je ni sawa kukatwa NSSF wakati wa kipindi cha probation miezi 3???!

je ni sawa kukatwa NSSF wakati wa kipindi cha probation miezi 3???!

muhandu

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2011
Posts
311
Reaction score
83
naomba kufahamu kama ni sawa kukatwa hela ya nssf wakati nipo kwenye kipindi cha matazamio.nimepata nafasi ya kufundisha shule fulani ndiyo mwenye shule kanimbia hivyo.wataalamu naomba kufahamu.
 
Ni sawa, kinachotakiwa uwe umejiunga na huo mfuko na pesa zako zinapokatwa zipelekwe huko.
 
samahani kama nitakuwa sikueleweka,ni uungwana kama nitakuwa nimekwenda tofauti na mawazo yako nakutaka radhi kwa maudhi.kilichonifanya niulize ni kuwa sina hata hiyo namba ya nssf na wala sijajiunga na fedha inakatwa je itakuwa inakwenda wapi ?hata hivyo nashukuru sana kwa majibu.
 
Ni kweli ukiwa probation, michango inakatwa!

Cha msingi andika official letter kumjulisha account namba yako katika mfuko husika. Iweke katika kumbukumbu zako. Kama hujajiunga fanya hivyo.

Then after 3months nenda mfuko husika, ulizia michango yako. Wao ndio wana wajibu wa kufuatilia.

Indapo utakuachisha kazi, barua uliyomlima itakuwa kama kielelezo katika usuluhishi wa mgogoro kwa CMA.
 
samahani kama nitakuwa sikueleweka,ni uungwana kama nitakuwa nimekwenda tofauti na mawazo yako nakutaka radhi kwa maudhi.kilichonifanya niulize ni kuwa sina hata hiyo namba ya nssf na wala sijajiunga na fedha inakatwa je itakuwa inakwenda wapi ?hata hivyo nashukuru sana kwa majibu.

Na maswali yake mbona hujajibu?
 
Unapoajiriwa makato yafuatayo ni lazima
1. Kodi (kama mshahara wako au posho yako iko juu ya kima cha chini)
2. Hifadhi ya Jamii (N.S.S.F, GEPF, PPF, LAPF au PSPF)
3. Bima ya afya (kutegemeana na utaratibu wa sehemu husika). Kama Mwajiri wako anakugharimia matibabu au unajigharimia mwenyewe hiyo ni habari nyingine lakini
Haya matatu huhitaji kujsajili kwanza ni sehemu ya ajira yako.

Kukuongezea tu maarifa ni kwamba N.S.S.F ni hela yako ya baadaye, wewe unalipa 10% na yeye (Mwajiri) 10% (au zaidi kulingan na utaratibu) kama hujakatwa maana yake wewe ndio utakayepunjiaka as hutapata hela ya mwajiri wako utakapomaliza mktaba wako.
 
....kwa taratibu za NSSF ili uanze kukatwa makato ni mpaka uwe tayari umejisajiriwa kwenye mfuko huo wa hifadhi ya jamii; ili ijulikane kuwa umesajiriwa ni mpaka ujaze fomu ya njano(yellow form) inayotolewa na NSSF na kupatiwa akaunti namba. Kinyume na hapo Mwajiri hawezi kukukata makato hayo...kwani atakua hana pa kuyapeleka. Ila kwa waajiri ambao wako smart taratibu zote hizo wanazifanya mapema na siku ya kwanza unapo report kazini basi unajaza hizo fomu kisha zinapelekwa NSSF na hapo utalazimika kukatwa mwisho wa mwezi.
 
nashukuru kwa ushauri kwani kuna mambo ambayo sikuwa nayajua nawatakieni baraka tele wote mliochangia.nayafanyia kazi maoni yote.
 
Back
Top Bottom