mr.chengachenga
Senior Member
- Mar 6, 2014
- 155
- 104
Habari za muda huu wadau wa JF.
Naomba niende moja kwa moja katika hoja.
Wote tunajua kuwa sasa hivi nchi inapatwa na janga kubwa sana la corona ambalo limepelekea uchumi wa sekta mbalimbali kuyumba.
Leo nimeshtushwa sana baada ya kuona kuna shule flani ya private inalazimisha wafanyakazi wake (walimu) wa-sign fomu za likizo zisizo na malipo, jambo ambalo ni kinyume na utaratibu.
Natamani kutambua kutoka kwa wataalamu wa sheria kuwa hii kitu inakuwaje maana wengine ni dada zetu huko wana kaelimu kao ka kufundisha na sio wajuzi wa sheria na hivyo kujikuta wakinasa katika huu mtego. Je, kisheria ipo namna ya kumsaidia aliyekwisha ku-sign?
Sasa huu unaonekana kama ni wizi maana walimu wanapewa likizo pasipo malipo na ada kwa wazazi watalipa yote pasipo kupunguziwa hata senti.
Je, vipi kuhusu taratibu za usajili wa shule, hua hawazingatii amount ya pesa katika account mwanzilishi ili mambo kama haya yanapotokea waweze kukabiliana nayo?
Leo unampa mtu likizo isiyo na malipo halafu yeye ataishi vipi kwa kipindi hiki kigumu cha haya maisha?
Naomba serikali ichunguze sana hizi taasisi maana naona kuna baadhi zinafikiria kuumiza watu kwa kisingizio cha corona na huku walikubaliwa kuendesha shule hizo kwa kuwa walionekana wamekidhi vigezo na wanajiweza. Ni bora shule ingeingia makubaliano ya kuwalipa wafanyakazi kwa kuchelewa na sio kudhulumu haki zao kwa kuwalazimisha ku-sign likizo zisizo na malipo (huu ni utapeli)
Niliona ujumbe wa chama cha walimu wa shule binafsi kuwa kinafuatilia haki za walimu wa shule hizo binafsi hasa kipindi hiki lakini sijaona mrejesho na sijui wamefikia wapi, wanapaswa kutambua na hili pia.
Ngoja nikamshawishi mhusika nikifanikiwa nitaweka hapa copy ya mikataba yao ya wizi hiyo ya likizo pasipo malipo ila nitafuta au kuficha jina la muhusika.
This is too much!
Karibuni wakuu kwa mawazo huru.
Asanteni sana