Lavit
JF-Expert Member
- May 16, 2011
- 14,834
- 32,522
Ni record ambayo ni ngumu kuivunja, ni rekodi ya ubora katika utayarishaji wa muziki wa hapa nyumbani!! Kuwa na nyimbo zaidi ya 80% katika chatt za muziki si jambo rahisi kama wengine wanavyoweza kufikiri!! Ila kwa miaka kadhaa P funk majani aka Kinywele kimoja aliliweza hili!! Ilifika kipindi kila wimbo mzuri ukitoka wengi walisikika wakisema "Majani huyo", mara nyingi ilikuwa hivyo japo watayarishaji wengineo walikuwa wakifanya kazi nzuri pia!! Kuna ambao wanasema kwamba studio/watayarishaji walikuwa wachache na ndiyo maana ilikuwa rahisi Majani kung'ara.
Mimi sikubaliani na hii nadharia, maana watayarishaji waliokuwa wakijibiidisha walikuwa wengi sana, kwa uchache naweza kuwataja Bizman &Enrico(Soundcrafters), Master J (Mj records), Bonny luv (Mawingu Studio), Mika Mwamba, Rajabu marijani, Said Comoriery, KGT, Roy, Prof Ludigo na wengine wengi!! Ni Majani aliyefanya record za mwanzo kabisa za akina Juma Nature(Kighetogheto), Jay Moe (Majukumu), Prof J(Jina langu), SoloThang(Mambo ya pwani), Zay B (Gado remix), Mb Dog (Latifa), Mangwea (Gheto langu), TID (Zeze), Pig Black (Nini mnataka), Crtic(Mnizoee),Daz Baba (Namba 8), Starehe (Feruz), Pina (Mstari wa mbele), Mandojo na Domokaya(Nikupe nini),Afande Sele(Mayowe) na wengine wengi!!
Ni P funky ambaye ameweza kutengeneza beats na baadaye kutumika kwenye nyimbo nyingine na bado zikahit, uchache naweza taja beat ya wimbo wa Nitoke vipi wa Misosi ambayo baadaye ilikuja ilikuja kutumiwa na Man x katika kibao chake matata kilichojulikana kama "Nimechezea bahati", beat ya Promoter anabeep ya Prof J ilikuja kutumiwa tena na Ngwea katika "Napokea simu", vile vile beat ya Alikufa kwa ngoma baadaye aliitumia Dully Sykes katika I love My chicks"! P funky anakiri kupata ujuzi zaidi kwa kushirikiana na producers mbali mbali wa kipindi hicho kama Prof Ludigo, Bonny Luv na Master Jay! P funky amefanikiwa kunyakua tuzo ya utayarishaji bora wa muziki katika tuzo za Kili mwaka 2003, 2005 na 2006.
P funky pia ameweza kutengeneza kazi yake mwenyewe kama Ndani ya Club na Please Forgive me! Pia amefanya chorus kama "Yote maisha" ya Madee pia Famous ya Jmoe!!
NB; Kwa miaka ya sasa siuoni ule umahiri ya kipindi kile, sielewi tatizo liko wapi..pamoja na ushindani kuwa mkubwa ambao kwa vyovyote inabidi uongeze ufanisi lakini hali imekuwa tofauti sana!! Je unafikiri ni studio gani kwa sasa tunaweza ifananisha na Iliyokuwa Bongo Records ya kipindi kile!?