Je ni sawa polisi kumwapisha mtu.

Je ni sawa polisi kumwapisha mtu.

tisa desemba

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2011
Posts
434
Reaction score
115
Wadau, leo asubuhi nikiwa mtwara stendi kwenye bus la sumry kabla ya safari ya kuja dar kuanza, aliingia ndani ya bus askari mwenye cheo cha koplo akajitambulisha na kuanza kutoa maelekezo kwa abiria kama umuhimu wa kufunga mikanda, umuhimu wa kuandika majina halali kwenye tiketi, namba za dharura endapo kutakuwepo na ukiukwaji wa sheria za barabarani n.k

ghafla
, akasema sasa ni wakati wa dereva kula kiapo mbele yangu na ninyi abiria.

dereva akaanza, mimi (akataja jina) dereva wa bus la sumry lenye namba T......ABD, naapa kwamba nitaendesha bus kwa kufuata sheria na taratibu zote za usalama barabarani na ninaahidi kutoa ushirikiano na msaada kwa abiria wangu wakati wote wa safari, safari yangu itapitia mikoa ya mtwara, lindi, pwani na dar es salaam, eeh Mwenyezi Mungu naomba nisaidie.

JE HII NI SAWA KISHERIA.
 
Wanazuoni wa sheria watakujibu ila mimi nadhani alikuwa akifanya joke na kuendeleza ulinzi shirikishi. Alihitaji dereva awe sehemu ya nyinyi. Kwani huyo muapaji alishika biblia, Quran, au nini? Usukani?
 
Mtu mwenye mamlaka ya kuapisha ni mwanasheria mwenye power ya 'attorney' huyu ni wakili. Pia state attorney anaapisha...mahakimu wote wanaapisha. Ila ktk kesi za kuapisha wanasiasa wanapochukua form za uchaguzi, mwenye jukumu hilo ni hakimu pekee, awe hakimu wa primary court or RMC.
 
Back
Top Bottom