Je, ni sawa wananchi wa Ngorongoro kuhamishwa?

Joined
Feb 8, 2019
Posts
94
Reaction score
124
JE NI SAWA WAKAZI WA NGORONGORO KUHAMISHWA..?

Na Thom munkondya.
Kwa mujibu wa sheria zetu za ardhi,mtu yoyote au mmiliki yoyote wa ardhi katika eneo lolote la nchi yetu awe na hati miliki au asiwe na hati miliki anaweza kuondolewa kwenye ardhi yake kama tu jambo linalofanywa au linalotakiwa kufanywa kwenye hiyo ardhi lina manufaa kwa umma.

Sasa manufaa ya umma ni yapi..? Huu unaweza kuwa ni mjadala mwingine. Lakini sheria haijatoa tafsiri ya moja kwa moja ya nini maana ya manufaa kwa umma ila imeorodhesha baadhi ya manufaa ya umma kama;
1)matumizi ya serikali.
2)miradi ya serikali.
3)kilimo
4)viwanda
5)Mahitaji mengine ya jamii(barabara,hospital nk)
6)biashara na madini

Vile vile kipengere cha 4(2) kimempa rais mamlaka ya kulipa ardhi shirika au kampuni kwa mtazamo wake pale atakapojiridhisha na kuona kama inafaa hilo kampuni kupewa kwaajili ya ujenzi wowote ambao utakuwa ni kwa matumizi ya wote au jambo lenye kuleta manufaa kwenye uchumi wa nchi.

Na zoezi hili la utwaaji wa ardhi sio la hiyari ni la lazima(compulsory land acquisition) kwasababu ardhi nchini Tanzania sio mali binafsi ni mali ya umma inayosimamiwa na serikali chini ya rais ambaye ndiyo msimamizi mkuu au mdhamini. Kwa kifupi nchini Tanzania watu wote sisi ni wapangaji kwenye ardhi na mwenye ardhi ni rais(baba au mama mwenye nyumba) ndiyo maana huwa tunapewa muda maalumu wa kutumua ambao ukiisha huo muda lazima uombe tena. Muda huo unaweza kuwa miaka 33,66 na 99 na unapewa mkataba ambao unamasharti ya namna ya kutumia hiyo ardhi. Na mkataba huo ni HATI YA HAKI MILIKI(hati miliki).

Aidha,sheria zetu za ardhi zinataka watu wote watakaoondolewa kwenye ardhi zao ni lazima wapewe FIDIA na fidia hiyo ni lazima iwe ya haki,iwe kamilifu na ilipwe kwa wakati ndani ya miezi 6.

Hivyo basi,kwa ufupi nchini kwetu ardhi yako inaweza kuchukuliwa au ukahamishwa hilo eneo muda wowote hata kama umekaa muda mrefu ni takwa la kisheria. Pia utakapotakiwa kuondolewa kwenye ardhi yako ni lazima upewe FIDIA.

SUALA LA WAKAZI WA NGORONGORO.
Mjadala wa kuondolewa au kutoondolewa wakazi wa ngorongoro utakuwa wenye tija kama hatutaweka masuala ya uharakati,ukabila,upinzani na ushabiki.

Kwanza lazima tukumbuke kwamba mtu yoyote anaweza kuondolewa kwenye ardhi yake kama ni kwaajili ya manufaa ya umma.
Kwahiyo ndugu zetu wa ngorongoro wanaweza kuondolea ngorongoro kama ambavyo watanzania wengine mahali popote nchini wanaweza kuondolewa au wamewahi kuondolewa.

Kwahiyo suala la wao kuondolewa haliwezi kuwa mjadala kwasababu mtu yoyote kwenye nchii hii anaweza kuondolewa na ardhi yake ikapangiwa matumizi mengine yenye manufaa kwa umma.

Suala la kujadili ni je utaratibu wa wao kuondolewa umefuata sheria..? Je wamelipwa fidia..? Hiyo fidia ni ya haki..? Imelipwa kwa wakati..? Fidia inajitoshereza..? Haya ndiyo masuala ya kujadili na sio wao kuondolewa kwasababu wao ni kama watanzania wengine ambao wanaondolewa kwenye maeneo yao kupisha miradi ya maendeleo au uchumi.

Maswali ya mjadala.
1)Je sababu inayofanya wao kuondolewa ina manufaa kwa umma..?
2)Utaratibu wa wao kuondolewa umefata sheria..?

Hutakiwi kusema “wasiondolewe” kwasababu sheria inaruhusu watu kuondolewa. Wengine wanasema ile ni ardhi ya mababu zao. Je waliondolewa mahali pengine nchini sio ardhi ya mababu zao..? Utakuwa ni mjadala wa upendeleo.

Labda tulalamikie sheria inayoruhusu watu kuondolewa na inayo umpa rais mamlaka hayo na sio zoezi lenyewe.

Tunaweza kuomba upendeleo kwa serikali kutazama jambo hili kwa namna ya pekee ila sio kwa jicho la kisheria kwasababu sheria inaruhusu jambo hilo la wao kuondolewa, hata wakisema waende mahakamani hawawezi kupata ushindi.strictly application of rule of law will not give them favor but maybe the government should apply rule of fairness and respect .

Suala la serikali kuruhusu jambo hilo la kuhama ngorongoro kuwa la hiari ni jambo la busara kwasababu sheria inasema utwaaji wa ardhi ni wa lazima kama ni kwaajili ya manufaa ya umma.

Tunaweza kujadili sasa.karibu.

Imeandikwa na;
Thom Munkondya.
(Mpima ardhi,Mtalaamu na mshauri wa masuala ya ardhi).
0744336336.
IMG_4221.jpeg
 
Ikiwezekana kuwahamisha wazenji,wapemba na waunguja ili tutunze mazingira na kuhamasisha uwekezaji visiwani pia itakuwa sawa kuwahamisha wamasai wa ngorongoro.
 
Kama wanahamishwa kwa maslahi mapana ya taifa ni jambo jema, muhimu watengewa maeneo mapya mazuri ya kuishi na kufanyia shughuli zao za ufugaji
 
Mimi ni MTANGANYIKA, kura yangu ya Urais 2025 nitapiga KITANGANYIKA!
 
View attachment 3073525
Naona ID mpya fasta kuja kutetea unyang'anyi. Kwa hiyo Rais kajisikia kuuza ardhi ya Wamaasai?
 
Kwahiyo mpaka sasa maswala ya uhamisho wa wakazi wa ngorongoro yanafanyika kwa mujibu wa katiba (sheria).

Sasa chadema wanailakamikia nini serikali ikiwa wanao magwiji na wabobezi wa sheria mfano Mh. Lisu,Kibatala na n.k inamaana hili hawalijui?
 
Kama wanahamishwa kwa maslahi mapana ya taifa ni jambo jema, muhimu watengewa maeneo mapya mazuri ya kuishi na kufanyia shughuli zao za ufugaji
Wanahamishwa kwa maslahi manono ya watawala na maslahi makubwa ya Waarabu!
 
Back
Top Bottom