Salaam,Shalom!!
Ndugu mmoja akapita Kwa jamaa zake katika eneo alilokuwa akifanyia biashara, akawashirikisha kuwa amepata mchumba na ataoa hivi karibuni, hivyo anaomba michango Kutoka Kwa wadau.
Jambo Hilo likawa kheri masikioni mwa Rafiki zake. Ndugu huyo, akachangisha michango pesa nyingi sana na kuahidi kuleta kadi ya harusi Kwa wote waliochangia.
Ilipobaki wiki Moja kabla ya tarehe ya harusi ndugu muoaji aliyoahidi wachangiaji, alisafiri na kupotea kusikojulikana Kisha akaja kuonekana baada ya miezi miwili kupita,
Alipohojiwa kuwa kwanini hakuleta kadi za harusi Kwa wachangia harusi kama alivyoahidi, alijibu kimkato kuwa mchumba alibadili maamuzi hivyo ndugu muoaji akaamua kutumia pesa aliyokusanya kama michango kuongeza mtaji wa biashara yake.
Kwa kuwa wachangiaji, hawakulazimiashwa Kutoa michango, waliishia kuguna na kufyonza na kununa!!!
Nakifananisha kisa hiki na watia nia wanaokusanya michango ilhali " UCHAGUZI"Bado.
Cc: Lucas Mwashambwa na johnthebaptist
Karibuni🙏