Kuna wakati unamsikiliza kiongozi mkubwa wa serikali akiongea hadharani, unalazimika kushika kichwa na kujiuliza: hivi hawa watu huwa wanasoma hata vile vitabu wanavyoviasaini au huwa wanaongea kwa mihemko na jazba???
Hicho ndicho unachokipata ukimsikiliza Waziri wa mambo ya ndani ya nchi akijitahidi kwa nguvu zote kufafanua kwa ujasiri mkubwa jambo asilolijua, akidai kuwa Kitambulisho cha Taifa si taarifa binafsi bali ni "Public" kwa sababu tu raia wanapiga fotokopi wanaponunua viwanja au kusajili laini za simu.
Ni kauli inayofichua pengo kubwa la uelewa kati ya viongozi wetu.
Mheshimiwa Waziri anahitaji kusaidiwa shule ndogo ya msingi (na ikiwezekana apelekwe semina elekezi) kwa sababu hizi hapa:
1. Waziri anapingana na Sheria ya Nchi.
Ni aibu kubwa kwa kiongozi wa ngazi ya uwaziri kusimama na kupigilia msumari hoja inayopingana moja kwa moja na Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya Mwaka 2022 iliyotungwa na Bunge.
• Sheria Na. 11 ya 2022 iko wazi kabisa: Taarifa binafsi ni alama yoyote inayomfanya mtu atambulike. Namba ya NIDA (NIN), tarehe ya kuzaliwa, na picha yako vinamtambulisha mtu mmoja tu mahususi.
• Kama Mheshimiwa haelewi hata sheria za serikali anayoitumikia. Hilo ni suala la aibu kwa Taifa kuwa na viongozi wa namna kama yake.
2. Kuchanganya "Matumizi ya Lazima" na "Mali ya Umma"
Waziri anadhani kwa sababu tunapiga fotokopi vitambulisho vyetu kila siku, basi data hizo zimeshakuwa mali ya kila mtu na yeyote anaweza kuzichezea. Huu ni uelewa wa kiwango cha chini sana unaofaa kujadiliwa kwenye vijiwe vya kahawa, si kwenye vyombo vya habari vya taifa.
• Tunapotoa fotokopi ya NIDA kwa wakili au kampuni ya simu, hatuzigawi taarifa hizo ziwe mali ya umma; tunatoa ridhaa yenye masharti maalumu (conditional consent) kwa ajili ya huduma hiyo tu.
• Ndio maana kuna Wakala wa Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) nchini. Kazi ya wakala huyu ni kuhakikisha wale mawakili na makampuni ya simu wanazilinda zile fotokopi kama siri kubwa. Kama taarifa hizo zingekuwa za "umma" kama anavyodai Waziri, kusingekuwa na haja ya kuwa na chombo cha kisheria (PDPC) kinachotumia kodi za wananchi kulinda kitu ambacho "si binafsi."
3. Hatari ya Kiusalama: Kuhalalisha Wizi wa Utambulisho (Identity Theft)
Katika karne hii rasilimali yenye thamani na hatari zaidi ni data (Data is the new oil). Kauli ya kiongozi mkubwa kudharau usalama wa taarifa binafsi, hii ni hatari sana.
• Siku mhalifu akitumia hizo taarifa za "umma" kughushi akaunti ya kitapeli kwa taarifa zangu. Je huyo katambi atakuja mahakamani kunitetea kuwa taarifa hizo hazikuwa zangu binafsi???
Waziri anapaswa kurejea kwenye maandiko ya sheria za nchi, na asahihishe kauli hii ✊️✊️
Kauli hii ya ovyo inapaswa kufutwa mara moja, na Mheshimiwa Waziri anapaswa kujifungia ofisini kwake na kusoma sheria za nchi kabla hajasimama tena mbele ya vipaza sauti na kutuaibisha kama taifa.
Msisahau kwamba ndo huyu huyu aliyetutangazia hali ya hatari nchini na kumpa maagizo IGP 😆😆😆.
YAANI INATIA MPAKA KINYAA🤧