Je,ni UDOM pekee katika mashindano ya ICT kwa vyuo vya Tanzania?

Tanzanian kid

Member
Joined
Apr 1, 2025
Posts
98
Reaction score
168
Kuna jambo ambalo bado najiuliza kuhusu vyuo vyetu hapa Tanzania linapokuja suala la mashindano ya ICT. Maana naona vingi vipo kimya sana — ukiachana na UDOM (University of Dodoma).

Jana nilikuwa napiga stori na rafiki yangu wa SUA (Sokoine University of Agriculture) kuhusu masuala ya IT. Ni kama vile nilimkumbusha jambo, akafungua simu yake na kunionyesha short clip ikiwaonesha wanafunzi wa UDOM wameshinda katika mashindano ya ICT yaliyoandaliwa China chini ya kampuni ya Huawei. Sikutilia maanani sana kwa sababu kwangu hilo si jambo jipya — tayari nimeshawahi kuyaona mafanikio yao kwenye mashindano ya kitaifa kama Cyber Champions.

Lakini leo, katika pitapita zangu LinkedIn nikitafuta maarifa na fursa, nikakutana na post ya kijana mmoja akikabidhiwa zawadi. Awali nilitaka kuipita tu, lakini neno Ethical Hacking likanifanya nisimame kidogo. Nilipoisoma vizuri nikagundua kuwa alikuwa mwanafunzi wa UDOM — japo jina limenitoka — akikabidhiwa zawadi kutoka Vodacom, ambao ndio waandaaji wa tukio hilo.

Hapo ndipo swali likarudi tena kichwani:

Je, kwa Tanzania ni UDOM pekee wanaofanya vizuri kwenye masuala ya ICT?
Vyuo vingine viko wapi? Au hawana vyombo vya habari vya kuwaangazia? Au ni uzembe wangu binafsi katika kufuatilia?

Swali hili linanitesa kidogo...

Inawezekana kabisa kuna vipaji vikubwa katika vyuo kama IFM, DIT, UDSM, CBE, TIA, na vinginevyo. Lakini je, wanapewa nafasi ya kushiriki mashindano kama haya? Je, mashindano yanatangazwa kwa uwazi? Kuna juhudi za makusudi za kuandaa timu za kuwakilisha vyuo hivi kwenye masuala ya teknolojia kama AI, cybersecurity, software development, robotics, networking, na kadhalika?

Na kama kweli ni UDOM pekee wanaoonekana wakilipeperusha vema bendera ya taifa kwenye jukwaa la teknolojia, basi kuna jambo wanalo wamefanikiwa kulifanya tofauti.

Na sisi wengine tunasubiri nini?
 
Hivi MUST haipo kweli kwenye list ya vyuo vyenye wanafunzi wazuri wa IT ?
 
T

Taarifa wanapata vizuri sana sema kuna michujo vyuo vingi vinatoka hatua za awali sana CIVE wako serious wao wenyewe wana competitions za hapo hapo chuoni
 
Jalalani wanafundishwa kukariri masomo ya IT ndio maana weupe.....
 
  • Kicheko
Reactions: al1
T

Taarifa wanapata vizuri sana sema kuna michujo vyuo vingi vinatoka hatua za awali sana CIVE wako serious wao wenyewe wana competitions za hapo hapo chuoni
Hapa sasa umenifungua bro,ahsante sana
 
Hapa sasa umenifungua bro,ahsante sana
Ndo hivo waache visingizio competitions zinaarika vyuo vyote washiriki ila unakuta chuo hakina mwamuko wa mambo ya tehama wanakimbizana na assignment tu wapate vyeti ila UDOM - CIVE wao wenyewe wanajiandalia mashindano yao na kujiweka tyr kwa mda wote.
 
Chuo cha Kata,
Kumbe ulisomea IT jalalani hao hawapatagi kazi za IT hasa makampuni binafsi yenye hela ndefu
Hasira za nn msomi kutoka chuo cha kata, wengi wako mtaani wana mbwela mbwela tyuuh.
😂😂😂😂😂😂
 
MUDA utafika UD huenda isisikike kabisa kwenye soko.
 
UDOM kwenye issue ya ICT kwa ujumla wamejidhatiti kuanzia Vifaa(wana vifaa vya kisasa), Mazingira na kila kitu lakini pia wako kipractical zaidi.

Katika tasnia hii vyuo vingine vijipange. Nahisi wameamua ku specialize katika tasnia hiyo.
 
Back
Top Bottom