Je, ni ubora wa wasanii au umahiri wa Producer?

Lavit

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2011
Posts
14,834
Reaction score
32,522
Ni record ambayo ni ngumu kuivunja, ni rekodi ya ubora katika utayarishaji wa muziki wa hapa nyumbani!! Kuwa na nyimbo zaidi ya 80% katika chatt za muziki si jambo rahisi kama wengine wanavyoweza kufikiri!! Ila kwa miaka kadhaa P funk majani aka Kinywele kimoja aliliweza hili!! Ilifika kipindi kila wimbo mzuri ukitoka wengi walisikika wakisema "Majani huyo", mara nyingi ilikuwa hivyo japo watayarishaji wengineo walikuwa wakifanya kazi nzuri pia!! Kuna ambao wanasema kwamba studio/watayarishaji walikuwa wachache na ndiyo maana ilikuwa rahisi Majani kung'ara.

Mimi sikubaliani na hii nadharia, maana watayarishaji waliokuwa wakijibiidisha walikuwa wengi sana, kwa uchache naweza kuwataja Bizman &Enrico(Soundcrafters), Master J (Mj records), Bonny luv (Mawingu Studio), Mika Mwamba, Rajabu marijani, Said Comoriery, KGT, Roy, Prof Ludigo na wengine wengi!! Ni Majani aliyefanya record za mwanzo kabisa za akina Juma Nature(Kighetogheto), Jay Moe (Majukumu), Prof J(Jina langu), SoloThang(Mambo ya pwani), Zay B (Gado remix), Mb Dog (Latifa), Mangwea (Gheto langu), TID (Zeze), Pig Black (Nini mnataka), Crtic(Mnizoee),Daz Baba (Namba 8), Starehe (Feruz), Pina (Mstari wa mbele), Mandojo na Domokaya(Nikupe nini),Afande Sele(Mayowe) na wengine wengi!!

Ni P funky ambaye ameweza kutengeneza beats na baadaye kutumika kwenye nyimbo nyingine na bado zikahit, uchache naweza taja beat ya wimbo wa Nitoke vipi wa Misosi ambayo baadaye ilikuja ilikuja kutumiwa na Man x katika kibao chake matata kilichojulikana kama "Nimechezea bahati", beat ya Promoter anabeep ya Prof J ilikuja kutumiwa tena na Ngwea katika "Napokea simu", vile vile beat ya Alikufa kwa ngoma baadaye aliitumia Dully Sykes katika I love My chicks"! P funky anakiri kupata ujuzi zaidi kwa kushirikiana na producers mbali mbali wa kipindi hicho kama Prof Ludigo, Bonny Luv na Master Jay! P funky amefanikiwa kunyakua tuzo ya utayarishaji bora wa muziki katika tuzo za Kili mwaka 2003, 2005 na 2006.

P funky pia ameweza kutengeneza kazi yake mwenyewe kama Ndani ya Club na Please Forgive me! Pia amefanya chorus kama "Yote maisha" ya Madee pia Famous ya Jmoe!!

NB; Kwa miaka ya sasa siuoni ule umahiri ya kipindi kile, sielewi tatizo liko wapi..pamoja na ushindani kuwa mkubwa ambao kwa vyovyote inabidi uongeze ufanisi lakini hali imekuwa tofauti sana!! Je unafikiri ni studio gani kwa sasa tunaweza ifananisha na Iliyokuwa Bongo Records ya kipindi kile!?
 
Mi sijui ni kwann lakini namkubali sana Nahreel beat zake zinautofauti tofauti na wengine touches zao zinaingiliana vile
 
Mikono ya Majani ndio ilikua nyoko mzee yani ata ikigongwa beat bila vocal inakua hit tosha...

ufanyaji kazi muda mrefu ulifanya jamaa aamue kupumzika na sio yeye utamuona ata Master J aliamua kupumzika na kumuachia mikoba Marco Chali..
 
No one like majani ...mziki wasaivi beat zimejaa uwongo na janja nyingi nyingi ambazo wasanii wa kisasa hupenda ndio maana watu real kama kina majani inakuwa inaonekana kama kuna shida
Trust me majani ile ni kichwa ya beat ukisikiliza beat ya nitoke vipi ata bila kuimba mtu unaenjoy
 
Ni record ambayo ni ngumu kuivunja, ni rekodi ya ubora katika utayarishaji wa muziki wa hapa nyumbani!! Kuwa na nyimbo zaidi ya 80% katika chatt za muziki si jambo rahisi kama wengine wanavyoweza kufikiri!! Ila kwa miaka kadhaa P funk majani aka Kinywele kimoja aliliweza hili!! Ilifika kipindi kila wimbo mzuri ukitoka wengi walisikika wakisema "Majani huyo", mara nyingi ilikuwa hivyo japo watayarishaji wengineo walikuwa wakifanya kazi nzuri pia!! Kuna ambao wanasema kwamba studio/watayarishaji walikuwa wachache na ndiyo maana ilikuwa rahisi Majani kung'ara.

Mimi sikubaliani na hii nadharia, maana watayarishaji waliokuwa wakijibiidisha walikuwa wengi sana, kwa uchache naweza kuwataja Bizman &Enrico(Soundcrafters), Master J (Mj records), Bonny luv (Mawingu Studio), Mika Mwamba, Rajabu marijani, Said Comoriery, KGT, Roy, Prof Ludigo na wengine wengi!! Ni Majani aliyefanya record za mwanzo kabisa za akina Juma Nature(Kighetogheto), Jay Moe (Majukumu), Prof J(Jina langu), SoloThang(Mambo ya pwani), Zay B (Gado remix), Mb Dog (Latifa), Mangwea (Gheto langu), TID (Zeze), Pig Black (Nini mnataka), Crtic(Mnizoee),Daz Baba (Namba 8), Starehe (Feruz), Pina (Mstari wa mbele), Mandojo na Domokaya(Nikupe nini),Afande Sele(Mayowe) na wengine wengi!!

Ni P funky ambaye ameweza kutengeneza beats na baadaye kutumika kwenye nyimbo nyingine na bado zikahit, uchache naweza taja beat ya wimbo wa Nitoke vipi wa Misosi ambayo baadaye ilikuja ilikuja kutumiwa na Man x katika kibao chake matata kilichojulikana kama "Nimechezea bahati", beat ya Promoter anabeep ya Prof J ilikuja kutumiwa tena na Ngwea katika "Napokea simu", vile vile beat ya Alikufa kwa ngoma baadaye aliitumia Dully Sykes katika I love My chicks"! P funky anakiri kupata ujuzi zaidi kwa kushirikiana na producers mbali mbali wa kipindi hicho kama Prof Ludigo, Bonny Luv na Master Jay! P funky amefanikiwa kunyakua tuzo ya utayarishaji bora wa muziki katika tuzo za Kili mwaka 2003, 2005 na 2006.

P funky pia ameweza kutengeneza kazi yake mwenyewe kama Ndani ya Club na Please Forgive me! Pia amefanya chorus kama "Yote maisha" ya Madee pia Famous ya Jmoe!!

NB; Kwa miaka ya sasa siuoni ule umahiri ya kipindi kile, sielewi tatizo liko wapi..pamoja na ushindani kuwa mkubwa ambao kwa vyovyote inabidi uongeze ufanisi lakini hali imekuwa tofauti sana!! Je unafikiri ni studio gani kwa sasa tunaweza ifananisha na Iliyokuwa Bongo Records ya kipindi kile!?
Kuna siku nilimsikia akihojiwa, anasema zamani kulikuwa na maproducer ila sasa hv kuna ma-beats makers.
 
Wao walikuwa wanaumiza Vichwa zaidi ndomana kuna utofauti wa kazi za zamani na sasa.

Sa si waendelee kuumiza vichwa wakimbize gemu.,. why now wanakimbizwa na watu wasioumiza vichwa,.. Wao nyakati ziliwabeba, walkua wachache,kumiliki studio ilikua ghali,wanamziki walikua wanajielewa wanaimba vitu vya maana,..now ukiwa na compyuta na mic ghetto hio ni studio tayari.
 
Na ukiwa na Cherehani 4 ni kiwanda tayari hicho.
 
Sa si waendelee kuumiza vichwa wakimbize gemu.,. why now wanakimbizwa na watu wasioumiza vichwa,.. Wao nyakati ziliwabeba, walkua wachache,kumiliki studio ilikua ghali,wanamziki walikua wanajielewa wanaimba vitu vya maana,..now ukiwa na compyuta na mic ghetto hio ni studio tayari.
Yaani studio zimekuwa nyingi kama vibanda vya M-PESA
 
Back
Top Bottom