Je ni sawa na halali kuliita bunge hili la 2025-2030 Bunge Tukufu?

Je ni sawa na halali kuliita bunge hili la 2025-2030 Bunge Tukufu?

Superbug

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
16,583
Reaction score
42,992
Wote tunajua maana ya neno Tukufu kwamba ni kitu kisafi chenye hadhi ya utakatifu. Rais Benjamin William Mkapa alikataa asiitwe mtukufu rais kwakuwa alijua hadhi na upekee WA neno Hilo.

Sasa swali langu ! Wote tunajua namna bunge hili lilivyoingia madarakani asilimia 99% ni mafia style na wizi wa kura kiufupi ni bunge la kijambazi.

Sasa je ni sawa na halali kuliita bunge Tukufu? Kweli linastaili hadhi ya utukufu? Naomba swali hili walijibu wabunge wenyewe ambao tunaamini wana dini na shamira zinazowasuta ndani Kwa ndani je kweli wao ni watukufu? Na hilo Bunge lao ni Tukufu? Karibuni tujadili utukufu wa bunge letu.
 
Mule hakuna Muwakilishi wa wananchi.
Wale wote ni wawakilishi wa CCM
Kazi yao ni kuitetea CCM
Kumshabikia Samia
Kuitetea Selikali.
Uchawa nk

Wabunge karibu wote hawajui kazi za Kibunge (policy, sheria,Budget)

Wengi wao ni wapumbavu sana.
Tuna Bunge Dhaifu sana.
 
Bunge tukufu, mapinduzi tukufu na mtukufu rais ni lugha ya hovyo sana ya CCM za kujimilikisha ukuu. Hata kwenye nchi zenye uongozi bora sana duniani za Ulaya, Japan, Canada na Korea Kusini hawaiti hayo mambo matukufu.
 
Alafu wale watu ni Wadhambi mno
1.Waongo mno.
2. Wanakufuru kwa kuapa Uongo na kudanganya.
3.Wasingiziaji.
4. Wanafiki.
5. Wauaji.
6. Wapo Radhi kupindisha shria na katiba kwa maslahi yao binafsi

Wale Binadamu wote waliomo Mulehawafai kwa Mustakabali wa Tanzania

NCHI ILIPOFIKA PANATISHA SANA.
 
Yani jambo la kijinga na la mateso Kwa wananchi wao watasema ndioooo huku wanapiga MEZA. Binafsi lile bunge ni kama kikao Cha wachawi.
 
Since 2020 hii nchi haijawahi kumiliki bunge lililotokana na matakwa ya wananchi. Hivyo badala ya kuitwa bunge tukufu, liitwe bunge kibogoyo.
 
Wote tunajua maana ya neno Tukufu kwamba ni kitu kisafi chenye hadhi ya utakatifu. Rais Benjamin William Mkapa alikataa asiitwe mtukufu rais kwakuwa alijua hadhi na upekee WA neno Hilo.

Sasa swali langu ! Wote tunajua namna bunge hili lilivyoingia madarakani asilimia 99% ni mafia style na wizi wa kura kiufupi ni bunge la kijambazi.

Sasa je ni sawa na halali kuliita bunge Tukufu? Kweli linastaili hadhi ya utukufu? Naomba swali hili walijibu wabunge wenyewe ambao tunaamini wana dini na shamira zinazowasuta ndani Kwa ndani je kweli wao ni watukufu? Na hilo Bunge lao ni Tukufu? Karibuni tujadili utukufu wa bunge letu.
Sio sawa! Ni Bunge haramu. Punto.
 
Back
Top Bottom