe mali zenu kwa sheria ipi.kuna ya dini na ya serikali na yakimila.mimi ni shahidi ktk hili tumegawana milathi yetu kwa sheria ya kiislamu ktk mahakama ya magomeni hapo drs
 
Aisee! Mali hizi!
 
Hii kesi mama atahukumiwa kwa kupanga mauaji,hata aliemuua erasto alihukumiwa kwa kupanga mauaji yani kudhamini watu waue na kuwalipa
 
Main character wa sakata lote hilo ni mtoto wa kiume wa
marehemu.
Huyo kijana atafutiwe councelor au lawyer ili amshauri aache ulevi na kutegemea hao wajomba na wafilisi wengine.
Ajitahidi kumsomesha dada yake na ndg zake ili wawe na msingi mzuri.
Ajiepushe na magomvi na beef za kifamilia.
Ajiunge chuo asomee BManagement ili awe nguzo ya familia hiyo, ajitambue asibebwe kama kiwete.
Asimwamini saana huyo mama yake na mjomba, kama alimchinja shangazi yake hashindwi lolote.
Arudi kwa Babu Msuya apate ushauri mzuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…