Ni kweli maeneo mengi huwa inafanyika kinyume na Sheria.
Na huu ni udhaifu wa kimfumo.
Ilitakiwa hawa wenyeviti walipwe hata kama wamegombea wenyewe.
Mbona Diwani analipwa, Mbunge analipwa, waziri na Rais analipwa na wao si wachaguliwa?
Kwanini huyu Mwenyekiti wa mtaa asilipwe na ndiye anaeweza kuwa anafanya kazi nzito katika mazingira magumu yasiyo na nyenzo wala kuwezeshwa kuliko hao wote juu.
Kwahiyo yanayofanyika ni Makosa, na endapo ukiwa na ushahidi madhubuti unaweza kuripoti Takukuru na akashtakiwa.
Lakini tambua mazingira yao halisi ya utendaji Kazi wao na mfumo uliopo nchini.