Je, ni Speed gani kubwa zaidi ushawahi kutembea na gari au pikipiki?

Ilikuwa natoka Kahama kwenda Nyakahura niende Bukoba, maeneo ya Ushirombo kuna mkeka safi sana no Tuta, no shimo hakuna mabuje barabarani (Asante STRABAG kwa kazi ile) nilitembea nikashtuka dashboard inasoma 200Km/H.

Gari ilikuwa ni Audi Q5

Ila sishauri mtu atembee huo mwendo. Maana lolote likitokea huwezi jitetea.
 
German machines huwa zina jeuri sana.
 
Tunapenda urojo baba wa kwenye misiba mkuu
 
Hakuna gx100, gx100 zote zina 1g-fe na zenye 1jz na 2jz ni jzx100 tena hiyo ya kwako sio kabisa maana zenye 1jz ni roulant edition ndo zina 1jz gte na hazipo hivyo kama hii yako, so yako inawezekana ni 1jz ge ni jzx100 ila non turbo
#HomeGarageTz
 
Nimesikitika sana kwa sisi waendesha baiskeli kutopewa nafasi ya kutoa shuhuda zetu za namna tunavyowanyanyasa barabarani wenye magari na pikipiki kwa spidi zetu kali
 
X5 50d yenye 400hp na 900 nm ina accelerate faster kuliko X5 50i yenye 550hp na 700nm?

Nina uzoefu na baadhi ya gari za diesel na petrol. Ninapokwambia torque ni kwenye milima na kubeba mizigo najua ninachosema.

Ndo nasikia kwako leo.
vp uzito au ukubwa wa body umeuzingatia ?
 
Hivi ukiendesha kwa "spidi kali sana" unapata faida gani?

Mimi nilijua wavuta bangi ndiyo hufanya hivyo, kumbe mpaka majitu mazima?
Kuna raha yake Mkuu, muhimu usilete rally na mtu mwingine
 
Nilienda 240 na BMW e30 Left Hand Drive, ile gari ya zamani ila mziki wake sio mdogo. Sikuwahi kurudia tena huo mchezo maana kidogo inizidi uwezo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…