Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 6,238
- 8,194
Swali langu ni hilo kwenu nyinyi mnaoshangilia na kuruka ruka mnaposikia Israeli imewapa vipondo majirani zake. Naomba mnipe majibu yenye msingi wa Maandiko.
Mimi Biblia yangu inanikataza kufurahia vita na mauaji na badala yake inanihimiza kuombea amani na kuwa mpatanishi.
"Heri wapatanishi, maana hao wataitwa wana wa Mungu." — Mathayo 5:9
"Usishangilie kuanguka kwa adui yako; usifurahie moyoni mwako kujikwaa kwake..." — Methali 24:17
"...Nawasihi muombe dua, msali na kumshukuru Mungu kwa ajili ya watu wote, kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, ili tupate kuishi maisha ya utulivu na amani pamoja na uchaji wa Mungu na mwenendo mwema. Jambo hili ni jema na lampendeza Mungu Mwokozi wetu, ambaye anataka watu wote waokolewe na wapate kuujua ukweli." — 1 Timotheo 2:1–4
"Sifurahii kifo cha mtu yeyote. Hivyo tubuni ili mpate kuishi. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema.” — Ezekieli 18:32