Je ni salama sasa kuifadhi fedha katika benki za ndani Tz?

Je ni salama sasa kuifadhi fedha katika benki za ndani Tz?

Rutunga M

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2009
Posts
1,769
Reaction score
1,390
Wana bodi.
Nafikiri kila mmoja amesoma na kusikia taarifa ya BOT baada ya kufungia benki 5 kwa kushindwa kufikia mtaji wa Bilioni 2 kulingana na sheria zao.

Kilichoshangaza wengi ni kuwa wateja waliokuwa na fedha ndani ya benki husika zaidi ya sh 1.5milioni nao wamefilisiwa na BOT kwa kuwa benki yao imefilisika.

My take.
1:Mimi nilifikiri BOT ndiyo dhamana ya wateja iwapo benki inafilisika lakini kumbe si kweli maana benki zilizobaki nazo zikifilisika nawe umefilisika. Hii ikoje?

2:Je wewe ulikoifadhi fedha zako unajua mtaji wa hiyo benki? Je unajua lini itafilisika? Fedha zako ziko salama?
Karibu kwa mjadala
 
Zangu naweka kwenye mpesa mkuu maana pogba wa tz kashaua uchumi
 
Chakushangaza zaidi ya yote hapa ni BOT kulipa dividends kwa kutumia retain earnings pamoja na faida yote. Kwanini wasingelitowa hizi pesa kwa ajili ya kuziokowa hizi bank zilizofilisika kama ruzuku au ata additional capital ili kutowa msukumo katika uchumi kama injections. Eti BOT kuna wasomi sijaelewa.
Tunaona mifano nchi kama China inavyotowa pesa zake kwenye central bank na kuziingiza katika long term investments. Sie hapa bongo tunagawana faida yote na malimbikizo ya faida ya miaka iliopita. Hawa wasomi wetu hapa wanatupeleka siko. Angalia kina Prof Lip anavyotumika, Dr. Silahaaaaa ya maangamizi
 
wewe unaonaje ? fanya kile moyo wako unachoona ni sahihi
 
Hapa nafikilia nikatoe mpunga wangu wote nifungie gheto mana ningekuwa customer wa hzo benki nadhan now ningekuwa ICU
 
Hata chiz hawezi kuwa na imani na local banks zetu.
 
Back
Top Bottom