Je ni sawa kuwaamni madaktari 100%

ubongokid

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Posts
2,154
Reaction score
4,184
Wadau;
Nimewahi kwenda katika hospitali na kuandikiwa vipimo pamoja na dawa na wataalam wa tiba.Sina shaka na uwezo na utaalamu wao bali ninahoji iwapo ni busara kufanyan background check kwa tiba au maelekezo unayopewa na dakatari.

Kwa mimi bainafsi nimekuwa na tabia ya kusoma mitandaoni na vitabu mbalimbali vya tiba kuhusu ugonjwa,dalili au tiba yoyote ninayopitia au inayohusu mwanafamilia wangu na mara nyingi nimeona niko sahihi kwani imenisaidia.Kuna wakati huwa narudi kwqa daktari na kuhoji kwa nini amanipa dawa fulani badala ya dala fulani ukizingatia madhara ya dawa hizo na wakti mwingine gharama ya tiba hizo.

Ningependa kujua tu kama ni utamaduni mzuri ili nihamisishe wengine wawe na utaratibu wa kuelewa tiba wanazopewa na madaktari wao
 
Ki utarabu tunapaswa kuwaamini kutokana na kwamba wao ndio wenye mamlaka na utaalamu, ila wengi wanatumia mamlaka yao vibaya nakuweka hali ya pesa mbele bila kujali hali ya mgonjwa,

Wanaweza kujua kabisa kuwa dawa fulani ni bora kwako lakini tu kutokana na hali ya pesa basi watakupa nyingine hata kama inaweza kuwa na adhari wako baada ya kukuponya na ugonjwa,
 
Hakuna haja ya kuwaamini kwa 100% tuwetuna fanya viutafiti vyetu tu ilikujiridhisha kwa baadhi ya mambo ambayo tuna tilia mashaka.
 
Tunapaswa kumwamini tu kwa 100 % madaktari wetu ..maana hicho unachokisoma na kupata hoja za kuhoji huenda sio sahihi ...kumbuka kuwa daktari anapokuwa anafundishwa taaruma hiyo hasomi ugonjwa moja kwa moja kama usomavyo wewe ..ataanza na bio medicals kama pathology, pharmacology , microbiology nk..hivyo anapokuja kusoma hizo clinical subjects anakuwa na uelewa mpana mno wa hayo magonjwa...jinsi yanavyo tokea (pathophysiology) ,visababishi ..tiba yake na jinsi dawa husika inavyofanya kazi (mechanism of action) , hivyo anafahamu akupatie dawa gani kutokana na nature ya ugonjwa wenyewe ...na madaktari sio kwamba wanatibu tu..bali hutibu kwa hufuata miongozo mbalimbali ..mfano tanzania hutumia STG (standarnd treatment guideline) pia miongozo ya WHO hutumika...ingawa wanafundishwa pia respect of autonomy (The right of patients to make decisions about their medical care without their health care provider trying to influence the decision.)...ila naona si sahihi mgonjwa kujichagulia dawa ya kutumia ...
 
Mkuu, Mimi ni Kama wewe, Sina imani kabisa na hawa madaktari Wetu,
Mara nyingi huwa najitahidi kujisomea nalala za afya na tiba ili kujiongezea ufahamu zaidi.

Kutoka na na kufahamu kwangu baadhi ya dawa,magonjwa na matibabu, Imeniongezea kujiamini hasa nikutanapo na hawa madaktari.

Nashukuru naweza kumtambua daktari asiye na vigezo kwa haraka kutokana na maongezi tu
 
Kweli mkuu ni muhimu wa kujijengea utamaduni wa kujisomea. Madaktari hasa wa Tz si wa kuwapa asilimia 100%.
Nimeshashuhudia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…